Uislam na Ukristo siyo maadili ya Mtanzania na Mwafrika, ni moja ya nyenzo ya mmomonyoko wa maadili

Dini imeleta mafundisho mengi sana na ndio maana watu husema tumestaarabika maana kuna watu mpaka leo wana maadili na tabia za hovyo
Kinachomfanya MTU awe muungwana ni Elimu Sahihi. Siô Dini.
Dini kûna mafundisho àmbayo siô ya kiungwana.
Tusingefuata dini sidhani kama tungekuwa hivi
Pamoja na Dini kusema Usafi ni moja katika Imani lakini bado watu ni wachafu kupindukia
Mbona zîpo jamii Ambazo hazijafuata Dini za Uislam na ukristo na zîpo Mbali na wasafi. Mfano wachina
Kuna uzi unaongelea kuhusu uchafu wa mama ntilie wa Tz na ukifananisha na mama ntilie wa Rwanda kwa usafi

Mama ntilie wàpo wasafi na wàpo wachafu na wôte hawatagemei Dini
Sisi mbali na watu kusema wana dini fulani lakini bado kuna tatizo kubwa hata maadili ni tofauti
Kwani Vigodoro na kucheza uchi ndio maadili unayoona yanafaa
Sasa akija Padri au Shehe akakemea utamshangaa?
 
Pia dini zimeleta mambo mengine ya hovyo na ajabu ajabu, nafikiri kikubwa na kwamba Waafrika walichukua kila kitu kilicho kwenye na kufikiria kila yaliyoandikwa kwenye hivi vitabu ni matukio na maisha halisi(literally).
Tatizo la muafrika alishindwa kujikomboa kifikra tangu wazungu walipokuja na baadae waarabu
Hebu fikiria walisombwa na wengi kuuwawa waliojaribu kupinga
Mila na desturi zikafa na kuzikwa
Wazee wetu vyote walivyokuwa wanaamini na kufuata vikachomwa moto na mpaka lugha wakasahau kwa kuchanganywa wa huku na huko

Leo mpaka mtu mweusi alieko America hataki kuwa mwafrika kwa sababu babu yake aliitwa Malcolm au George

Kwa kweli tulibeba mambo yao yote na kuyafurahia ingawa babu zetu waliteseka sana
Leo hii kuna machafuko 🇬🇧 kisa mtoto aliekuwa anabaguliwa tangu mtoto shuleni na kuamua kuwachoma visu watoto wadogo wa kizungu
Mtoto ni mzaliwa wa hapa ila bado walimbagua sana

Inabidi tujielewe na kuwa proud to be Black
Sisi tamaduni zetu tunaziuwa wenyewe
Tulikuwa tuna dawa zetu kwa kutumia miti na mizizi ila Leo wamechoma moto kila sehemu na miti mingi imekwisha na kulazimika kutumia sumu zao tunazoziita dawa
Tuamke na kufanya yetu
Elimu waliyoiacha ni ya kuvumbua vitu na kukuza uchumi ila sisi tumeona tuwachape watoto fimbo sana ili wakariri na kuwaita wasomi

Msomi hata bawaba hawezi kutengeneza
 
Lakini haupingi uvaaji wa nguo za viwandani (ulizoletewa na hao waleta dini), matumizi ya simu, usafiri, na umesoma elimu yao😂😂
Si ni wabaya kwa nn usivikatae vyote?
 

first off yote ulioyaorodhesha siyo Ukristo kwanza ni kinyume chake ni anti christ, pili kulikuwa hakuna kitu kama ndoa kama tuijuavyo leo hii kabla ya Ukristo kuingia kwetu, tulikuwa ni polygamy sasa kama polygamy ni bora klk Christian marriage hilo unaweza kuamua mwenyewe …
 
Kwa wengi wetu
Hili la mpende jirani labda aliefuata msimamo kwa Dini ila sio maadili ya wengi
Mpaka leo ugomvi wa jirani ni mkubwa sana kwa baadhi ya watu na pia wafugaji na wakulima kwetu bado ni tatizo
Ukienda Misri utaona mto Nile ambapo wakulima na wafugaji wanaishi in harmony
Upande mmoja wa ziwa ni wakulima na upande mwingine ni wafugaji na kwenye ziwa wavuvi je ni raha iliyoje kama mtaelewana kama binadamu?

Kweli maisha yalikuwepo kabla ya dini kuja ila tumejifunza mema mengi pia ingawa wengine wanaona ni za kuja

Maadili ni jambo la kuzingatia sana na sisi hilo hatulifundishi popote zaidi ya kwenye dini na nyumbani ila mashuleni ni mwendo wa kukariri tu

Nani wa kumlaumu kwa hao vijana wanaochungulia wanawake wanaojifungua hospital ya Tabora ?
Hii ilikuwa kwenye taarifa za habari nchini
Je nani wa kulaumiwa?
Watoto lazima wafundishwe maadili na tabia njema kila mahali
 
Yote hayo Mbona ni kinyume na Ukristo na uislam Wala hayaruhusiwi hayo kwa dini hizo
 
Nashindwa kutofautisha kati ya maadili na dini kwani dini ni nyenzo ya kuyafikia maadili mema

Ndani ya dini kuna maadili na tamaduni pamoja na mila hivyo dini ipo kwa ajili ya kufundisha maadili mema sio mabaya

Dini ni asili ya mwanadamu, ukiristo na uislam ni miongoni mwa dini(njia za kumjua Muumba) lakini zipo nyingi zaidi ambazo kimsingi zinaelekea kuhimiza maadili mema. Kuhusu kutofautiana ni mapokezi tu ya wafundishwaji

Kabla ya ujio wa waarabu na wazungu mataifa yote yalikuwa na dini ambazo pia zinaelekeza maadili mema.
 
Muhammaad ni mtume wa Mewisho aliyepewa Qur'an. Mitume yote kabla yake ilileta ujumbe huo huoi mmoja tu. Uislam.

Uislam ndiyo mfumo kamili wa maisha uliopo ambao hauna mfano wake.
 
Sio mmomonyoko, kimsingi ni mageuzi. Na hii ni kwasababu sio maadili yote yanatoweka tamaduni zikichanganyika. Kuna maadili ya jumla ambayo jamii zote zinafuata mfano watoto kuheshimu wazazi...

Tulichobadilishiwa ni mambo madogo tu kama mavazi, lakini maadili binafsi(subjective morality) ambayo hayachochewi na tamaduni yeyote ni ya jumla na kila mwanadamu anayafuata.

Yale haufundishwi unayajua kadri unavyoishi na viumbe wenzako, hata wanyama wana maadili yao....
 
Muhammaad ni mtume wa Mewisho aliyepewa Qur'an. Mitume yote kabla yake ilileta ujumbe huo huoi mmoja tu. Uislam.

Uislam ndiyo mfumo kamili wa maisha uliopo ambao hauna mfano wake.
Nenda China kawaambie hivyo uone jinsi watakavyokunyoosha kwenye re-education camps.
 
Udugu, kuwakarimu wageni, kuwasaidia wenye shida, kuwatunza wajane na yatima, wagonjwa na kuzikana wakati wa misiba, nk - kwa neno moja au mawili unaweza kusema ni kitu gani?
 
Tukiongelea maadili tunaongelea mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu au utaratibu wa kuishi

Jinsi ya kula, kuvaa, kulala, kujamiiana(kuhusiana), kuongea, muonekano, mtazamo, hisia(kuhuruma, upendo, kutokuwa katili na roho mbaya n.k), kutembea na mengine mengi katika maisha ya mwanadamu yanatakiwa yafanyike ki maadili zaidi yaani ki tabia njema

Ukiangalia kwa undani dini nyingi zipo kwa ajili ya kuhamasisha mambo hayo kupitia imani za kiungu na uumbaji hata kabla ya ujio wa uislam na ukiristo katika jamii zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…