Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Njoo znz ule hadharani mchana wa Ramadhan. Km wewe kweli mkereketwa
Nilishafanya hivyo mwaka jana pale Forodhani, watu wakawa wananitizama na wengine wakaniuliza mbona sikufunga nikawaambia frankly mimi sifungagi hata siku moja naamini Mungu tu. Hapo hapo mbele kidogo nikaona jamaa mmoj dizaini ya mbugia unga anakula kichapo kwa kunywa chai saa tano ya asubuhi, wakawa wanasema eti ana tabia mbaya hafungagi, nikawashangaa sana. Yaani mnampiga mwenzenu kwa kuwa hataki kuwa mwendawazimu kama wengine? Zanzibar mlifanya mapinduzi ya nini, si mlitaka kuwa huru kutoka mikono ya makafiri (sultan na utawala wake wa kiarab)? Sasa mnarudi kule kule kunyanyasana kufuata dini isiyo na mantiki kwenu.
 
Hakuna sehemu nimesema 'dhambi' alafu unapaswa kutambua kuna watu ni waislam lakini wanakula kutokana na sababu mbalimbali, so nao ni dhambi?.

Haya christian akiwa anakula je?
Unajuwa tatizo la waislam wengi ni kwamba bado wanaishi kwenye karne ya 7 enzi za Mohammed, mtu anaulizwa a simple answer anashindwa kujibu mpaka aende kuchukua Quran aanze ku-refer/quote......yaani mtu anashindwa kutumia akili yake mwenyewe. Haya ndiyo matatizo ya kutokwenda shule na kuona madrasat ndiyo elimu ya maisha. Huwezi ishi maisha ya karne ya 7 kwa karne hii, never.
 
Sijui wewe ni dini gani, lakini kama dini yako inamaandiko(kitabu), hivi ukisema watu watumie akilizao kujibu masuala ya dini pasi na kurefer mafundisho ya dini, sasa kuna haja gani ya kuwepo hayo maandiko?

Na kama dini yenu inafanya hivyo, hapo mjinga( wa dini) ni yupi na mwenye elimu(ya dini) ni yupi? Maana kila mtu akili anayo, hivyo anaweza kuropoka lolote tu kwa upeo wake.

Na kuhusu kufuata mafundisho ya zamani, sijui labda uwe ni mfuasi wa Zumaridi, maana huyu ndio dini yake imeanza juzi, lakini dini nyingi mafundisho yake ni yazamani.

Hivyo hata wewe unaishi Karne ya 7 maana unafuata mafundisho ya zamani, kama hoja yako ndio hiyo.
 
Tukija upande wa uislamu.

Kwanza umetusingizia, sio kweli kwamba tunarefer Kila jambo katika Quran, tunafanya hivyo ikiwa jambo ni la dini, maana Quran ndio muongozo wetu, hivyo tunatumia akili zetu katika masuala ya dini kwa kufuata muongozo wa dini(elimu ya dini).

Hivyo ukiniuliza kuhusu pembejeo za kilimo wala sitofungua msaafu, lakini ukiniuliza jambo la dini kwa nini nitumiae kichwa kitupu?

Pili uislamu ni dini inayokwenda na wakati, hivyo inafaa katika kila nyakati na zama, kwa sababu sheria zake zimegusia kila nyanja ya maisha ima kwa kulitaja jambo moja kwa moja au kwa kuweka misingi ambayo hilo jambo litarejea hapo.

Hivyo hata kama jambo lilatokea kesho, basi uislamu ulishalitolea muongozo kwa misingi iliyowekwa.
 
Mkuu unazungumza kwa ujumla sana.
 
Wacha upuuzi kijana, Uislam si mwongozo wa maisha ya binadamu wote bali wale waarab wa karne ya 7. Utaishije maisha yako kama mtu wa karne ya 7? Na ndiyo maana watu wengi hapa tanzania wanaoshabikia Uislam hawana maendeleo yeyote zaidi ya kuwa wanafiki tu.
 
Si kweli hata kidogo, Uislam unamfanya mtu kuwa mnafiki mno, muongo, mfuga majini
 
Kuwa critical thinker kwenye uislam Ni Sawa Na Kuwa sharobaro kwenye Banda la mbuzi...
Anyways kongole kwako
 
Sahihi mkuu.

Bila akili tutachukua mawazo ya wasomi wa zamani kana kwamba sisi hatuishi kabisa na hatuna mawazo kabisa.
Mkuu sawa umeeleweka

Naomba nkulize swali, we dhehebu gani

Ova
 
Habarini za kutwa nyote.

Naomba niseme kwamba katika dini yetu ya uislamu hakuna pahala mtume kamkataza asiyekuwa muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna pahala qurani imekataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna sehemu wakati wa mtume imeonesha kwamba walikatazwa wasiokuwa waislamu wasile mchana wa ramadhani.

Katika masharti ya mtu kulazimika kufunga kwanza awe muislamu.

Kwa maana asiyekuwa muislamu hailazimiki kufunga,kama halazimiki kufunga maana yake ana uhalali wa kula mchana wa ramadhani kwa sababu sio muislamu.

Mtu anaweza akasema kwamba wamekatazwa wasile hadharani ?

Hadharani kwanza ni wapi kwa mujibu wa sheria ya dini ?

Watu wanakula kwenye migahawa hakuna anayekunywa chai na chapati anatembea pale kariakoo.

Hivyo kuhusu kula hadharani uislamu pia haujakataza kwa sababu neno hadharani ni pana katika muktadhwa huu.

Uislamu umekataza kwa muislamu ambaye hana udhuru wowote alafu akala mchana wa ramadhani,huyu anapata dhambi.

Lakini kuwakataza watu wasile mchana na kuwashambulia sio katika adabu za kiislamu kwa sababu

Kuna wagonjwa hawatakiwi kufunga.
Kuna wanawake wako kwenye siku
Kuna watoto
Kuna wazee
Kuna wasafiri
Kuna wasiokuwa waislamu

Hawa wote ruhusa kula mchana kwa mujibu wa ssheri ya uislamu wetu.

Sasa kama wanaruhusiwa kula mchana vipi wasiruhusiwe kula hadharani wakati hakuna katazo lolote la kula hadharani katika uislamu.

Allah anasema..

"Hakuna kulazimishana katika dini"

Asiye muislamu kumkataza asile mchana maana yake unamlazimisha akae na njaa jambo ambalo sheria ya dini imekataza.

Tutaheshimu sheria itakayowekwa na serikali lakini tunaomba sheria hizo zisinasibishwe na uislamu.

Ni bora uislamu ulaumiwe kwa sheria ambayo kweli imeiweka kama vile viboko kwa wazinifu n.k

Kuliko uislamu kulaumiwa kwa sheria ambayo haijaiweka kama hizi kukataza kula mchana wa ramadhani

Nakaribisha maswali.

Naomba kuwasilisha.
Nimependa ulivyoeleza bila kujali udini
 
Pamoja aisee

Karibu kwa swali lolote
Huu ufahamu uliowasilisha ni busara na hekima zako tu 'ufahamu wako' au ndivyo inavyotakiwa kuwa 'ufahamu sahihi'?

Je hali inajitofautisha kati ya Taifa la Kiislamu mfano: Mauritania na Taifa lenye mchanganyiko wa imani mbalimbali mfano: Burundi?
 
Wacha upuuzi kijana, Uislam si mwongozo wa maisha ya binadamu wote bali wale waarab wa karne ya 7. Utaishije maisha yako kama mtu wa karne ya 7? Na ndiyo maana watu wengi hapa tanzania wanaoshabikia Uislam hawana maendeleo yeyote zaidi ya kuwa wanafiki tu.
Unataka uniambie mpaka leo waislamu bado tunatumia ngamia na farasi kama chombo cha usafiri na tunawasiliana kwa njia ya barua zilizoandikwa kwenye ngozi?

Au nini maana ya kuishi kama Karne ya saba?
 
Huu ufahamu uliowasilisha ni busara na hekima zako tu 'ufahamu wako' au ndivyo inavyotakiwa kuwa 'ufahamu sahihi'?
Ufahamu sahihi una sifa zipi ndugu ?
Je hali inajitofautisha kati ya Taifa la Kiislamu mfano: Mauritania na Taifa lenye mchanganyiko wa imani mbalimbali mfano: Burundi?
Hali gani unaizungumzia...?
 
Back
Top Bottom