Kwanza naomba kujua wazungu dini yao ni ipi? Naikiwa unafikiri ukristo ni dini ya wazungu hapo umepotea kwasababu ukisoma biblia maandiko yake hayaendani na uzungu. Wazungu walicho fanikiwa ni kuidanganya dunia kwa kutengeneza mapicha mengi ya mitume ambao wamewaweka wote ni wazungu yaani walivyo washenzi hadi malaika wanewaweka taswira ya Uzungu.
Ukristo inabaki kuwa dini ya wazungu maana hapo kabla hakukuwai kuwepo hiyo dini ya ukristo.
Ukristo umeanzishwa na warumi ambao ndio chanzo cha kanisa Catholic ambao nao waliiba tamaduni za Afrika na kuunda huo uongo uitwao uyahudi na baadae Ukristo.
Ndivyo hata ktk uislam ni dini ya waarabu ambayo dini hiyo nayo chanzo chake ni maandiko ya Kanisa la Catholic+tamaduni za kiarabu.
Dini zote mafundisho yao yamebase kwenye kudanganya, kupotosha na kuutukuza utamaduni wa mahala fulani.
Naposema kupotosha ninamaanisha mfano dini ya uislam kusema kuwa muislam wa kwanza ni Adamu wakat huo huo uislam umenza juzi tu huo ni uongo, kama vile ukristo kusema mtu wa mwanzo ni adamu aliyeumbwa hapo Asia, wakati kiusahihi Mtu wa kwanza aliishi Maelfu ya miaka na hakuishi huko majangwani bali Afrika.
Vile vile ushenzi wa dini ni kupotosha na kuharibu taswira za jamii zingine kwa kuona tamaduni zao hazifai, ila wao na imani zao ndizo sahihi, mfano unawezaje kubadili majina ya watu eti kisa uyatafsiri kwa lugha fulani? Je majina hubadirishwa? Unaweza kutoa maana ya jina lolote lile lakini si kulibadiri kama hizo dini zenu zilivyobadiri majina ya wahusika wa biblia.
Kiuhalisia hakuna mtu aliyewai kuitwa Adamu, wala Yesu sijui wakina paulo, haya ni majina ya wazungu walioamua kuiba tamaduni za watu wengine na kuzipa uhusika wao na majina yao, vile vile wakajipa na uhusika wa historia isiyowahusu, kama walivyofanya hapo middle east kwa kusema lile taifa la Biblia ndio hao wazungu/waarabu hapo israel feki, hili jambo tunaliongea humu kila siku na tutaendelea kuliongea mpaka watu waelewe kuwa kwa sasa wazungu wamefanikiwa kuupotosha ulimwengu kwa kila jambo, wameiba historia zisizo zao, wameiba gunduzi na technolojia zisizo zao na kusema wao ndio wagunduzi.
Wameharibu maadili na utamaduni wa kiafrika kwa kuleta ushetan wanaopamba jina kwa kuita Dini.
Hapo kabla waafrika hawakuwa na dini bali walikuwa na imani, kunatofauti kati ya dini na imani, dini ni sheria,taratibu, mafundisho ya jamii fulani kuhusu mfumo wa maisha, huku imani ikiwa jambo la mwisho, wakati huo Imani ni hisia na ufahamu wa jambo uliloliona,ulilosikia, ama ambalo bado hujaliona na kusikia bali una hisia nalo.
Hivyo babu zetu walikuwa na imani ndiomaana walifanya mengi makubwa zaidi yetu sisi wapumbavu tuliokataa imani na kushikilia Ushenzi uitwao dini.
Si kweli kuwa waafrika waliabudu mizimu, kuna tofauti kati ya kuomba na kuabudu, wanaoomba kupitia majina ya babu zao hawafanyi ibada za kuwaabudu hao babu zao bali maombi kupitia hao mababu the same thing wanafanya wakristo kupitia Bikra maria, Yesu kristo, baba yao wa mchongo ibrahimu.
Pia mujue kuwa si Imani zote za waafrika zilikuwa ibada ya mababu waliokufa bali kupitia Muumba pekee, na sala/ibada hizi zinafahamika kasomeni historia ya kweli ya afrika achaneni na hizo takataka tulizodanganywa mashuleni.
Ni kweli kuwa tumedanganywa sana na kupotoshwa sana lkn tujitahidi kuamka na kupata elimu sahihi maana kwa kizazi chetu tumebahatika kupata source kubwa na nzuri ya kuujua ukweli wa mambo na siri nyingi kupitia hiyo hiyo mitandao ya kijamii ktk internet waliyounda wao, tutumie maendeleo yao kuufahamu Ukweli halisi na sio kujidharau na kuwakatisha tamaa wanaojaribu kuwafungua macho waafrika wengine.
Huwa nashangaa sana muafrika mweusi pure kumdharau na kumpinga mwafrika mwenzie anayejaribu kuuinua Ukuu wa mwafrika, kisa tu kutetea Uzungu&uarabu, huo ni ujinga na upumbavu wa kukosa akili.
Tuamke jamani.