Uislam na Ukristo siyo maadili ya Mtanzania na Mwafrika, ni moja ya nyenzo ya mmomonyoko wa maadili

Uislam na Ukristo siyo maadili ya Mtanzania na Mwafrika, ni moja ya nyenzo ya mmomonyoko wa maadili

Na hii ndo mbaya yani kama watanzania hatuna utambulisho wowote wala muongozo wa maadili ya kwetu
Leo hii ukitaka uwaweke watoto kwenye so called maadili mema ni lazima akiwa mdogo tu uanze kumpeleka akajazwe funza kichwani tulizoletewa na wageni
 
Fundisho lipi la uislam sio sahihi kwa jamii nyingine?

Yapo mafundisho mengi tuu inategemea na jamii inayopelekewa
Mfano fundisho la wake wengi siô Sahihi Kwa jamii za Wakristo na jamii za kizungu.

Fundisho la Quran kuua wasio Waislam siô Sahihi Kwa jamii za kiungwana,

Fundisho la Mavazi, kwamba mwanamke sharti ajisitiri NI Sahihi Kwa Waislam lakini siô Sahihi Kwa wazungu na jamii za kiafrika na Kikristo.

Fundisho la Kutokula Nguruwe NI Sahihi Kwa Waislam lakini siô Sahihi Kwa wazungu, waafrika na wachina.

Yapo mengi
 
UISLAM NA UKRISTO SIÔ MAADILI YA MTANZANIA NA MUAFRIKA NI MOJA YA NYENZO YA MMOMONYOKO WA MAADILI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kîla jamii inamaadili yake. Maadili yanatokana na ûtamaduni wa jamii Husika. Kîla jamii inautamaduni wake.

Maadili ni mafundisho yanayotolewa kwèñye jamii yenye kuonyesha Tàbia Njema na tàbia Mbaya na kutaka Watu wafuate mambo Mema.
Maadili ya jamii Moja huweza kutofautiana na maadili ya jamii zingine. Ingawaje Yapo maadili àmbayo yanafanana.

Kukiuka Maadili ya jamii yako ndîo huitwa MMOMONYOKO WA MAADILI.

Muafrika anamaadili yake kutokana na tamaduni Zake.
Wazungu wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.
Waarabu wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.
Wachina, wahindi n.k wôte wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.

Kîla jamii ina Mila na desturi nzuri na Potofu. Mila na desturi au tuite maadili huwa potofu Kwa sababu mbalimbali lakini sababu kûbwa ni Wakati(Zama) na sababu ya pili utofauti Kimila.

Mfano, kile kinachoonekana NI maadili Mema Kwa jamii Moja siô ajabu kikawa NI maadili potofu Kwa jamii ñyiñgine
Mathalani, Ndoa za mitala NI maadili Mema Kwa jamii nyingi za kiafrika na Mashariki ya kati lakini Kwa jamii ya kizungu siô maadili

Ukeketaji ni maadili Mema Kwa Baadhi ya jamii za kiafrika lakini Kwa wazungu NI Mila Potofu.

Mahari ni maadili Mema Kwa jamii nyingi Duniani ikiwemo jamii za kiafrika lakini Kwa jamii nyingi za kizungu NI maadili potofu.

Upotofu na usahihi mara nyingi hutokana na mabadiliko ya kizama(kinyakati) na tofauti za kiutamaduni.

Ukristo na Uislam siô maadili ya Mtanzania na Muafrika Kwa ujumla.

Huwaga nashangaa nikisikia Mtu akiwaita Wengine Hawana maadili Wakati Muda huohuo MTU huyo NI muislam au Mkristo.
Muafrika mwenye maadili hawezi kuwa Muislam au Mkristo. Kuwa Muislam au Mkristo ni kukosa maadili ya kiafrika na pia ni mmomonyoko wa maadili.

Kukaidi, kukiuka, kutofuata maadili yako ya asili na kufuata maadili ya jamii ñyiñgine hiyo ndîo tofsiri halisi ya MMOMONYOKO WA MAADILI.

Maadili humong'onyolewa na vitu vingi lakini kikubwa zaidi ni Muingiliano WA tamaduni zaidi ya Moja Kwa kile kiitwacho utandawazi.

Huwezi Acha ûtamaduni wako na kuita tamaduni za Wengine ni maadili. Kitendo cha kuacha tuu na kusaliti ûtamaduni wako ni mmomonyoko wa maadili tosha.

Kabla ya Wageni kuja, waafrika walikuwa na maadili Yao Mema tuu. Hii haimaanishi hapakuwa na Mila mbaya na potofu.

Nilishasema kîla jamii inamila Zake nzuri na Mbaya.
Mila mbaya kama uchawi, Kutoa Watoto kafara, unyanyasaji WA kijinsia, n.k zilikuwepo Karibu jamii zote hata jamii za kizungu zilikuwa na Mila hizô.

Jamii za kiafrika zilikuwa zinaabudu katika Mungu Mmoja kupitia mizimu ya mababu kama ilivyo Kwa Waislam na Wakristo ambao huamini katika Mungu Mmoja katika mitume na Manabii.

Kabla ya ujio WA uislam na ukristo waafrika walikuwa na maadili kuliko Zama hizi baàda ya ujio wa Dini hizi.

Ûkienda kwèñye jamii Ambazo hazina Ukristo au Uislam zina maadili ukilinganisha na jamii Zenye Ukristo na Uislam.
Nenda Umasaini ndanindani, nenda Kwa Wahadzabe na watindiga Huko utajionea mwenyewe

Maadili ya kwèli hayafundishwi Kanisani au Misikitini. Maadili hufundishwa nyumbani.
Maadili yanauhusiano na asili ya Mtu na mîungu Yao.

Baadhi ya mafundisho ya kikristo na kiislam yanaweza kuwa mazuri Kwa kiwango cha juu lakini haimaanishi NI mafundisho Bora kuliko yale mafundisho ya asili Yenu, Wazazi wako, Babu zako Ambao wewe ndîo umetokea.

Maadili pia hufanyiwa matengenezo (reformations) ili yaendane na wakati Husika. Hata maadili ya kiislam na Kikristo yamefanyiwa marekebisho mengi tuu kufikia Hapo yalipo.

Maadili NI utambulisho yaani ûtamaduni. Mtu kutokuwa na maadili ya Kwao inamaanisha Hana utambulisho na Hana maadili na amemomonyoko kimaadili.

Yàani kikawaida Huwezi kuwa Muafrika Ukawa Mkristo au muislam alafu ukajiita unamaadili labda Kama hujui mantiki ya maadili yenyewe.

Unaweza Ukawa mwema na Mtu Bora Kwa kufuata tamaduni za kwetu zile zilizobora. Lakini zile zilizombaya ukaziacha.

Kûna wale watakaokuja na hoja ya Teknolojia.
Kwamba Kwa nini tunatumia Teknolojia za kigeni.
Mfano Simu au Magari n.k.
Tunaweza Kutengeneza Simu Kulingana na ubunifu wa tamaduni zetu.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
Kwa Sasa Dar es salaam
Tulichukua tamaduni za watu na kuzifanya zetu tukaacha maarifa yao ambayo yangetuwezesha kuboresha tamaduni na maisha yetu kwa ujumla.
 
Na hii ndo mbaya yani kama watanzania hatuna utambulisho wowote wala muongozo wa maadili ya kwetu
Leo hii ukitaka uwaweke watoto kwenye so called maadili mema ni lazima akiwa mdogo tu uanze kumpeleka akajazwe funza kichwani tulizoletewa na wageni

😀😀
Alafu hizô funza zikianza kufukuta kichwani zinaona Watu WA Dini ñyiñgine wabaya na kuleta utengano
 
Kama umejitambua kwa elimu ya mzungu basi ulichoandika ni unafiki , wazee wa zamani walikuwa smart na more resistant kuliko wa sasa , ilikuwaje dini zikaingia? Hpo hamna jibu bali dini ni mpango wa Mungu ndio maana zilisambaa mpaka ulaya.

Hakuna ushahidi wa babu wa mtu anajua zaidi ni maandisho ambayo ukienda kitabu kingine ukisoma yapo tofauti .

Unaposema mwafrika alikuwa na tamaduni zake ni unafiki hata kihistoria mwanadamu alitoka sehemu kwenda nyingine ili kupata ustaarabu na maendeleo, mwafrika alikuwa anakula nyama mbichi baadae akagundua moto mpaka kuanza kutengeneza zana zake mwenyewe...Hii inaonyesha lazima binadamu apate maendeleo kulingana na mabadiliko , dini za leo ndipo ambpo mwanadamu alipangiwa kuwepo leo kwa sababu hata maandiko kayasoma kweny vitabu ...Hiyo miaka ya kuishi pangoni mlikuwa mnajua kuandika?

Huwezi kusema unajua mila za muafrica wakati hata mwaka 1800 mwafrica alikuwa kashajitambua anaishi mbali na wanyama , Mila zako inategemea wazazi wako huwezi kusema sijui babu zako walikuweje huko nyuma .Mila sio conservativness mila zinabadilika kila siku kwa sababu binadamu anajifunza kulingana na mazingira.

Basi usisome wala kutumia jf na simu kabisa maana babu zako hawakusoma , hata hao watu weupe nao walianzia chini kama mwafrika.
 
Yapo mafundisho mengi tuu inategemea na jamii inayopelekewa
Mfano fundisho la wake wengi siô Sahihi Kwa jamii za Wakristo na jamii za kizungu.

Fundisho la Quran kuua wasio Waislam siô Sahihi Kwa jamii za kiungwana,

Fundisho la Mavazi, kwamba mwanamke sharti ajisitiri NI Sahihi Kwa Waislam lakini siô Sahihi Kwa wazungu na jamii za kiafrika na Kikristo.

Fundisho la Kutokula Nguruwe NI Sahihi Kwa Waislam lakini siô Sahihi Kwa wazungu, waafrika na wachina.

Yapo mengi
Sawa.haya niambie mtu mweusi ana mafundisho gani ambayo ni sahihi
 
Sawa.haya niambie mtu mweusi ana mafundisho gani ambayo no sahihi
Ngoja atuambie kwanza, mtu analeta story za babu zake waliozaliwa kijijini hapo ...Wzee hao walikuwa wanatembea matako wazi , sasa muacha atembee matako wazi 😀 😀 😀 .

Mimi babu yangu nilimuona alikuwa anavaa nguo so huwezi kuniambia kulikuwa na mila z mwafrica , nifuate kitu ambacho hata babu yangu hakijui .
 
Ngoja atuambie kwanza, mtu analeta story za babu zake waliozaliwa kijijini hapo ...Wzee hao walikuwa wanatembea matako wazi , sasa muacha atembee matako wazi 😀 😀 😀 .

Mimi babu yangu nilimuona alikuwa anavaa nguo so huwezi kuniambia kulikuwa na mila z mwafrica , nifuate kitu ambacho hata babu yangu hakijui .

Hakuna jamii àmbayo haikutembea matako Wazi Kulingana na historia ya Dunia
 
Mkuu Robert Heriel Mtibeli Dini zote mbili ulizo taja zimesababisha ukoloni, biashara ya utumwa kuingia afrika, pia zimesababisha vifo Kwa maelfu na maelfu katika Bara la Africa,

Lakini cha ajabu viongozi wa Ki afrika Wana Kaa na viongozi wa kidini ambapo kiasili ni maadui zao tokea Zamani.

Maadili ndîo tatizo
 
Back
Top Bottom