Nikikwambia ukweli utasema dada yako nakudanganya.
Sisi tuliojilipia ada shule kwa kukosa mikopo ndo tulitoka salama chuo hao watoto wa loan board uwasamehe boom likiisha wana njaa sana.
Nakumbuka kila mtu alikuwa akijiuliza mpz wangu ni nani mpaka nilimaliza bila kuwa na mahusiano chuo hiyo yote nilikuwa busy na biashara hata kuliko masomo so vijipesa vya kula sikuvikosa.
Sasa wewe mdogo wangu kwa umri huo kweli unaweza muhudumia msichana wa chuo na walivyo na tamaa?
Huyo kapata bwana wa mitaani na vigari vyako kama baby Walker ndo anamuweka mjini.
Wewe mdogo wangu upo unapambana ujenge kama sio kununua kiwanja. Mwenzio anahitaji wa kumpeleka shopping
Dear mdogo wangu achana na wasichana wa chuo.date msichana ambae ashatoka chuo, hao wengi wanataka ndoa na sio starehe.
Ukimsamehe huyo dada mkarudiana utakuja kulia sana.unajisikiaje eti mtoto mdogo hivyo ashatoa mimba?
Tafuta kwanza pesa wanawake wako wengi
Na usinambie kuwa pesa unayo, kwa umri wako bado unatafuta una vishiling vya kula na kuendesha maisha yako ila sio vya kumpa mwanamke.
Hata kama unatokea familiya tajiri hivyo vi pesa unatoa kwenu.
Ukifikisha miaka 30 anza kutafuta mke wa ndoa kwa sasa play safe. Tafuta pesa usisahau kutumia condom utabambikiziwa mtoto.