Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Ujinga mtupu, yaani niache kula mchana kwa sababu ya dini ya mtu tena ya kuletewa? Siku nile aje mpuuzi eti aniulize kwanini nakula mchana haki ya nani huyo mtu aombe Mungu wake tu asiingie anga zangu. Atakula kichapo cha kufa mtu mpaka atajuta kuzaliwa.
Njoo znz ule hadharani mchana wa Ramadhan. Km wewe kweli mkereketwa
 
kati ya vitu ambavyo huwa vinanifanya nitamani tuachane na zanzibar, ni kuwachapa viboko wakristo ambao hawajafunga kula mchana, ni ukatili na ugaidi kabisa. hapo ndio huwa naiondoa kabisa zenji moyoni mwangu.
Sio kula mchana. Kula hadharani. Na Sio mwakristo tu hata waislam wanaokula hadharani wanachapwa vile vile. Mbona watu washazoea. Hapo tunakumbushana tu
 
Why mnafukuza na kuwafunga wananchi wanaokula wakati wao hawafungi?.

Wakati huo huo msaafu wenu unakutaka usionekane mbele za watu kama mtu aliyefunga!.
Hayo sio maswali ya kuniuliza mimi.

Inatakiwa uwaulize hao wanaofukuzA watu
 
Habarini za kutwa nyote.

Naomba niseme kwamba katika dini yetu ya uislamu hakuna pahala mtume kamkataza asiyekuwa muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna pahala qurani imekataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna sehemu wakati wa mtume imeonesha kwamba walikatazwa wasiokuwa waislamu wasile mchana wa ramadhani.

Katika masharti ya mtu kulazimika kufunga kwanza awe muislamu.

Kwa maana asiyekuwa muislamu hailazimiki kufunga,kama halazimiki kufunga maana yake ana uhalali wa kula mchana wa ramadhani kwa sababu sio muislamu.

Mtu anaweza akasema kwamba wamekatazwa wasile hadharani ?

Hadharani kwanza ni wapi kwa mujibu wa sheria ya dini ?

Watu wanakula kwenye migahawa hakuna anayekunywa chai na chapati anatembea pale kariakoo.

Hivyo kuhusu kula hadharani uislamu pia haujakataza kwa sababu neno hadharani ni pana katika muktadhwa huu.

Uislamu umekataza kwa muislamu ambaye hana udhuru wowote alafu akala mchana wa ramadhani,huyu anapata dhambi.

Lakini kuwakataza watu wasile mchana na kuwashambulia sio katika adabu za kiislamu kwa sababu

Kuna wagonjwa hawatakiwi kufunga.
Kuna wanawake wako kwenye siku
Kuna watoto
Kuna wazee
Kuna wasafiri
Kuna wasiokuwa waislamu

Hawa wote ruhusa kula mchana kwa mujibu wa ssheri ya uislamu wetu.

Sasa kama wanaruhusiwa kula mchana vipi wasiruhusiwe kula hadharani wakati hakuna katazo lolote la kula hadharani katika uislamu.

Allah anasema..

"Hakuna kulazimishana katika dini"

Asiye muislamu kumkataza asile mchana maana yake unamlazimisha akae na njaa jambo ambalo sheria ya dini imekataza.

Tutaheshimu sheria itakayowekwa na serikali lakini tunaomba sheria hizo zisinasibishwe na uislamu.

Ni bora uislamu ulaumiwe kwa sheria ambayo kweli imeiweka kama vile viboko kwa wazinifu n.k

Kuliko uislamu kulaumiwa kwa sheria ambayo haijaiweka kama hizi kukataza kula mchana wa ramadhani

Nakaribisha maswali.

Naomba kuwasilisha.
😍
 
Mimi ni mkristo lkn nawaheshimu waislamu kama ww ambao mnajielewa na ni watu wazuri sana Mungu azidi kukupa heri zake
 
Ona huyo [emoji1489]

Real IQ inahitajika.
Sasa shida ipo wapi Mr. real IQ, si ufafanue swali ulilouliza, ili nikufahamu uzuri.

Au real IQ yako imeishia kuuliza tu swali ambalo huwezi hata kulifafanua?

Labda IQ yangu ndogo, ndio maana nikakuuliza point yako ni ipi?
 
Msaada wandugu; hivi dhambi unapambana nayo uishinde au unaipiga marufuku isiwepo?.

Na utaonekana vipi mshindi endapo hakuna kitu unachotakiwa kukishinda?.
Dhambi lazima iwepo na uishinde ili kuongeza kiwango chako cha imani, na wanaoishinda dhambi kwetu wakristu hao ndio wataurithi ufalme wake.

Huwezi kwenda peponi kwa free pass.

Hiyo part two ya swali lako imekosa maana baada ya jibu la part one.
 
Msaada wandugu; hivi dhambi unapambana nayo uishinde au unaipiga marufuku isiwepo?.

Na utaonekana vipi mshindi endapo hakuna kitu unachotakiwa kukishinda?.
Kufanya mema na kuacha uovu ni mzani unaotakiwa kubalance.

Katika uislamu kunakuamrisha mema na kukataza maovu pia.

Hivyo mtu anatakiwa afanye mema na aache maovu, na wakati huohuo kukataza maovu ni wema na kuacha uovu utendeke ni uovu.

Zinaa ni dhambi, hivyo mtu hatakiwi kuzini na pia anatakiwa kukataza zinaa.

Sasa ukisema uovu uwepo ili watu waushinde, ni sawa na kusema watu wafanye maovu.

Hivyo nitakuuliza huyo anayetakiwa kufanya maovu ili yawepo ni nani?

Au ulikusudia nini uliposema kuwepo kwa dhambi?
 
wewe ndiyo muislamu original siyo wale wengine wamekalilishwa bila kujisomea,masuala yakwenda peponi kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe
 
Kufanya mema na kuacha uovu ni mzani unaotakiwa kubalance.

Katika uislamu kunakuamrisha mema na kukataza maovu pia.

Hivyo mtu anatakiwa afanye mema na aache maovu, na wakati huohuo kukataza maovu ni wema na kuacha uovu utendeke ni uovu.

Zinaa ni dhambi, hivyo mtu hatakiwi kuzini na pia anatakiwa kukataza zinaa.

Sasa ukisema uovu uwepo ili watu waushinde, ni sawa na kusema watu wafanye maovu.

Hivyo nitakuuliza huyo anayetakiwa kufanya maovu ili yawepo ni nani?

Au ulikusudia nini uliposema kuwepo kwa dhambi?
Hakuna sehemu nimesema 'dhambi' alafu unapaswa kutambua kuna watu ni waislam lakini wanakula kutokana na sababu mbalimbali, so nao ni dhambi?.

Haya christian akiwa anakula je?
 
Kafiri ni mtu yoyote yule asiye amini uwepo wa MUNGU au yule anae amini uwepo wa Miungu mingine zaidi ya MUNGU mmoja alieumba mbingu na nchi.

Hata kama anajiita ni muislamu ila kama anaamini na kuiomba/kuitegemea miungu mingine imtatulie shida zake zaidi ya MUNGU mmoja mfano mizimu, nyoka, majini n.k huyo pia anahesabika ni kafiri vile pia.

Swali: kwa nini waislamu wanawaita wakristo ni makafiri?

Jibu: sio matakwa yetu kuwaita hivyo ila Qur'ani tayari imeshaelezea ukafiri wa wakristo na imewetaja wakristo ni makafiri.

Swali: Ni upi haswa ukafiri wa Wakristo?

Jibu:
“Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja.” (al-Maida, 5/73).

“Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu. Sema: Ni nani mwenye kumiliki cho chote mbele ya Mwenyezi Mungu ikiwa Yeye angetaka kumuangamiza Masihi mwana wa Maryamu, na mama yake, na wote waliomo katika ardhi? Na mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ni vya Mwenyezi Mungu. Huumba apendavyo. Na Mwenyezi Mungu anao uweza juu ya kila kitu.” (al-Maida, 5/17)

“Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.” (al-Maida, 5/72).

Kama bado una swali lolote kuhusu ukafiri unaruhusiwa kuuliza.
Soma Al hajuraati 13
 
Hakuna sehemu nimesema 'dhambi' alafu unapaswa kutambua kuna watu ni waislam lakini wanakula kutokana na sababu mbalimbali, so nao ni dhambi?.

Haya christian akiwa anakula je?
Mr. Real IQ unaniangusha, mbona unaanza kuuliza maswali ambayo majibu yake yapo wazi.
Inamaana hata hii mada hujaielewa!?

Ndio maana nilikutaka ulifafanue swali lako ili twende sawa, ukaniona......
 
Back
Top Bottom