UTANGULIZI.
Ujamaa nitakaojikita nao ni (UBUNTU).
Rejea (Kamusi ya karne ya ishirini na moja 21 Toleo jipya uk wa 555)
Ubuntu ni mfumo katika jamii unaowawezesha wanajamii kuishi kwa kushirikiana katika kila jambo.
Ninaye rafiki yangu niliyepotezana naye muda mrefu kutokana na safari yangu ya kielimu, nilipokuwa kwenye pirikapirika zangu nilipigwa na butwaa nilipomkuta kwenye duka kubwa la nguo na kunisimulia kisa chake mpaka kuwa na hilo duka ninaloliona na kunivutia, ni upendo alioupata kwa jamaa yake aliyehishi naye nakuziona ndoto zake baada ya kutembeza bahasha kwa miaka mitatu bila kuambulia kitu kulinga na kile alichokisomea.
Rafiki yangu alinidokeza shauku yake ya kuendeleza mnyororo huo pale duka lake litakapozalisha duka lingine kwani hilo ni deni la kuupanua myororo kwa watu yaani kuwafanyia hisani vijana anaowaona na bahasha mkononi kwani alipitia magumu na Machungu.
Katika kupembua kwangu alichokivuna kutokana na shughuli hii ndani ya miaka miwili ni urahisi wa kujipatia mahitaji yake ya kimsingi kama vile chakula bora, mavazi nadhifu na kile anachodunduliza katika kulinda mtaji na faida anayoitunza ili kutimiza ndoto zake.(Tanzania tunaitaji sera ya ubuntu kwa maendeleo bila ya ubaguzi wa kikanda.
Kauli ya “uchawa” isifishe mazuri ya ujamaa kwani ikikua itadumaza watu kwa kuwabwetesha huku ikimfanya mwanaujamaa kujenga roho ya umimi na kuona kile alichonacho ni chake binafsi bila ya kufikiria wahitaji ndani ya jamii.
Mfano mwingine halisi wa ubuntu ni kitendo cha jamii yangu kujichanga mfukoni ili nipate Elimu ya juu na bila ya huo ujamaa pengine ningelikosa au ningechelewa kupata haya maarifa niliyonayo hadi sasa, vilevile nimeshuudia ujenzi wa miundombinu bora ya shule kutoka kwa watangulizi kwa kujishika pamoja mifukoni na wadau wengine wa kijamaa, hii ni ishara ya ukuzaji wa maendeleo kwenye ngazi ya kijamii.
AJIRA ZA MUDA KATIKA UKUZAJI UCHUMI WA KIJANA.
Katika kupunguza makali ya maisha kwa vijana yanayotokana na lundo la ukosefu mkubwa wa ajira ninaona suruhisho lake ni suala la uwepo kazi za muda kutoka Serikalini na taasisi binafsi kuliko kusubiria zile za kudumu.
Ajira hizi za muda hazitapunguza tu umaskini wa kupitiliza kwa vijana bali zitaendeleza kulinda taaluma za vijana na uwezo wao yaani zitawapatia uzoefu kazini bila ya kuwaacha tu mtaani huku maarifa yale waliyoyapata vyuoni yakiendelea kuwachachia ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona kijana anakosa kazi kwenye taasisi au kampuni kwa kigezo cha ukosefu wa uzoefu kazi, wakati ndio tu anatoka chuoni je kwanini uzoefu wa mafunzo kwa njia ya vitendo authaminiwi, taasisi zinasahau kuwa kupitia wao au kampuni mhitimu anaongeza huo uzoefu kulingana na maarifa aliyonayo kutoka chuoni, “ kila taasisi ikitumia kigezo cha uzoefu kazini na kuwatupilia mbali vijana, huo uzoefu wataupata wapi?”. Tuamini vyuo vyetu na wakufunzi tulionao ili nao waone umuhimu wa kuwaandaa vyema vijana ili wasiende kuwatia aibu na kuharibu taswira ya chuo.
(“”Itafana kila mwaka tasisi binafsi, kampuni au serikali ikituma maombi ya moja kwa moja vyuoni huku wakiomba majina ya wahitimu wanaofanya vizuri ili kuwapatia ajira za muda ili wapate kile cha kuanzisha maisha ya kujitegemea hapo baadae””) huku wakiwafanyia usaili (upimaji) wenye na wajiridhishe na uwezo wa hao vijana na kuzuia mianya ya kuchaguliwa kwa kujuana na rushwa.
Ajira ya muda itasaidia kuwanyanyua vijana wenye mitaji midogo katika kuikuza na kuwainua pale zitakapowalenga : mfano wa ajira ambazo zimewainua baadhi ya vijana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ni Zoezi la uandikishaji na usimamizi wa wapiga kura, zoezi la uadikishaji wa anwani za makazi zilizofanyika mwaka huu 2022, sensa ya idadi ya watu na makazi nimeona shauku ya vijana.
MKAKATI MWINGINE.
Nchi ya Tanzania inapaswa kuwa na ; “NYUMBA YA MALEZI” Kwa vijana wanaotoka vyuoni kutoka kila mkoa ikiwa ni kuwaandaa vijana watakao tekeleza ubuntu, Viongozi bora kimaadili na Wazalendo pia vijana wenye nguvu ya ushawishi na wabunifu, mfano Tanzania tangu tumepata uhuru bado hatujawa na vazi rasmi la nchi wakati tunao wabunifu na watu wenye ushawishi wa kutumia utandawazi kupitia mitandao ya kijamii katika kutangaza mitindo mbalimbali kutoka nje, wabunifu kutoka kwenye nyumba ya malezi wabuni vazi la taifa kwa watoto, vijana, watu wazima na wazee na zitengenezwe nchini na zipatikane kwa gharama nafuu (ili tumalize hitaji la mavazi nadhifu). Si haya tu ndiyo yatakuwa mafanikio tu kwa vijana bali itakuza maadili mema kwani kila kijana atatamani kuwa barozi mwema wa jamii yake na kuwa mtu wa mfano kwa kizazi kilichopo na kile kijacho. (Tanzania tunaitaji sera ya Ubuntu).
Nyumba ya malezi itoe wabunifu na wasanifu wa majengo. Yaani ramani ya nyumba kwa kila familia au mtanzania wa pato la chini, kati na juu kwa gharama zote hadi kukamilika ili tumalize hitaji la (makazi bora) huku serikali ikiratibu suala la bei elekezi za vifaa vya ujenzi na unafuu wa upatikanaji wake kulingana na eneo la kijiografia. (Twaweza kuwa wanaubuntu) kulingana na hali zetu za kimaisha mbali na utofauti uliopo kiuchumi yaani Viwango/ngazi. Mfano wa nyumba hizi za malezi zitumie mifumo ya “Big brother Afrika na “Big brother nigeria” kwani zimekuwa nguzo kubwa ya kuwaandaa vijana katika kubuni mawazo chanya yenye kuchagiza maendeleo ya vijana na mataifa yao kwa ujumla na kuzitangaza nchi zao na vivutio vilivyomo.
“Ubuntu uliokomaa unaweza pia kukuza uchumi wa nchi”
Mfano halisi wa ubuntu kupitia michezo.
Hapa nchini Tanzania kuna kituo cha televisheni kilichobuni wazo la “ nani zaidi ?” kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu ndani ya wiki mbili Timu (A) ilikusanya zaidi ya milioni mia moja na timu ( B) ilikusanya zaidi ya milioni hamsini kutoka kwa wanajamii. Serikali ikibuni mawazo kama haya ya ubuntu kulingana na vyanzo vya mapato vilivyopo, nchi yetu ya haiwezi kukosa Viwanda vya mavazi ya nguo rasmi, za kawaida na zile za kimichezo.
Bado nchi yetu ya Tanzania inahitaji utekelezaji wa sera ya ubuntu kuelekea kwenye kujitegemea kwani mshikamano wa pamoja katika kuinuana utakuza maendeleo kuanzia kwenye ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye familia hadi kufikia kwenye ngazi ya kitaifa.
(Picha kwa msaada wa mtandao). Katika kuonyesha nguvu ya ubunifu na ushawishi.

Upvote
6