Umenena fact sana mkuu ...kumsingizia nyerere kwa kila kitu kwa sasa ni hoja zaifu mno....hayo mambo yalishapita tunafanya nn sasa ndo jambo la msingi zaidi....Hivi mpaka leo bado tuna hangover ya vita ya Kagera. Inahitaji miaka mingapi kubadili uchumi wa nchi?. Nadhani adui mkubwa wa uchumi wetu ni Ufisaidi na kutokujali:
1. Huduma mbovu ya maji
2. Umeme kukatikakatika
3. Kuachilua rasilimali zetu kuchukuliwa kiholela
Na mengine mengi.
Ukweli hatujapata viongozi wenye maono. Tuache kumsingizia Nyerere. Tuache udhaifu
Kuna nchi kama saba hivi pamoja na kuwa kwenye jumuiya ya nchi za Ulaya (EU) lakini hazitumii sarafu ya Euro na badala yake zinatumia tu sarafu zao.Ungezitaja ingekuwa njema sana.
Hahahahahaha
Sio kweli labda mwaka 1978 ulikuwa hujazaliwa au ulikuwa mtoto mdogo sana. Uchumi wa Tanzania ulianza kuyumba baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 lkn baada ya vita 1979 ndio ukafa kabisa hadi leo.