Uingereza yatuma kikosi maalum cha makomandoo wa SAS Msumbiji kumuokoa raia wao aliyetekwa

Uingereza yatuma kikosi maalum cha makomandoo wa SAS Msumbiji kumuokoa raia wao aliyetekwa

Hata mimi huwa naona kama ni propaganda tu. Yaani nchi na jeshi lake washindwe na kakikundi ka watu wachache??? Nchi ina vikosi vingapi vya jeshi???? Wana silaha za aina gani nzuri kuliko hao waasi?
Mkuu huoni hata kule Nigeria Boko haram wanavo zingua na Jeshi la nigeria lipo ....mm nazani na serikali hua zinahusika kufuga hawa mmbwa .
 
SAS(special air service)
SBS(special boat service)

Vyote ni vikundi vya SF vya Uingereza, na kazi zao zinautofauti kidogo sana lakini training na selection yao ni sawa. Not for the faint hearted, wanakwambia, sio kila jeshi anafaulu selection course ya vikundi hivi. Na wanaofaulu na kuhitimu ndio wale viumbe unaweza dhani ka progamiwa kiaina, yaani wako almost to perfection quality of SF
Kidogo nifuzu mafunza ya SAS.. sema sipendi show off🤨
 
Hivyo kupitia ISCAP kikundi hiki moja ya vyanzo vyake kifedha ni kutumia njia ya waasi wa nchini Congo ambao nao hupata mapato yao kupitia biashara za madini na rasilimali zingine.
Dah sasa hayo madini na rasilimali nyingine wanafanya biashara na nani na kwa routes zipi?
 
Hv SADC hawawezi kuungana kupiga joint special operation kusafisha hawa jamaa.Maana instability wanayotujengea hata sisi wa Tz hatutakuwa salama soon.
Wanaungana kwenye chaguzi na kuongoza miaka ya utawala.... kwa hili wamefanikiwa 💯
 
Watanzania kadha wa kadha wapo jeshi la GB.. vikosi kama SAS wanaangalia mambo mengi sanaaa.. tofauti na mjeshi wa kawaida
Kuna mshikaji mmoja wa KE alikuja training zile zao huku 'BATUK', alionyeshwa kwa news, jamaa bado anapiga 'Kiswahili sheng' cha Ghetto yaani huwezi dhani anaishi GB, alafu kafuga rasta, dah huku kwetu upara kwenda mbele, tena tatoo nazo pia shida, yaani requirements kibaoo zenye hazina msingi. Huyu dogo yuko upande wa Catering, basi kazi Kilaini aisee 🤣
 
Kuna mshikaji mmoja wa KE alikuja training zile zao huku 'BATUK', alionyeshwa kwa news, jamaa bado anapiga 'Kiswahili sheng' cha Ghetto yaani huwezi dhani anaishi GB, alafu kafuga rasta, dah huku kwetu upara kwenda mbele, tena tatoo nazo pia shida, yaani requirements kibaoo zenye hazina msingi. Huyu dogo yuko upande wa Catering, basi kazi Kilaini aisee 🤣
Ulaya ni Ulaya tu mkuu.. Wanatumia akili nyingi kuliko Maguvu.. hata vita za sahihi ni akili nyingi na Technology sio maguvu mengi
 
Mkuu, tukianza kuongelea hawa jamaa itachukua muda sana.

Hivi wafahamu kuwa hawa huweza kuingia katika nchi kama watalii na kukaa kuleee mbugani.

Huko huweza kutuma drone ikazunguka Mererani yote na kutuma picha makao makuu bila hata mtu kutambua?

Ogopa sana hawa watu.

?
Acha uongo hiyo drone unafikiri inarushwa rushwa ovyo tu!!!


Acha story za vijiweni!!!
 
Daaaaaaah Mmakonde anaponzwa na Gesi yakeee
Dunia ina mambooo hiiiii
hatariii
 
SBS MARINES abseiling from helicopter holding MP5 A3 9mm submachine guns helmets wet suits gas masks goggles

Makomandoo wa kikosi maalum kiitwacho Special Boat Service: Picha na Royal Marine ya Uingereza.

Uingereza imetuma makomandoo watatu wa SAS kwenda nchini Msumbiji kusaidia kumuokoa raia wa nchi hiyo bwana Phillip Mawer ambae ametekwa na kikundi cha kigaidi cha ISIS.

Gazeti la The Times la Uingereza limeripoti kuwa makomandoo hao watatu wanatoka katika kambi ya jeshi la Uingereza iliyoko mjini Nairobi nchini Kenya ambayo pia hutoa mafunzo ya vita ya msituni au "Bush Warfare".

Majeshi maalum ya Marekani tayari yapo nchini humo yakitoa mafunzo maalum kwa makomandoo wa Msumbiji.

Raia huyo pamoja na raia wengine wa nchi hiyo walikuwa wakijaribu kukimbia mji wa Palma ambao ulivamiwa na kikundi hicho cha ISIS ambacho baadae kilitoa taarifa ya kuthibitisha mashambulizi yake kupitia kituo chake cha habari cha Amaq.

Bwana Mawer ni mhandisi aliekuwa akifanya kazi katika kampuni ya RA yenye makazi yake Dubai na hujishughulisha na kazi za ugavi na makazi ya muda kwa wataalam mbalimbali wanofanya kazi nchini Msumbiji.

Pia bwana Mawer alikuwa akisaidia kufunga mitambo ya mafuta ya kampuni ya Total ya Ufaransa katika mji wa Palma ambao upo mpakani kabisa na Tanzania pamoja na mji mwingine wa Mocimboa da Praia ambayo ipo ndani ya jimbo la Cado Delgado ambalo mji mkuu wake waitwa Pemba.

Gazeti la Daily Teleghraph pia linaripoti kuwa kikundi hicho cha ISIS kilifanya shambulizi lake siku ya jumatatu huku magaidi wakitokea pande tatu tofauti na baadae wakatangaza kupitia ujumbe wa mtandao wa Telegram kuwa wamefanya shambulizi hilo na mji wa Palma uko chini ya himaya yao.

Watu saba waliuawa akiwemo raia mmoja wa Uingereza walipokuwa wakikimbia kutoka hoteli ya Amarula walokuwa wakitumia kwa makazi ana ambayo ipo karibu kabisa na mradi wa gesi wa Total.

Kikundi cha ISIS nchini Msumbiji kilianza kushamiri kuanzia mwaka 2015 kikitumia jina la Ansar al- Sunna sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo kikifuata itikadi za Aboud Rogo Mohammed ambae hutba zake ziliwagusa vijana wasio na ajira katika eneo lenye wingi wa gesi ya mafuta.

Baadae kikundi hichi kikaanza kujenga shule za madrasa pamoja na misikiti kiasi cha kuwavuta wenyeji wengi walokuwa wakiishi katika eneo hilo.

Mwaka 2017 kikundi hicho kikaanza kufanya mashambulizi wakitumia jina la Al shabab wa Somalia ingawa hawakuwa na uhusiano wowote na kiongozi wa kikundi hicho.

Baadae kikundi hicho kikaanza kutuma picha katika mtandao wa Telegram kikionyesha picha zenye alama za ISIS wapiganaji wake wakiwa wamebeba bendera za ISIS huku wakilitaja jina la kiongozi wa kikundi hicho Abu Bakr al Baghdadi.

Baadae ISIS makao makuu wakatoa taarifa kuwa kikundi hicho cha Msumbiji kimeingzwa rasmi katika jimbo la ISIS la Afrika ya kati kwa jina la ISCAP pamoja ya kikunchi cha waasi cha jamhuri ya kidemokrasia ya Congo au Congo DRC.

Tangu wakti huo kikundi hicho kimekuwa kikifanya mashambulizi kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ya nchini humo wakiua raia kwa kuwachinja na kutuma picha zake kwenye mtandao.

Kikundi hicho mara nyingi kimekuwa kikizidhihaki nchi za Afrika na nchi za magharibi kwa kushindwa kuingilia shughuli zake na kusema wazi kuwa kiini cha mashambulizi yake ni fedha, makaa ya mawe na gesi asilia iliopo ambazo ni rasilimali zilizopo nchini Msumbiji.

Mwezi Decemba 2020 Marekani ilitoa onyo kuhusu kuimarika kwa kikundi hichi kimuundo na kimkakati huku kikibeba itikadi ya ISIS, mbinu na taratibu na mwono wa kikundi mama cha ISIS ambacho mara nyingi azma yake kubwa ni kuteka eneo moja na kulitumia kwa shughuli zake mbalimbali.

Tayari kikundi hicho kimeutangaza mji wa Macimboa da Praia kuwa ni makao makuu ya ISCAP.

Hivyo kupitia ISCAP kikundi hiki moja ya vyanzo vyake kifedha ni kutumia njia ya waasi wa nchini Congo ambao nao hupata mapato yao kupitia biashara za madini na rasilimali zingine.

Vyanzo vya habari: Daily telegraph, The Times, Telegram na Amaq news.
Duh
 
Back
Top Bottom