Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

M
Mke wangu anafanya kazi katika Kituo cha Afya. Kuna times ananiambia LEO WATEJA NI WENGI binafsi neno hili huwa linanikereketa.
 
kati ya vitu ambavyo huwa vinanifanya nitamani tuachane na zanzibar, ni kuwachapa viboko wakristo ambao hawajafunga kula mchana, ni ukatili na ugaidi kabisa. hapo ndio huwa naiondoa kabisa zenji moyoni mwangu.
 
Kwanini hii misosi mnayafunga kula mchana huwa mnairundika mpka usiku na kibugia s bora msingewasaidia wenye uhitaji?
Mkuu usitishwe na picha za mitandaoni ambazo mara nyingi huoneshwa futari ya wenye uwezo. Kuna watu wanafuturu kipande cha muhogo na chai na hao ndio wengi.

Lakini pia kuna watu wanejitengenezea utaratibu wa kula vizuri zaidi wakati huu sawa na wewe unavyokula vizuri siku ya pasaka au krisimasi, hatuwezi kukupangia eti kile chakula ukawape wengine. Wapo watu wengi tu wanatoa kwa wenye uhitaji ila sio kwa njia ya maonesho
 
Ujinga mtupu, yaani niache kula mchana kwa sababu ya dini ya mtu tena ya kuletewa? Siku nile aje mpuuzi eti aniulize kwanini nakula mchana haki ya nani huyo mtu aombe Mungu wake tu asiingie anga zangu. Atakula kichapo cha kufa mtu mpaka atajuta kuzaliwa.
 
kwani ni lazma ale watu wamuone?
Kuna mazingira unaweza ukakaa ukala.
Mwingine atataka kununua muhindi atembee nao
 
Ulazima ndp huo ustaarabu ninaosema.
Anunue chakula chake akae sehemu ale
Kwani ni lazima akila watu wasimuona ?

Kuna ulazima gani kwamba akila akajifiche wakati kula sio jinai kwa wale ambao hawalazimiki kufunga ?
 
ushahidi funga ni nguzo ya uislam
Wenzio wakiwa wanatimiza hyo nguzo usiwakere.
Weka ushahidi kwamba mtu ambaye halazimiki kula eti haifai akila huku watu waliofunga wanamuona .
 
Kuna mifungo miwili inaendelea hivi sasa labda wameamua kuwakumbusha na wale majirani maana ya kufunga
 
Hili suala la kujificha wakati wa kula lingekaa kistaarbu, kuoneana huruma kwa mapenzi ingekuwa vyema na wala si kulazimishana.

Iwe ni hiyari, mtu kwa kumuonea huruma swahiba wake, rafiki yake jirani yake kwamba mwenzangu ana swaumu hivyo si vema nile mbele yake, ila akiamua kula muacheni ale. Ni kama vile mvuta sigara mstaarabu anaona aah, makaveli havuti sigara hivyo si vema nikaenda kuvuta nae akiwa karibu, mkeo mjamzito chakula fulani alikuwa anakioenda hapo kabla ila kwa sasa hawezi kukitia kinywani si vema ukanunua kwenda kukila mbele yake n.k n.k

Kwanza tunakubali soote hakuna kulazimishana katika dini.. Hii dini ni ya huruma na mapenzi japo watu(waislam tukichangia) tumeinajisi dini yetu, inaonekana ni dini ya ubabe, ugomvi kuchinjana chinjana n.k.

Enzi za mtume aliishi na watu wasiokuwa waislam
Kuna kisa kimoja cha umar ibn khattab kipindi cha uongozi wake, ilikuwa wale wadiojiweza wanapewa fungu(kwa sasa tunasema ama tunaweza fananisha na pensheni). Akamkuta mzee mmoja yuko dhaifu,ombaomba, kumuuliza vipi wewe pato lako unatumiaje, akasema yeye hapati chochote sababu yeye ni kafiri, umari akamuuliza ujanani mwako ulikuwa unatoa kodi, akajibu ndio, umar akawaamrisha wasaidizi wake aorodheshwe katika watu wanaopewa fungu, haiwezekani ujanani mwake alipe kodi vizuri tu kisha uzeeni asifaidike na alichotoa, jamaa akaanza kula pensheni

Hivi visa havipo kutufurahisha ila ni mafunzo kwetu, mtume aliishi na majirani wasiokuwa waislam vipi aliishi nao, kila mmoja ni muwakilishi wa Uislamu, huenda mtu asisome msahafu wala hadithi za mtume ila akajifunza uislam kupitia wewe.
Watu wamekuwa brainwashed mnoo, elimu hawana, allah aliposisitiza elimu alikuwa na maana yake, baada ya adamu kuumbwa cha kwanza kupewa ni elimu, mtume alipokabidhiwa utume ilifata ni elimu.

Tujitahidi kusoma, mwenye elimu ataendelea nayo akiendelea kuitafuta, ila pindi anapoona katosheka ndio ujinga unapoanzia.
 
Laiti misimamo kama hiyo Zanzibar ingekuwa inafanywa kwenye vitu vingine kama matamasha mziki na mambo mengine ya hovyo katika jamii ambayo kinyume na Uislamu ningewapa kongole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…