Uingereza yasikitishwa na yaliyotokea kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa nchini Tanzania

Uingereza yasikitishwa na yaliyotokea kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa nchini Tanzania

Wao ni nani kivipi? Kila mtu na nchi yake.
Kama asilimia kubwa ya Watanzania wameridhika wao ndo waje kutudanganya tuna shida?
Wajishughulikie kwanza huko wasiwashwe na yasiyowahusu.
Ni kweli hujui wao ni nani?
Hiyo asilimia kubwa ya watz walioridhika ni CCM, hilo nakubaliana na wewe 100%.
 
Nchi yangu isidharau haya matamko ya hawa watu wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu 2020. Hawa watu huenda kuna kitu, wanatuandaa kisaikolojia. Siamini tu kwamba wanaongea hivyo alafu wanaishia hapo, anyway muda ni mwalimu mzuri
Marekani alishamtolea matamko mengi sana hata Museven, nadhani sasa hivi yatakuwa yamejaa file zima, lkn Museven bado anadunda tu pale Uganda.

Point yangu ni kwamba Tanzania haijawa na haitakuwa na hali mbaya kuzidi Uganda.
 
Watanzania mkiwa nafkira kwamba mapambano ya demokurasia nchini yatafanywa na nchi za Ulaya na Marikani naona kama hiyo ni dhana potofu......kabla ya uingereza kusikitika nyie mmefanya nini kupambana na hiyo hali?
Msimu wa mvua huuu tupo shambani. Demokrasia tumewaachia nyie wa mjini muitafute na mkiipata mtujulishe
 
Naona hata angesema JPM ni rais wa Tz bado ungemwona muongo. Hayo aliyosema yalifanyika mchana kweupe! Uongo wake ni upi?
Embu soma vizuri alichoandika tena huyo bibi analaumu serikari kwa kuondoa wagombea ambao wote walirudishwa.

Analaumu serikari kwa maamuzi ya upinzani kujitoa, hata baada ya kubembelezwa mbele ya dunia.

Inawezekana huyu mama kachoka kuishi Tanzania anatafuta sababu za kutunga aichokoze serikari arudishwe kwao kama anavyotaka.

Maana hakuna la maana analoongea.

Kama ana ku-miss kwao atume tweet kushiriki mjadala unaondelea huko chief Rabbi amemponda kiongozi wa labour kwa madai ya anti semitism swala ambalo limewakera Jewish community wanao support labour na sehemu kubwa ya jamii kwa kuingiza dini kwenye siasa

Lakini kwa hili la uchaguzi ukisoma hayo malalamiko yake apeleke ushahidi ni kituo gani kilikuwa hakina majina ya wagombea wa vyama vingine na kwa vipi serikari inahusika wapinzani kugoma wakati wametumia muda kweli kuwabembeleza. Sasa kama anao ushahidi mwingine alete.
 
Msimu wa mvua huuu tupo shambani. Demokrasia tumewaachia nyie wa mjini muitafute na mkiipata mtujulishe
Hahaha .....mkuu ila bila demokurasia na utawala washaria nchini hata hivyo utakavyo vuna vitakosa soko huru unaweza ukanyagnywa na usilipye.....kwa hiyo utawala bora na demokurasia nimuhimu kwa kila sekita nchini
 
Waziri wa mambo ya nje ana kazi kubwa!! maana haya mataifa huwezi kuyapa masa 24 yafungashe virango, huwezi kabisa.
 
Embu soma vizuri alichoandika tena huyo bibi analaumu serikari kwa kuondoa wagombea ambao wote walirudishwa.

Analaumu serikari kwa maamuzi ya upinzani kujitoa, hata baada ya kubembelezwa mbele ya dunia.

Inawezekana huyu mama kachoka kuishi Tanzania anatafuta sababu za kutunga aichokoze serikari arudishwe kwao.

Maana hakuna la maana analoongea.

Kama ana ku-miss kwao atume tweet kushirika mjadala unaondelea huko chief Rabbi amemponda kiongozi wa labour kwa madai ya anti semitism politics swala ambalo limewakera Jewish community wanao support labours na jamii kwa kuingiza dini kwenye siasa.

Lakini kwa hili la uchaguzi ukisoma hayo malalamiko yake apeleke ushahidi ni kituo gani kilikuwa hakina majina ya wagon bra wa vyama vingine na kwa vipi serikari inahusika wapinzani kugoma wakati wametumia muda kweli kuwabembeleza. Sasa kama anao ushahidi mwingine alete.
Mkuu sote tupo hapa Tz tusijifanye hatujui kilichotokea kwenye huu uchaguzi.
 
Huyu sasa ndio wakuitwa atuelezee mgombea yupi alikuwa disqualified.
balozi wa Uingeleza haitwi kienyeji enyeji kama unavyofikiri - hapo Wizara lazima itoe maelezo ya kina. ...hivi ndiyo viashiria kuelekea 2020
 
View attachment 1274916

Kitendo cha Watendaji kuamriwa kujificha kwa gharama yoyote ile ili kuhakikisha Wagombea wa vyama vya upinzani hawachukui ama kurudisha fomu za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa lengo la kuwabeba wagombea wa CCM kwa mbeleko ya chuma, kimeusikitisha mno ubalozi wa Uingereza.

My take: Nchi inazidi kudhalilika kwenye jumuiya ya Kimataifa
Mku mkumbushe balozi atoe tamko pia kwa figisu za rafiki yake huko Marekani maana inaonekana na huko uchaguzi una figisu figisu hadi mpaka sasa wanafikishana kujadili Kwenye Bunge na congress mchezo wa Bwana mkubwa Marekani kuwatolea nje wapinzani wake ili wakose sifa za kugombea. Hapo tutajua anayo fair play. Ukiona tangazo lake nibip.
 
balozi wa Uingeleza haitwi kienyeji enyeji kama unavyofikiri - hapo Wizara lazima itoe maelezo ya kina. ...hivi ndiyo viashiria kuelekea 2020
Whatever the process huyu mama anatakiwa alete ushahidi wa hoja zake sio kuropoka ovyo.
 
Mkuu sote tupo hapa Tz tusijifanye hatujui kilichotokea kwenye huu uchaguzi.
Liko wazi upinzani umeanza tabia za kitoto kutaka kubembelezwa kushiriki kwenye misingi ya demokrasia.

Hakuna mwenye huo muda nao
 
Haya ni manyunyu mkuu naomba udiyapuuze, amini nikuambiayo kuwa nchi zote za Ulaya zitatoa kauli kama hii, sasa sikilizia 2020.
Hawa ni watu makini sana, haya matukio yataunganishwa na mengine ndipo wachukue hatua.
Nchi yangu nzuri inaelekea kubaya Mungu atunusuru.
Wataishia kusikitika la kufanya hakuna juzi marekani leo uingereza kesho canada au pakistani
 
Mkuu ndivyo nilivyosema, tuendako tusipobadilika tutaaibika
Nchi yangu isidharau haya matamko ya hawa watu wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu 2020. Hawa watu huenda kuna kitu, wanatuandaa kisaikolojia. Siamini tu kwamba wanaongea hivyo alafu wanaishia hapo, anyway muda ni mwalimu mzuri
 
Back
Top Bottom