Ni ngumu sana kuwaelewa hawa watu.
1. Wanakununua na kukuuza, wakiona biashara imekua ghali kuiendesha wanaanzisha kampeni ya kuipinga. Mpiga zumari kwenye kampeni husika anakua ni muathirika wa biashara ya utumwa.
GHAFLA MZUNGU ANAANZA KUSIFIWA KWA KUPINGA BIASHARA ALIYOKUA AKIIFANYA. Wanaomsifu ni miongoni wa WATUMWA.🎓
2. Anakuja nchini kwako kiharamia, anajichimbia na kuanza kukubagua ndani ya nchi yako! Badala ya kupambana kumtoa unaanza mapambano asikubague😁Akishathibitisha kuwa umeshapoteza kumbukumbu za uhalali wake kuwa nchini kwako anatengeneza magitaa, vinubi na matari kisha anazisha kamoeni ya kupinga UBAGUZI WA RANGI. Mwongoza kampeni anakuwa mzawa mwathirika wa uvamizi wa maharamia na kisha ubaguzi wa rangi.
Hatima ya kampeni ANASIFIWA MZUNGU MVAMIZI na anajipatiamo uhalali wa kumiliki na kutawala sawasawa na wazawa.
HUYO NDIO MUZUNGU.