Uhusiano wangu na baba yangu

Ninachokiona kutoka kwako ni u much know mwingi kwenye fuvu lako. Hizi dini za kuja zinawapogusha Sana vijana na kuona wachungaji na wazee wa kanisa ndio Wazazi wenu. Nina uhakika kuwa Richa ya kuwa umeenda mpaka chuo lakini maisha Yako hayana Amani kisa ujuaji na kukosa ndugu. Baba Yako amekuvumilia Sana licha ya dharau zako unazomuonesha

Sasa dogo, nenda Kwa ndugu ukaombe msamaha na useme kuwa ulimkosea baba Yako. Mpaka Sasa niamini Mimi ya kuwa umeunganishwa na mama Yako. Yaani wanakuona kuwa wewe na mama Yako lenu ni Moja na wanahisi labda mama alikuonesha baba mwingine. Ili kuyaepuka haya na mengine kubali yaishe.
 
Pole, kwakua tayari unafamilia yako, kama unaweza jaribu kuona kama mnaweza kuyamaliza na mzee, maisha haya mafupi sana, ouwekeana vinyongo sio poa
Sasa masharti ya kwenda kuungama makaburini ya nini zama hizi?
 
Well said. Mimi binafsi nimemueleza mengi hapo juu. Hawa watoto wanapenda sn kuleta ligi hata kwa wazazi wao kwa kuokota ushauri kutoka kwa wenzao waliokwisha shindikana kwa wazazi wao.

Nimekukubali sn kwa ushauri uliompa. Kumbe vijana wenye akili bado mpo nilidhani wamebaki wahuni tu na mashoga kumbe wenye busara bado mpo. Cha ajabu utaona anadharau ushauri wako anachukuwa wa wale wanaomwambia aachane na huyo baba yake yeye akomae kivyake na maisha yake.
 
Ushauri mzuri.
 
Akili na umri mkubwa(>80yrs) huwa viko vice versa.
 
Huna tatizo lolote wewe focus na maisha yako ila usiache kumhudumia mzee nyumbani, hakikisha unamrushia kitu kidogo ale na ma' mdogo ajue huna shida naye.
Hapana huyo mama ni mshrikina na ndio anawakoroga ogopa wanao ingilia mambo ya watu
 
Pole kwanza kwa kupitia hiyo experience ambayo si ya kawaida kwa jamii zetu za kiafrika, yaani mzazi kuweka kisasi na mtoto ni jambo la ajabu kama sio nadra kulisikia na tena ukilisikia basi ni mtoto mtukutu asiye na adabu ambae hasikii na ni mkaidi na viburi juu ndipo mzazi hufanya kubwaga manyanga na kumsusa kama sio kumkana kama sehemu ya uzao wake sababu ya kukosa utii na mwenendo mzuri.

Lakini hili lako ni la tofauti na inashangaza sana tena sana eti baba mzazi kumsusia mtoto wake wa kiume kwasababu ameamua kuwa na maisha na maamuzi yake binafsi. Na mbaya zaidi anafikia hatua ya kukugombanisha na ndugu zako wa familia moja na mbaya zaidi anakuongelea mbovu.

Kumradhi kama nitakuwa nimekukera na kauli yangu ila ukweli ni kuwa hapo hauna baba, bali huyo ni mtu ambaye amejitolea kutoa mbegu zake ili wewe uzaliwe.

Baba huwa ni kiongozi rafiki ambaye bila kujali mazingira ni yapi ila haitatokea yeye aharibu mahusiano na mtoto wake kwa sababu yoyote ile na siku zote anabakia kuwa kiongozi na mshauri namba moja kwa mtoto. Huyu uliyenae ni kinyume cha Baba bali ni msela aliyekulea.

Usivunjike moyo, kujisikia vibaya wala kuhisi umepotea njia. Ungekuwa mtu mwenye matatizo usingeweza kuishi vizuri na watu baki hadi wakakusaidia nyakati ngumu za msiba ambapo yule unayemtambua kama baba mzazi ameamua kukuletea upinzani usio na mbele wala nyuma na mbaya zaidi analeta udwanzi wake kwenye swala ambalo hata watu baki wasingeweza kukutenga.

Upo sahihi, hii utaweza kuipima kwa namna umeweza kuishi vema na jamii iliyokuzunguka mbali na familia uliyotokea. Ndugu ni kufaana sio kufanana. Chukua glass ya maji kunywa shusha pumzi. Then futa mawazo ya majuto kuwa kuna mzazi umemkwaza. Muache aishi hayo maisha ya chuki na uhasama hadi uzeeni mwake.

Endelea kujijenga kijamii na watu waliokuzunguka na shirikiana nao vema hao hao kwenye hali na mali. Mzazi wako pia ni binadamu. Wanadamu huwa na visirani vya ajabu nyakati zingine hadi unajiuliza imekuwaje mtu anakuwa na mambo ya ajabu kiasi hicho. Sasa ukiendelea kumstaajabu utaona kama Dunia inakuelemea. Ila ukimpuuza na kumuona mwehu tu then upuuzi wake wowote anaofanya hautakudhuru wala kukuumiza.

Chukulia kama tayari ulishamzika huyo anaekusumbua ni mtu baki au baba mdogo. Unafanya vema sana kumkalia mbali na kumpotezea hii inakujenga kuishi bila kero zake na kujipanga kivyako. Na huo ndio uanaume. Wanasema utaachana na baba na mama yako utashika Tecno yako mkononi utaenda uraini kupambana ukitafuta maisha.

Endelea kujenga ukoo wako na uhakikishe hicho kirusi cha tabia mbovu ya baba yako hakitakuja jirudia kujipandikiza katika uzao wako milele.

Yangu ni hayo tu naomba kuwasilisha.
 
Pole, kwakua tayari unafamilia yako, kama unaweza jaribu kuona kama mnaweza kuyamaliza na mzee, maisha haya mafupi sana, ouwekeana vinyongo sio poa
Umesoma lakini alichokiandika au umetoa tu ushauri boss?
 
Haukusoma alipoandika kuwa siku ya msiba wa bibi yake waligoma kuzika hadi yeye na baba yake waombane msamaha na mzee wake akasema yaishe. Then mzee wake akaliwasha tena ? Kuna wazazi ukiwaendekeza hautafanya maisha yako.

Usiombe haya yakukute unatamani urudishe siku nyuma uombe kubadilishiwa mzazi wa kukuleta duniani.

Haya anayofanya huyu mzee ni mwiko tena marufuku kabisa kwa mzazi kumfanya mtoto wako asotee kupata maelewano na wewe mzazi wake.

Mtoto hanaga ujanja kwa mzazi sasa ni ujinga kwa mzazi kuanza kumtesa mtoto.
 
Ona sasa, mzee anaruka na beki tatu. Na anafamilia. Hivi anajielewa kweli huyu mzee?

Inaonekana ukoo wa baba yako ni changamoto, jiweke nao mbali hivyo hivyo, hawana maajabu hao na hakuna kitu watakufanya.
 
Dahhh umeongea kama Baba

Embu amsikilize huyo mama.
Your browser is not able to display this video.
 
Huu sio ushauri mzuri hata kidogo na sitoshauri muhusika aufanyie kazi.

Hii mifumo ya kikoloni ya kuwapa wazazi u'Mungu mtu hata pale pasipostahili imepelekea kuvuruga vijana wengi sana kuishi maisha nje ya rada zao.

Sasa wewe unataka nambia huyu kijana hana maisha yake kwasasa?!

Kwann baba yake atake kijana wake awe polisi ya lazima?! Ndio maana tuna askari wasiotendea haki hii kazi halafu tunawalaumu kumbe ni matokeo ya kuwa na mitazamo kama hii ya kutii wazazi hata pale isipostahili kuwapa utii.

Mzazi anapewa hadhi ya MUNGU wa pili Duniani endapo atakuwa ni mtu wa hekima, subira, upendo, kiongozi, mshauri na msimamizi mzuri kwa kijana au binti yake.

Sio mzazi analeta bangi wewe unasema mtu ahangaike nae. Mtu kama hakukua vizuri au amelelewa makuzi yankudeka deka ndio iwe haki yeye kusumbua wengine eti kisa ni mtoto wake, THAT'S NONSENSE TOP MOST.

Ingekuwa huyo mzazi yupo sahihi basi huyo kijana asingekuwa na maisha. Mtu kapotea miaka 5 yote na ana maisha yake mazuri tu shida ni nini sasa.
 
Naomba unisaidie. Katika huo msamaha anatakiwa kusema maneno gani?!

"Baba naomba unisamehe kwa kukataa upolisi" au anasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…