Carnivora
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,650
- 6,015
M
Mke wangu anafanya kazi katika Kituo cha Afya. Kuna times ananiambia LEO WATEJA NI WENGI binafsi neno hili huwa linanikereketa.Mkuu kafiri maana yake ni kila asiyekuwa muislamu.
Kwa maana ni jina la jumla kwa kila asiyekuwa muislamu, badala ya uislamu kutamka dini zote ikaona iweke kwa ufupi tu kuwa wasiokuwa waislamu ni makafiri.
Hili jina linaonekana baya kwa sababu ya mindset zetu zimejengeka na tunalisikia likitajwa katika maeneo hatarishi.
Kama vile katika mambo ya kuuana utaskia anatajwa kaafiriii, mtu ataona hee kumbe kafiri hii ni jitu la kuuawa kabisa kumbe sivyo kabisa.
Hivyo kafiri ni jina la utambulisho kwa wasiokuwa waislamu mkuu.
Ni kama ukienda kwenye fani ya afya mgonjwa ataitwa mteja, utajiuliza kwamba mimi naumwa alafu naitwa mteja?
Kumbe Maana yake mteja ni mtu ambaye anakuja pale kutaka huduma.
Hivyo neno mteja ni jina la jumla kama ambavyo neno kafiri ni la jumla