Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Unachekea nini? Kati ya wewe ambae Zanzibar unayochekea umeiona kwenye barua na yule ambae ndio yuko Zanzibar na inamuhusu.. nani anachekesha hapo!?
 
Mashallah!. Ubarikiwe sana kwa andiko Maridadi mno.

Kufunga ni swala la kiimani zaidi. Najua fika kuna waisilamu wanajidai kuwa kwenye funga huku wanakula mafichoni.

Nadhani hao ndiyo wanaoshindwa kuhimili wakiwaona Makafiri au makundi yaliyoruhusiwa wakipata mlo.

Isute nafsi yako katika kujitolea kumtukuza Mwenyenzi Mungu mwingi wa Rehma.
 
Shukran mkuu.
 
Unachekea nini? Kati ya wewe ambae Zanzibar unayochekea umeiona kwenye barua na yule ambae ndio yuko Zanzibar na inamuhusu.. nani anachekesha apo!?
Bila shaka nawe ni miongoni mwa wanafiki unayedhani ni mtakatifu sana kuliko wengine kisa umehamisha muda wa kula.
 
Kwa nini mnaita watu wengine wasio waislamu ni makafir?
Kafiri ni mtu yoyote yule asiye amini uwepo wa MUNGU au yule anae amini uwepo wa Miungu mingine zaidi ya MUNGU mmoja alieumba mbingu na nchi.

Hata kama anajiita ni muislamu ila kama anaamini na kuiomba/kuitegemea miungu mingine imtatulie shida zake zaidi ya MUNGU mmoja mfano mizimu, nyoka, majini n.k huyo pia anahesabika ni kafiri vile pia.

Swali: kwa nini waislamu wanawaita wakristo ni makafiri?

Jibu: sio matakwa yetu kuwaita hivyo ila Qur'ani tayari imeshaelezea ukafiri wa wakristo na imewetaja wakristo ni makafiri.

Swali: Ni upi haswa ukafiri wa Wakristo?

Jibu:
“Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja.” (al-Maida, 5/73).

“Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu. Sema: Ni nani mwenye kumiliki cho chote mbele ya Mwenyezi Mungu ikiwa Yeye angetaka kumuangamiza Masihi mwana wa Maryamu, na mama yake, na wote waliomo katika ardhi? Na mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ni vya Mwenyezi Mungu. Huumba apendavyo. Na Mwenyezi Mungu anao uweza juu ya kila kitu.” (al-Maida, 5/17)

“Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.” (al-Maida, 5/72).

Kama bado una swali lolote kuhusu ukafiri unaruhusiwa kuuliza.
 

Huku Smz sijui imekuaje maana hata restaurant zitafungwa kisa mfungo
 
Sielewi maana yake ndiyo maana nimemuuliza.Weye ukiitwa mbwa-koko utachekelea?Na wakati hujui maana yake?
Sasa mtu ameniita mimi mbwa koko....why nikasirike? Najua siyo mbwa koko...why should i bother? Kama yeye ananiona mimi mbwa koko basi naye atakuwa kiumbe flani ambacho hakipatani na mbwa....so sina haja ya kuhangaika na mtu wa hivyo.
 
Sawa,
Ila sisi ambao hatufungi basi ni vyema kutafuta sehemu ambayo haipo hadharani

Ni ustaarabu tu
 
Sasa mtu ameniita mimi mbwa koko....why nikasirike? Najua siyo mbwa koko...why should i bother? Kama yeye ananiona mimi mbwa koko basi naye atakuwa kiumbe flani ambacho hakipatani na mbwa....so sina haja ya kuhangaika na mtu wa hivyo.
Umeandika kiwepesiii utadhani ndivyo mlivyo.Jambo dogo tu huwa mnaanzisha taharuki hadi dunia inakataa kujizungusha kwenye muhimili wake.
 
Kwanini hii misosi mnayafunga kula mchana huwa mnairundika mpka usiku na kibugia s bora msingewasaidia wenye uhitaji?
 
Sawa,
Ila sisi ambao hatufungi basi ni vyema kutafuta sehemu ambayo haipo hadharani

Ni ustaarabu tu
Haukatazwi kujifungia hata chumbani kwa hiari yako fanya mkuu.

Ila sio kuwakataza watu ambao wanaenda migahawani kupata kula uwakataze ari kwa kuwa wewe umefunga no no
 
Haukatazwi kujifungia hata chumbani kwa hiari yako fanya mkuu.

Ila sio kuwakataza watu ambao wanaenda migahawani kupata kula uwakataze ari kwa kuwa wewe umefunga no no
Nimekupata mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…