Magufuli kwenye Corona alichezaga Kama pele wallah
Ngojea wafia vyama wakuvamie ,ila ndio ukweli wenyewe.UK walipo tangaza vuguvugu la tatu na kuamua watu wakae ndani ndipo maandamano yalianzia hapo.
Kenya na waonea huruma nchi mwaka jana umekumbwa na ukame,nzige na mafuriko ,wakaamua kuiga Kunya kwa tembo,huku vipuru vyao vidogo sasa hivi wanaugulia maumivu nao wanaandamana hawataki Lockdown.
Chanjo zenyewe za Corona nazo hazi eleweki kwa mujibu wa BBC baadhi ya wauguzi Kenya wengi wao,wamekataa kuchoma chanjo.Ujerumani kasitisha kwa muda matumizi ya Astrazaneca kwa walio chini ya miaka 60 sababu ya baadhi yao wanaochoma damu zinaganda.
Juzi CCN wamesema chanjo ya Pfizer inaisha nguvu baada ya miezi sita,leo tu wametangaza huko UK watu 30 kati ya mil 18 waliochoma chanjo ya AstraZaneca damu zimeganda na hapo hatujui effects ya hiyo chanjo siku za mbele ,so ukitizama kwenye chanjo kuna vurugu na sarakasi nyingi sana.
Ugonjwa wenyewe unasiasa za kimagharibi zimeingia, WHO alichelewa kuapprove chanjo ya Russia na Dr Fauci wa US anaiponda chanjo ya Russia haina ufanisi.
Hizi chanjo ni kuzisikilizia kama alivyosema Magu,huku ukifuatilia na baadaye ukipata uhakika ndipo tuamue tutumie ipi.