SoC02 Ujamaa(ubuntu) na ajira ya muda ni mkombozi wa uchumi wa Vijana kuelekea kwenye uchumi wa Kitaifa na kujitegemea

Stories of Change - 2022 Competition

Tibaiwa

Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
51
Reaction score
38
UTANGULIZI.

Ujamaa nitakaojikita nao ni (UBUNTU).

Rejea (Kamusi ya karne ya ishirini na moja 21 Toleo jipya uk wa 555)

Ubuntu ni mfumo katika jamii unaowawezesha wanajamii kuishi kwa kushirikiana katika kila jambo.

Ninaye rafiki yangu niliyepotezana naye muda mrefu kutokana na safari yangu ya kielimu, nilipokuwa kwenye pirikapirika zangu nilipigwa na butwaa nilipomkuta kwenye duka kubwa la nguo na kunisimulia kisa chake mpaka kuwa na hilo duka ninaloliona na kunivutia, ni upendo alioupata kwa jamaa yake aliyehishi naye nakuziona ndoto zake baada ya kutembeza bahasha kwa miaka mitatu bila kuambulia kitu kulinga na kile alichokisomea.

Rafiki yangu alinidokeza shauku yake ya kuendeleza mnyororo huo pale duka lake litakapozalisha duka lingine kwani hilo ni deni la kuupanua myororo kwa watu yaani kuwafanyia hisani vijana anaowaona na bahasha mkononi kwani alipitia magumu na Machungu.

Katika kupembua kwangu alichokivuna kutokana na shughuli hii ndani ya miaka miwili ni urahisi wa kujipatia mahitaji yake ya kimsingi kama vile chakula bora, mavazi nadhifu na kile anachodunduliza katika kulinda mtaji na faida anayoitunza ili kutimiza ndoto zake.(Tanzania tunaitaji sera ya ubuntu kwa maendeleo bila ya ubaguzi wa kikanda.

Kauli ya “uchawa” isifishe mazuri ya ujamaa kwani ikikua itadumaza watu kwa kuwabwetesha huku ikimfanya mwanaujamaa kujenga roho ya umimi na kuona kile alichonacho ni chake binafsi bila ya kufikiria wahitaji ndani ya jamii.

Mfano mwingine halisi wa ubuntu ni kitendo cha jamii yangu kujichanga mfukoni ili nipate Elimu ya juu na bila ya huo ujamaa pengine ningelikosa au ningechelewa kupata haya maarifa niliyonayo hadi sasa, vilevile nimeshuudia ujenzi wa miundombinu bora ya shule kutoka kwa watangulizi kwa kujishika pamoja mifukoni na wadau wengine wa kijamaa, hii ni ishara ya ukuzaji wa maendeleo kwenye ngazi ya kijamii.


AJIRA ZA MUDA KATIKA UKUZAJI UCHUMI WA KIJANA.

Katika kupunguza makali ya maisha kwa vijana yanayotokana na lundo la ukosefu mkubwa wa ajira ninaona suruhisho lake ni suala la uwepo kazi za muda kutoka Serikalini na taasisi binafsi kuliko kusubiria zile za kudumu.

Ajira hizi za muda hazitapunguza tu umaskini wa kupitiliza kwa vijana bali zitaendeleza kulinda taaluma za vijana na uwezo wao yaani zitawapatia uzoefu kazini bila ya kuwaacha tu mtaani huku maarifa yale waliyoyapata vyuoni yakiendelea kuwachachia ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona kijana anakosa kazi kwenye taasisi au kampuni kwa kigezo cha ukosefu wa uzoefu kazi, wakati ndio tu anatoka chuoni je kwanini uzoefu wa mafunzo kwa njia ya vitendo authaminiwi, taasisi zinasahau kuwa kupitia wao au kampuni mhitimu anaongeza huo uzoefu kulingana na maarifa aliyonayo kutoka chuoni, “ kila taasisi ikitumia kigezo cha uzoefu kazini na kuwatupilia mbali vijana, huo uzoefu wataupata wapi?”. Tuamini vyuo vyetu na wakufunzi tulionao ili nao waone umuhimu wa kuwaandaa vyema vijana ili wasiende kuwatia aibu na kuharibu taswira ya chuo.

(“”Itafana kila mwaka tasisi binafsi, kampuni au serikali ikituma maombi ya moja kwa moja vyuoni huku wakiomba majina ya wahitimu wanaofanya vizuri ili kuwapatia ajira za muda ili wapate kile cha kuanzisha maisha ya kujitegemea hapo baadae””) huku wakiwafanyia usaili (upimaji) wenye na wajiridhishe na uwezo wa hao vijana na kuzuia mianya ya kuchaguliwa kwa kujuana na rushwa.

Ajira ya muda itasaidia kuwanyanyua vijana wenye mitaji midogo katika kuikuza na kuwainua pale zitakapowalenga : mfano wa ajira ambazo zimewainua baadhi ya vijana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ni Zoezi la uandikishaji na usimamizi wa wapiga kura, zoezi la uadikishaji wa anwani za makazi zilizofanyika mwaka huu 2022, sensa ya idadi ya watu na makazi nimeona shauku ya vijana.


MKAKATI MWINGINE.

Nchi ya Tanzania inapaswa kuwa na ; “NYUMBA YA MALEZI” Kwa vijana wanaotoka vyuoni kutoka kila mkoa ikiwa ni kuwaandaa vijana watakao tekeleza ubuntu, Viongozi bora kimaadili na Wazalendo pia vijana wenye nguvu ya ushawishi na wabunifu, mfano Tanzania tangu tumepata uhuru bado hatujawa na vazi rasmi la nchi wakati tunao wabunifu na watu wenye ushawishi wa kutumia utandawazi kupitia mitandao ya kijamii katika kutangaza mitindo mbalimbali kutoka nje, wabunifu kutoka kwenye nyumba ya malezi wabuni vazi la taifa kwa watoto, vijana, watu wazima na wazee na zitengenezwe nchini na zipatikane kwa gharama nafuu (ili tumalize hitaji la mavazi nadhifu). Si haya tu ndiyo yatakuwa mafanikio tu kwa vijana bali itakuza maadili mema kwani kila kijana atatamani kuwa barozi mwema wa jamii yake na kuwa mtu wa mfano kwa kizazi kilichopo na kile kijacho. (Tanzania tunaitaji sera ya Ubuntu).

Nyumba ya malezi itoe wabunifu na wasanifu wa majengo. Yaani ramani ya nyumba kwa kila familia au mtanzania wa pato la chini, kati na juu kwa gharama zote hadi kukamilika ili tumalize hitaji la (makazi bora) huku serikali ikiratibu suala la bei elekezi za vifaa vya ujenzi na unafuu wa upatikanaji wake kulingana na eneo la kijiografia. (Twaweza kuwa wanaubuntu) kulingana na hali zetu za kimaisha mbali na utofauti uliopo kiuchumi yaani Viwango/ngazi. Mfano wa nyumba hizi za malezi zitumie mifumo ya “Big brother Afrika na “Big brother nigeria” kwani zimekuwa nguzo kubwa ya kuwaandaa vijana katika kubuni mawazo chanya yenye kuchagiza maendeleo ya vijana na mataifa yao kwa ujumla na kuzitangaza nchi zao na vivutio vilivyomo.

“Ubuntu uliokomaa unaweza pia kukuza uchumi wa nchi”
Mfano halisi wa ubuntu kupitia michezo.

Hapa nchini Tanzania kuna kituo cha televisheni kilichobuni wazo la “ nani zaidi ?” kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu ndani ya wiki mbili Timu (A) ilikusanya zaidi ya milioni mia moja na timu ( B) ilikusanya zaidi ya milioni hamsini kutoka kwa wanajamii. Serikali ikibuni mawazo kama haya ya ubuntu kulingana na vyanzo vya mapato vilivyopo, nchi yetu ya haiwezi kukosa Viwanda vya mavazi ya nguo rasmi, za kawaida na zile za kimichezo.

Bado nchi yetu ya Tanzania inahitaji utekelezaji wa sera ya ubuntu kuelekea kwenye kujitegemea kwani mshikamano wa pamoja katika kuinuana utakuza maendeleo kuanzia kwenye ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye familia hadi kufikia kwenye ngazi ya kitaifa.


(Picha kwa msaada wa mtandao). Katika kuonyesha nguvu ya ubunifu na ushawishi.​
 
Upvote 6
Sawa, bandiko zuri. Swali👇

Ndugu mwandishi umeshauri kuhusu ajira za muda mfupi . Je hizo ajira za muda mfupi ulizo shauri ziwe ni za muda gani ? mwaka, miaka , mwezi au miezi?
 
Hizi ziwe za muda mfupi kuanzia mwaka mmoja hadi mitatu (baada ya kutoka chuoni)
Mfano kama ni mwalimu (wa kujitolea) kama analipwa shilingi laki moja na nusu kwa alipwe elfu hamsini kwa ajiri ya kujikimu (inawezakuonekana ni ndogo) lakini huyu mhitimu atakuwa chini ya wazazi au walezi, huku laki moja ikiwekwa benki mpaka atakapomaliza mkataba wake kwa ajili ya kufanya kile kitu cha ndani yake.(ndoto)
Mwaka 1 = 1,200,000
Miaka. 2= 2,400,000
Mwaka wa 3= 3,600,000
Huku akipewa mtu sahihi wa kumwongoza kwa kile atakachokifanya ili asitapanye pesa ovyo kama kwake kiasi cha kuanzia milioni moja ni kikubwa pia atapata elimu juu ya changamoto atakazokumbana nazo na jinsi ya kuzitatua huku mwajiriwa huyu wa muda mfupi akitoa mwanya kwa wahitimu wengine.
 
Kwa nini isipitishwe sheria kuwa ajira zinapaswa kuwa ni za muda mfupi [ nacho maanisha ni kuwa muda wa kuhudumu wa mwajiriwa unapaswa kuwa mwisho miaka kumi alafu wanaajiriwa watu wengine. Kwenye nafasi zao ili kutatua tatizo la ajira miongoni mwa vijana nchini pamoja na kulinda taalumu za vijana wasomi zisiweze kupotea bure bila kuwa na manufaa katika nchi ] una maoni gani juu hiki nilicho nilicho andika?
 
"Wazo lako ni zuri na bora"
Ikipitishwa hii sheria ya kuajiri kwa muda nahisi hatutakuwa tena na ukosefu wa ajira au lundo kubwa tutakuwa tunapishana na kuwapatia fursa wengine huku kibindoni tukiwa na kile cha kuanzisha maisha ya kujitegemea. "Hii hiwe sera ya kitaifa" nachelea kusema hiwe kwenye mchakato wa kuwa sera kwasababu michakato inachelewasha sana maono ya kikombozi. Nashukuru sana.
 
Asante kwa maoni yako . Kidogo ninachoweza kuongeza . Mimi nadhani serikali yetu imekosa pia ubunifu mpya wa kimazo[ kitu ambacho ata wewe mtoa mada umezungumzia { swala la ubunifu }] . Serikali imeshindwa kabisa kuja na Mpango kazi utakao punguza au kokemesha kabisa swala la upungufu wa ajira nchini miongoni mwa vijana wasomi. Na hii yote naweza kusema ni kutokana na serikali kutowapa nafasi zaidi damu changa/ vijana katika vitengo mbalimbali ili waweze kutatua hili tatizo kwa kubuni mbinu mpya na iliyo bora ya kuajiri/ajira hapa nchini.
 
(Tunahitaji jumba la Malezi)
Serikali ilitambue kama hazina/Dhahabu ya ubunifu na maarifa. Huo ubunifu wao utekelezwe na si kuishia kwenye mafaili karatasi.
Je haya yote yanawafikiaje ili Suruhu ipatikane?
 
(Tunahitaji jumba la Malezi)
Serikali ilitambue kama hazina/Dhahabu ya ubunifu na maarifa. Huo ubunifu wao utekelezwe na si kuishia kwenye mafaili karatasi.
Je haya yote yanawafikiaje ili Suruhu ipatikane?
Suluhu inaweza kupatikana endapo serikali ikijifungua na kujiweka wazi kuruhusu mawazo mbadala na chanya ya kibunifu yatakayo leta matokeo chanya ndani ya jamii na taifa kwa ujumla . Je hili litawezekana kufanyika kwa namna gani? Hili litaweza kutekelezwa kwa serikali kuandaa mihadhara mbalimbali ya kisomi katika ngazi ya elimu ya upili na katika ngazi ya elimu ya chuo kikuu . Kwa kuwa wasomi wapatikano katika hizi ngazi mbili ndio haswa wabunifu na watendaji. serikali ikijifungua na kujiunganisha na wasomi na wadau mbalimbali wapatikanao katika hizi ngazi mbili hakika jumba la ubunifu litaendelea kutunzwa kwa kuwa litaendelea kuzalisha watu sahihi katika muda sahihi na wenye ubunifu na ujuzi wa kufanya usahihi wa kazi na hakika ubunifu hautaishia kwenye makaratasi .

-Serikali inatakiwa kufunga ndoa ya ushirikiano uliothabiti na hizi ngazi mbili [ Elimu ya upili na Elimu ya chuo kikuu ] na yenyewe kusimama Kama mlezi na mtunza jumba la ubunifu upatikano katika hizi ngazi mbili [ wasomi na wadau mbalimbali ] . Hakika taifa litakuwa katika mikono salama ya kibunifu kwa manufaa na maendeleo ya sekta mbalimbali na taifa kwa ujumla.
 
Tatizo linakuja pale watawala wanapotanguliza uchama katika mambo ya msingi km haya. Pia sisi km vijana tunakuwa nyuma kuungana na kutengenezs kitu cha kuishawishi serikali.mm ningependekeza kuwe na jukwaa huru la vijana ambalo litapeleka presha km hiz kwa serikali mawazo km haya ni muhimu sana kwa taifa letu.sema nn vijana waliosoma wako nyuma sana katika kuihimiza serikali juu ya matakwa yao
 
Umenena vyema ndugu, Majukwaa hayapo na ukiwafata ofisini utaulizwa wewe ni nani?? Swali hili na foleni ya kuja kuwaelewesha na kukubali pamoja karatasi zetu kuzikuta zimefungia vitumbua vya chai yao vinakatisha tamaa na kukiambia kielehele chako kikome, huku ukisubiri nafasi ya utekelezaji wewe mwenyewe na kuishia kwenye ndoto za abunuasi.
 
Nadhani ni dhana potofu kwa jinsi ninavyoona mimi

Unapo bundle people together tayari unaleta limitations

Cha kwanza na paramount ni individuals kwanza....jamii kama group inakuja baadae

Kila mwanadamu anatakiwa kua huru kujiamulia atakavyo kuyakabili maisha yake

Uhusiano wa mwanadamu mmoja na mwingine inatakiwa iwe purely win-win transactional,yaani una ninachotaka na mimi nina unachotaka,hivyo mutually tusaidiane kubadilishana

Ubuntu ni kwamba alienacho anaweza gawa freely kwa yeyote bila reciprocation which makes this system myopic na not endelevu in reality.

Nadhani human being kama individual akae katikati ya jamii kwanza,then jamii ikae nje,huyu mtu awe totally free to think and create for him/herself following the social and legal systems they have agreed upon and applied to everybody equally.

Huu ushenzi wa jamii kua superior zaidi ya individual person ni another useless and not practical system

Infact jamii most definitely hua wrong more often than an individual maana jamii ina wajinga wengi kushinda wenye akili,na group lenye wajinga wengi ni hatari kushinda kitu chochote

Matako ya Ubungu na ujamaa wa kipumbavu...waacheni watu wawe free,totally free then muone kama hawatayaweza maisha............

Grouping and bundling of people is another human tragedy....Nyerere na washenzi wenzie walifeli and still motherfvckers dont understand!
 
Tumia akili katika kufikiri na kupembua mambo.
1. Kwanini watu uchangishana kwenye harusi, misiba na kwenye majanga mbali mbali (kwanini kuna foundation)
2. Kwanini timu ya mpira wa miguu ina wachezaji 11 na wa akiba mbali na washangiliaji na benchi la ufundi.
3. Kwanini anayewaza kutengeneza gari halitengezezi peke yake mpaka kukamilika.
4. Kwanini kiwanda akiwi na run mmoja.
Nimetumia mifano ya kitoto kukufumbua uwezo wako wa kufikiri
"Rejea vizuri andiko" na upembue maana ⛓️⛓️⛓️⛓️⛓️⛓️ chain myororo.
 
Ni nani aliyeingia kwenye uwanja wa vita na kushinda peke yake bila ya kuwa na jeshi imara
Utasema "Daudi" kuna maendeleo ya one against one na yale yanayohitaji nguvu ya pamoja.
 
Tumia lugha ya kufaa kwenye machapisho ya heshima Kama haya ya mwandishi. Lugha chafu na zisizofaa zinashusha heshima yako, akili zako na kile ulichokusudia kufikisha Kama ujumbe . Kama hauwezi kuchangia kwa lugha zenye heshima ni bora ukasoma chapisho na kubonyeza kitufe cha "thanks" au “Nzuri” Kama unakubaliana na mtoa chapisho na unaweza pia kubonyeza kitufe cha “dislike” Kama haukubaliani na mtoa chapisho . Ni hivyo tu ninaweza kusema.
 
Umenena vyema
Katumia lugha ya maudhi bila kubainisha hoja yake ya msingi katika kukosoa na kuboresha.
 
Mkuu naona unajipa moral high ground

Yaani wewe ni clean sana in such a way upo humu kuwaelekeza watu wazima kama wewe waongee vipi na kwa namna gani

Mbona umejipa kazi ngumu sana na kwanza sio ya kwako....wewe jielekeze wewe mwenyewe nini cha kuongea na kuongea vipi sio mimi au mtu mwingine maana you have no authority on them.

Utasema unatoa ushauri,I didnt request your ushauri services,thank you very much!

Wewe kama umekasirika sana na "matusi" of which there aren't,then pasuka and Im sorry sana I cant help you.

Kama hujaona hoja yeyote kwenye post yangu then ni vizuri usinge hata isoma,ungeachana nayo maana ni uchafu...

Nimetoa hoja zangu,nimeziwakilisha ninavyotaka mimi sio wewe unavyotaka,hukuzitaka too bad I cant help you with hizo hasira zako!
 
Umenena vyema
Katumia lugha ya maudhi bila kubainisha hoja yake ya msingi katika kukosoa na kuboresha.
Lugha isiyo na maudhi ni ipi wandugu?

Lugha ambayo haikusifii au kukubaliana na wewe unaiita ya "maudhi"?Tupe universal definition maana nyie vichwa vyenu vina predefined meanings za lugha ya staha to your biases and favours then mnataka ku-impose to others?

Yaani mnataka muongelewe kwa lugha tamu zenye mrengo wa kupendwa na nyie?Like really?

Too bad aisee,I cant help you people.....I release my shyt I dont care whoever catches it!
 
Sijasema sijaona hoja yoyote kutoka kwako Ila, lugha za matusi ulizo tumia hapa sio mahali pake. Wasilisha ujumbe wako kwa lugha inayofaa mbona utaeleweka tu mkuu. Lakini matusi hayasaidii kitu , Jambo la muhimu na la busara kwa mtu mzima ni kuwa “UKIJIHESHIMU UTAHESHIMIKA USIPO JIHESHIMU UTADHARAULIKA”.
 
1. Kwanini watu uchangishana kwenye harusi, misiba na kwenye majanga mbali mbali (kwanini kuna foundation)
Kuchangia kwenye harusi na misiba nk ni predominantly happen to poor countries.

Ni tabia mojawapo wa jamii masikini

Hizi tabia za personal issues ku transfer into a society ni tabia predominantly to very poor societies

Ni tabia mbaya ya kinyonyaji kuhamishia matatizo au shughuli za kwako na kuigeuza ni shughuli ya wana jamii nzima ndio wabebe huo mzigo.

Stop this nonsense
2. Kwanini timu ya mpira wa miguu ina wachezaji 11 na wa akiba mbali na washangiliaji na benchi la ufundi.
Team ya mpira ni organized sport with everyone involved has specific role and get compensated accordingly

Infact sport ni larger system of each individual accountabilities and each is getting rewarded or punished kutokana na jasho lake.

Hakuna team kama hakuna kazi ya mmoja mmoja individually organized in a specific defined framework

Huwezi fananisha hii organized sport na stupidity ya ujamaa ambapo 80% of the members ni zero members eating jasho la 20%
Haya mengine yoooote ni upumbavu unaorudia ule ule..Hujui maana ya mifumo ya kijamii ku-organize themselves to run their daily social life kama capitalism au communism au socialism na mfumo mahususi wa kufanya jambo/process ili itoke output

Unachanganya the two different concepts....Hebu rudi usome zaidi then uje hapa tena.

Binadamu ni mtu anaepambana maisha yake yote kua huru na mwenye furaha....unapovunja vitu hivi viwili kumlazimisha afate group la wanadamu wengine lenye limitations ndio hapo mifumo yenu yote inapofeli inabakia capitalism tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…