Uingereza yatuma kikosi maalum cha makomandoo wa SAS Msumbiji kumuokoa raia wao aliyetekwa

Uingereza yatuma kikosi maalum cha makomandoo wa SAS Msumbiji kumuokoa raia wao aliyetekwa

Kusingetulia tungesikia hali iliyopo Msumbiji..we unaona hali ilitokuwepo sasa? Na hawa wa kibiti je jmewasikia?? Hao ndo walikua wafuasi wa Rogo
Kwahiyo kifo cha rogo hakijasaidia kitu, ukute wangemwacha hai na kumwelimisha nae angeelimisha wanafunzi/wafuasi wake
 
Hawa wavaa vipedo pusha si wa kuwadekeza, mkiwadekeza matokeo yake ndio haya.
Hao makomando watatu wako vizuri kiasi Cha kukwepa risasi?
SAS maana yake ni Special Air Service huja kwa ndege maalum wakadondoshwa mahala wakiachwa wakatekeleze kazi.

Kazi zao ni pamoja na kupambana ugaidi, magaidi pamoja na uokozi wa mateka.

Shughuli zao huwa ni siri au "classified" na wakiingia kazini wanakuwa wamepewa "go ahead" na serikali ya Uingereza na wizara ya ulinzi wa nchi hiyo.

SAS wana idara nyingi na huenda idara maalum ya majini yaani Boat Troops ambayo hutumia mitumbwi na ile ya kujaza upepo pamoja na uzamiaji na uibukaji pembezoni mwa bahati ndo walotumwa kwa kazi hiyo.
 
Kila kwenye mafuta na gesi Africa lazima kuwe na uwasi hata Tz tungecheza kidogo yangetukuta najiuliza makomando watatu wakaokoe mtu mmoja kwenye kundi la waasi ambao wameshikilia miji na mitaa msumbujii kama sio wao wenyewe kwenda kutoa mafunzo kwa magaid na ushaambiwa wao ni walimu wa" bush welfare"pia cha ajabu kampuni Total bado inafunga mitambo yake bila shida yn utaniutani msumbujii ndio bc tn
Hawa watatu wamekwenda kuongeza nguvu katika big operation.
 
Nadhani bado SADC haijaweza kuunda kikosi maalum cha hizo operations.

Hata hivyo jukumu hilo ni la AU.
Hiyo akili haipo, watauzana tu. Africa bado tuna shida sana.. mfano mwepesi UGANDA , RWANDA na CONGO
SAS maana yake ni Special Air Service huja kwa ndege maalum wakadondoshwa mahala wakiachwe wakatekeleze kazi.

Kazi zao ni pamoja na kupambana ugaidi, magaidi pamoja na uokozi wa mateka.

Shughuli zao huwa ni siri au "classified" na wakiingia kazini wanakuwa wamepewa "go ahead" na serikali ya Uingereza na wizara ya ulinzi wa nchi hiyo.

SAS wana idara nyingi na huenda idara maalum ya majini yaani Boat Troops ambayo hutumia mitumbwi na ile ya kujaza upepo pamoja na uzamiaji na uibukaji pembezoni mwa bahati ndo walotumwa kwa kazi hiyo.
SAS wanamwagiwa sana sifa. Huenda wakamaliza tatizo kama hawachezi na akili zetu, maama hiyo matukio yote huenda wao na tamaa zao za mafuta ndio wanaleta baraaa. Mzungu mtu wa ajabu sana. Ila hao watatu hawana suport ?
 
makomandoo watatu mpaka nimejikuta nacheka. asset tatu sawa na matrafiki 312 wa TZ. komandoo mmoja full equipd 62 mil tSH. jumlisha training sio watu hao ni mashine. makomandoo wetu tuache kuwavunjisha matofali na mafimbo. wao sio wanamazingaumbwe.
Katika makuruta 200 wakianza kuchujwa hubakia kama 30 hivi, hivyo ni asilimia 15 hadi 20 hivi.
 
Yani kumbe hao waasi wanauwa watu maeneo hayohayo na kazi za uchimbaji mafuta na mitambo inaendelea kufungwa lakini hawa leti madhara kwenye hayo makampuni?????.

Kweli wazungu sio wajombazetu.
Mkuu hao ndiyo walinzi wa mradi!
Hao makomando wa Uingereza walikuwa Nairobi wakifundisha sijui kina nani vita ya msituni. Wakati wao Waingereza kwao hakuna misitu.

Tabia ya Beberu ni kujirushia mkojo wake!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hiyo akili haipo, watauzana tu. Africa bado tuna shida sana.. mfano mwepesi UGANDA , RWANDA na CONGO

SAS wanamwagiwa sana sifa. Huenda wakamaliza tatizo kama hawachezi na akili zetu, maama hiyo matukio yote huenda wao na tamaa zao za mafuta ndio wanaleta baraaa. Mzungu mtu wa ajabu sana. Ila hao watatu hawana suport ?
Mkuu, tukianza kuongelea hawa jamaa itachukua muda sana.

Hivi wafahamu kuwa hawa huweza kuingia katika nchi kama watalii na kukaa kuleee mbugani.

Huko huweza kutuma drone ikazunguka Mererani yote na kutuma picha makao makuu bila hata mtu kutambua?

Ogopa sana hawa watu.

?
 
Uingereza imetuma makomandoo watatu wa SAS kwenda nchini Msumbiji kusaidia kumuokoa raia wa nchi hiyo bwana Phillip Mawer ambae ametekwa na kikundi cha kigaidi cha ISIS.

Gazeti la The Times la Uingereza limeripoti kuwa makomandoo hao watatu wanatoka katika kambi ya jeshi la Uingereza iliyoko mjini Nairobi nchini Kenya ambayo pia hutoa mafunzo ya vita ya msituni au "Bush Warfare".

Majeshi maalum ya Marekani tayari yapo nchini humo yakitoa mafunzo maalum kwa makomandoo wa Msumbiji.

Raia huyo pamoja na raia wengine wa nchi hiyo walikuwa wakijaribu kukimbia mji wa Palma ambao ulivamiwa na kikundi hicho cha ISIS ambacho baadae kilitoa taarifa ya kuthibitisha mashambulizi yake kupitia kituo chake cha habari cha Amaq.

Bwana Mawer ni mhandisi aliekuwa akifanya kazi katika kampuni ya RA yenye makazi yake Dubai na hujishughulisha na kazi za ugavi na makazi ya muda kwa wataalam mbalimbali wanofanya kazi nchini Msumbiji.

Pia bwana Mawer alikuwa akisaidia kufunga mitambo ya mafuta ya kampuni ya Total ya Ufaransa katika mji wa Palma ambao upo mpakani kabisa na Tanzania pamoja na mji mwingine wa Mocimboa da Praia ambayo ipo ndani ya jimbo la Cado Delgado ambalo mji mkuu wake waitwa Pemba.

Gazeti la Daily Teleghraph pia linaripoti kuwa kikundi hicho cha ISIS kilifanya shambulizi lake siku ya jumatatu huku magaidi wakitokea pande tatu tofauti na baadae wakatangaza kupitia ujumbe wa mtandao wa Telegram kuwa wamefanya shambulizi hilo na mji wa Palma uko chini ya himaya yao.

Watu saba waliuawa akiwemo raia mmoja wa Uingereza walipokuwa wakikimbia kutoka hoteli ya Amarula walokuwa wakitumia kwa makazi ana ambayo ipo karibu kabisa na mradi wa gesi wa Total.

Kikundi cha ISIS nchini Msumbiji kilianza kushamiri kuanzia mwaka 2015 kikitumia jina la Ansar al- Sunna sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo kikifuata itikadi za Aboud Rogo Mohammed ambae hutba zake ziliwagusa vijana wasio na ajira katika eneo lenye wingi wa gesi ya mafuta.

Baadae kikundi hichi kikaanza kujenga shule za madrasa pamoja na misikiti kiasi cha kuwavuta wenyeji wengi walokuwa wakiishi katika eneo hilo.

Mwaka 2017 kikundi hicho kikaanza kufanya mashambulizi wakitumia jina la Al shabab wa Somalia ingawa hawakuwa na uhusiano wowote na kiongozi wa kikundi hicho.

Baadae kikundi hicho kikaanza kutuma picha katika mtandao wa Telegram kikionyesha picha zenye alama za ISIS wapiganaji wake wakiwa wamebeba bendera za ISIS huku wakilitaja jina la kiongozi wa kikundi hicho Abu Bakr al Baghdadi.

Baadae ISIS makao makuu wakatoa taarifa kuwa kikundi hicho cha Msumbiji kimeingzwa rasmi katika jimbo la ISIS la Afrika ya kati kwa jina la ISCAP pamoja ya kikunchi cha waasi cha jamhuri ya kidemokrasia ya Congo au Congo DRC.

Tangu wakti huo kikundi hicho kimekuwa kikifanya mashambulizi kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ya nchini humo wakiua raia kwa kuwachinja na kutuma picha zake kwenye mtandao.

Kikundi hicho mara nyingi kimekuwa kikizidhihaki nchi za Afrika na nchi za magharibi kwa kushindwa kuingilia shughuli zake na kusema wazi kuwa kiini cha mashambulizi yake ni fedha, makaa ya mawe na gesi asilia iliopo ambazo ni rasilimali zilizopo nchini Msumbiji.

Mwezi Decemba 2020 Marekani ilitoa onyo kuhusu kuimarika kwa kikundi hichi kimuundo na kimkakati huku kikibeba itikadi ya ISIS, mbinu na taratibu na mwono wa kikundi mama cha ISIS ambacho mara nyingi azma yake kubwa ni kuteka eneo moja na kulitumia kwa shughuli zake mbalimbali.

Tayari kikundi hicho kimeutangaza mji wa Macimboa da Praia kuwa ni makao makuu ya ISCAP.

Hivyo kupitia ISCAP kikundi hiki moja ya vyanzo vyake kifedha ni kutumia njia ya waasi wa nchini Congo ambao nao hupata mapato yao kupitia biashara za madini na rasilimali zingine.

Vyanzo vya habari: Daily telegraph, The Times, Telegram na Amaq news.

Nashangaa sana Jeshi la msumbiji ,yaani wanashindwa kuwamaliza hao "WAVUTA BANGI wanaojiita ISIS"? Yaani wanaingia kwako na kufanya mauaji na wao wapo tu kambini wanakula mikate yenye siagi na chai ya maziwa? Hao ni Operation ya Week tu unawakamata na kuwakaanga kwenye concentrated Sulphuric acid.
 
Back
Top Bottom