Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Habari.
Juzi kati nilikuwa nasoma na Kufasiri kitabu cha Karl Marx na Friedrich Engels, The Communist Manifesto. Kwenye kitabu hicho Marx anaeleza hatua hususa za ukuaji wa makabwela hadi kuja kuuondoa ubepari.
Anasema kuwa ulianza ukabaila. Katika huu ukabaila kulikuwa na wajasiriamali wa mijini ambao polepole wakaanza kupokonya nguvu za makabaila. Hawa wajasiriamali walipokua na kukomaa ndiyo wakaja kuwa mabepari.
Mabepari hawa hawakujali kitu zaidi ya faida. Waliwanyonya watu vibaya sana ili kukuza mitaji na kupata faida. Walau watwana wa enzi za ukabaila waliweza kuishi, makabwela waliotokana na ubepari walikuwa na hali mbaya sana. Hivyo anasema mwishowe makabwela watawatoa mabepari kwa nguvu na kuunda jamii isiyo na matabaka. Anasema mapinduzi ya makabwela yanakua polepole yakifuata mlolongo huu.
Sasa kwenye sehemu moja (Critical-utopian socialism and communism) anaeleza kuwa kuna watu, kabla hata makabwela hawajakomaa na kuweza kuwaondoa mabepari kama ilivyo ada, wao wanataka kuunda jamii isiyo na matabaka hewani tu.
Anasema ni waota ndoto ambao wanafikiri kwa kutumia maarifa wanaweza kuunda jamii ya kijamaa isiyo na matabaka bila kupitia hatua husika. Anadai kwa kufanya hivyo wanalazimika kukubaliana na mambo fulani ya mabepari, hivyo wanachounda kinakuwa siyo ujamaa wa kweli. Na pia wanazizimisha harakati zozote za makabwela kwa madai kuwa wanaunda jamii bora.
"Kwa hiyo basi, watu hawa wanapinga harakati zote za kisiasa, na hasa harakati za kimapinduzi; wanataka kufikia malengo yao kwa njia ya amani, na mipango ambayo hatma yake ni kushindwa, na kwa kutengeneza njia kwa ajili ya injili mpya ya kijamii."
Anadai ujamaa wa aina hiyo hatima yake ni kushindwa.
Ukiangalia utaona hii inafanana sana na ujamaa aliotaka kuunda Nyerere. Hakutaka kuacha makabwela wakue kwa ukuaji wao wa kiasili, alitaka kuunda jamii ya kijamaa kutokana na maono yake. Pengine ndiyo maana ulifeli.