UISLAM NA UKRISTO SIÔ MAADILI YA MTANZANIA NA MUAFRIKA NI MOJA YA NYENZO YA MMOMONYOKO WA MAADILI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kîla jamii inamaadili yake. Maadili yanatokana na ûtamaduni wa jamii Husika. Kîla jamii inautamaduni wake.
Maadili ni mafundisho yanayotolewa kwèñye jamii yenye kuonyesha Tàbia Njema na tàbia Mbaya na kutaka Watu wafuate mambo Mema.
Maadili ya jamii Moja huweza kutofautiana na maadili ya jamii zingine. Ingawaje Yapo maadili àmbayo yanafanana.
Kukiuka Maadili ya jamii yako ndîo huitwa MMOMONYOKO WA MAADILI.
Muafrika anamaadili yake kutokana na tamaduni Zake.
Wazungu wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.
Waarabu wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.
Wachina, wahindi n.k wôte wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.
Kîla jamii ina Mila na desturi nzuri na Potofu. Mila na desturi au tuite maadili huwa potofu Kwa sababu mbalimbali lakini sababu kûbwa ni Wakati(Zama) na sababu ya pili utofauti Kimila.
Mfano, kile kinachoonekana NI maadili Mema Kwa jamii Moja siô ajabu kikawa NI maadili potofu Kwa jamii ñyiñgine
Mathalani, Ndoa za mitala NI maadili Mema Kwa jamii nyingi za kiafrika na Mashariki ya kati lakini Kwa jamii ya kizungu siô maadili
Ukeketaji ni maadili Mema Kwa Baadhi ya jamii za kiafrika lakini Kwa wazungu NI Mila Potofu.
Mahari ni maadili Mema Kwa jamii nyingi Duniani ikiwemo jamii za kiafrika lakini Kwa jamii nyingi za kizungu NI maadili potofu.
Upotofu na usahihi mara nyingi hutokana na mabadiliko ya kizama(kinyakati) na tofauti za kiutamaduni.
Ukristo na Uislam siô maadili ya Mtanzania na Muafrika Kwa ujumla.
Huwaga nashangaa nikisikia Mtu akiwaita Wengine Hawana maadili Wakati Muda huohuo MTU huyo NI muislam au Mkristo.
Muafrika mwenye maadili hawezi kuwa Muislam au Mkristo. Kuwa Muislam au Mkristo ni kukosa maadili ya kiafrika na pia ni mmomonyoko wa maadili.
Kukaidi, kukiuka, kutofuata maadili yako ya asili na kufuata maadili ya jamii ñyiñgine hiyo ndîo tofsiri halisi ya MMOMONYOKO WA MAADILI.
Maadili humong'onyolewa na vitu vingi lakini kikubwa zaidi ni Muingiliano WA tamaduni zaidi ya Moja Kwa kile kiitwacho utandawazi.
Huwezi Acha ûtamaduni wako na kuita tamaduni za Wengine ni maadili. Kitendo cha kuacha tuu na kusaliti ûtamaduni wako ni mmomonyoko wa maadili tosha.
Kabla ya Wageni kuja, waafrika walikuwa na maadili Yao Mema tuu. Hii haimaanishi hapakuwa na Mila mbaya na potofu.
Nilishasema kîla jamii inamila Zake nzuri na Mbaya.
Mila mbaya kama uchawi, Kutoa Watoto kafara, unyanyasaji WA kijinsia, n.k zilikuwepo Karibu jamii zote hata jamii za kizungu zilikuwa na Mila hizô.
Jamii za kiafrika zilikuwa zinaabudu katika Mungu Mmoja kupitia mizimu ya mababu kama ilivyo Kwa Waislam na Wakristo ambao huamini katika Mungu Mmoja katika mitume na Manabii.
Kabla ya ujio WA uislam na ukristo waafrika walikuwa na maadili kuliko Zama hizi baàda ya ujio wa Dini hizi.
Ûkienda kwèñye jamii Ambazo hazina Ukristo au Uislam zina maadili ukilinganisha na jamii Zenye Ukristo na Uislam.
Nenda Umasaini ndanindani, nenda Kwa Wahadzabe na watindiga Huko utajionea mwenyewe
Maadili ya kwèli hayafundishwi Kanisani au Misikitini. Maadili hufundishwa nyumbani.
Maadili yanauhusiano na asili ya Mtu na mîungu Yao.
Baadhi ya mafundisho ya kikristo na kiislam yanaweza kuwa mazuri Kwa kiwango cha juu lakini haimaanishi NI mafundisho Bora kuliko yale mafundisho ya asili Yenu, Wazazi wako, Babu zako Ambao wewe ndîo umetokea.
Maadili pia hufanyiwa matengenezo (reformations) ili yaendane na wakati Husika. Hata maadili ya kiislam na Kikristo yamefanyiwa marekebisho mengi tuu kufikia Hapo yalipo.
Maadili NI utambulisho yaani ûtamaduni. Mtu kutokuwa na maadili ya Kwao inamaanisha Hana utambulisho na Hana maadili na amemomonyoko kimaadili.
Yàani kikawaida Huwezi kuwa Muafrika Ukawa Mkristo au muislam alafu ukajiita unamaadili labda Kama hujui mantiki ya maadili yenyewe.
Unaweza Ukawa mwema na Mtu Bora Kwa kufuata tamaduni za kwetu zile zilizobora. Lakini zile zilizombaya ukaziacha.
Kûna wale watakaokuja na hoja ya Teknolojia.
Kwamba Kwa nini tunatumia Teknolojia za kigeni.
Mfano Simu au Magari n.k.
Tunaweza Kutengeneza Simu Kulingana na ubunifu wa tamaduni zetu.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
Kwa Sasa Dar es salaam