Wahenga wanasema; "mshikwa na ngozi ndiye mla nyama"
"Ngozi" ya utumwa, ubaguzi, unyanyasaji nk, ipo Caribbean, Marekani, Ulaya (Uingereza, Ufaransa nk ). Wengi wanaofanyiwa hayo madhila ni "lineage" ya Utumwa, katika Uarabuni hiyo lineage ya Utumwa haipo kabisa ni sawa na kusema " ushahidi umepotezwa" au jalada la kesi halionekani, Waafrika wengi waliopo Uarabuni ni wahamiaji na sio zao la utumwa hata kama watanyanyaswa wataambiwa huko ulifuata nini??? au ataambiwa; si shida yako iliyokupekeka huko!!.
Katika nchi za Asia ni angalau India tu ndiyo kuna masalia ya Watumwa (Sidis) huko Karnataka waliotoka Kenya.