Uingereza: Waziri Mkuu apigwa faini na Polisi kwa kutofunga mkanda wa Kiti akiwa ndani ya gari

Uingereza: Waziri Mkuu apigwa faini na Polisi kwa kutofunga mkanda wa Kiti akiwa ndani ya gari

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni Rish Sunak wa Uingereza

Source: Sky news

Hii kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla haiwezekani

----

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amepigwa faini kwa kutofunga mkanda kwenye gari lililokuwa likitembea wakati akirekodi video kwa ajili ya mitandao ya kijamii.

Polisi wa Lancashire wamesema kuwa wamempa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 42, adhabu ya kulipa faini isiyobadilika masharti.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kwamba Sunak amekubali kuwa hilo lilikuwa kosa na ameomba radhi na kuongeza kuwa atalipa faini hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Propaganda hizo hata huko pia haiwezekani labda kama wanataka kufanya show kama hivyo ili kuwadanganya watu, Malkia Elizabeth hajawahi kufunga mkanda na wala hakuwahi kuwa na leseni ya udereva na alikuwa anaendesha gari!
 
ha ha....Baniani huyo.
Hata hivyo haujasema kama alikuwa katika gari lake binafsi au la Kazi.

Wacha hizooo

Unafiki tuu
 
Ni Rish Sunak wa Uingereza

Source: Sky news

Hii kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla haiwezekani
Hata Huko kwa Ma-Komunist China na Ma-Fashisti Urusi hiyo kitu hajwezekani. Huko China na Urusi Marais wanaabudiwa Kama miungu watu.Hawana tofauti na Afrika kimfumo.
 
Propaganda hizo hata huko pia haiwezekani labda kama wanataka kufanya show kama hivyo ili kuwadanganya watu, Malkia Elizabeth hajawahi kufunga mkanda na wala hakuwahi na leseni ya udereva na alikuwa anaedesha gari!
Nyie kila kitu proganda yani mpo negative always khaa!!!
 
Back
Top Bottom