Habari.
Juzi kati nilikuwa nasoma na Kufasiri kitabu cha Karl Marx na Friedrich Engels, The Communist Manifesto. Kwenye kitabu hicho Marx anaeleza hatua hususa za ukuaji wa makabwela hadi kuja kuuondoa ubepari.
Anasema kuwa ulianza ukabaila. Katika huu ukabaila kulikuwa na wajasiriamali wa mijini ambao polepole wakaanza kupokonya nguvu za makabaila. Hawa wajasiriamali walipokua na kukomaa ndiyo wakaja kuwa mabepari.
Mabepari hawa hawakujali kitu zaidi ya faida. Waliwanyonya watu vibaya sana ili kukuza mitaji na kupata faida. Walau watwana wa enzi za ukabaila waliweza kuishi, makabwela waliotokana na ubepari walikuwa na hali mbaya sana. Hivyo anasema mwishowe makabwela watawatoa mabepari kwa nguvu na kuunda jamii isiyo na matabaka. Anasema mapinduzi ya makabwela yanakua polepole yakifuata mlolongo huu.
Sasa kwenye sehemu moja (Critical-utopian socialism and communism) anaeleza kuwa kuna watu, kabla hata makabwela hawajakomaa na kuweza kuwaondoa mabepari kama ilivyo ada, wao wanataka kuunda jamii isiyo na matabaka hewani tu.
Anasema ni waota ndoto ambao wanafikiri kwa kutumia maarifa wanaweza kuunda jamii ya kijamaa isiyo na matabaka bila kupitia hatua husika. Anadai kwa kufanya hivyo wanalazimika kukubaliana na mambo fulani ya mabepari, hivyo wanachounda kinakuwa siyo ujamaa wa kweli. Na pia wanazizimisha harakati zozote za makabwela kwa madai kuwa wanaunda jamii bora.
"Kwa hiyo basi, watu hawa wanapinga harakati zote za kisiasa, na hasa harakati za kimapinduzi; wanataka kufikia malengo yao kwa njia ya amani, na mipango ambayo hatma yake ni kushindwa, na kwa kutengeneza njia kwa ajili ya injili mpya ya kijamii."
Anadai ujamaa wa aina hiyo hatima yake ni kushindwa.
Ukiangalia utaona hii inafanana sana na ujamaa aliotaka kuunda Nyerere. Hakutaka kuacha makabwela wakue kwa ukuaji wao wa kiasili, alitaka kuunda jamii ya kijamaa kutokana na maono yake. Pengine ndiyo maana ulifeli.
Karl Marx alikuwa Sahihi kwa sehemu...
Kuna namna, Ujamaa pasi kufika katika vilele vya ubepari ni 'kugawana umaskini'...
Mwalimu Nyerere, akiwa ni mtu wa visomo na dhamira ya dhati kutokomoeza sura ya 'matabaka' na pia 'harakati za kimahadhi ya jamii', alichokifanya ni mwanzo tu mchakato wa 'dawa'...
Mwalimu Nyerere, alianza na awamu ya kwanza ya ukombozi -- namna ya pendekezo kwa elimu inayolandana ama tuseme yenye kujinasibu na kule kukabiliana na maadui watatu katika ustawi wa umma: 'Ujinga, Maradhi na Umaskini'.... Hii ni imetupatia muktadha wa visomo na Elimu 1.0...
Kuna namna nyingine ya kufanya visomo iliyo ni Elimu 2.0, hii ndiyo inayosubiriwa...
Chama cha Mapinduzi, hakikuitwa hivyo kwa makosa... Na wala haikua 'bahati mbaya' kwamba maudhui ya katiba ya nchi, ya mwaka 1977, yanaakisiana na yale ya katiba ya Taasisi hii-- iliyo ni chombo cha umma kwa madhumuni na muktadha na michakato ya demokrasia ya Uwakilishi...
Itazame katiba yetu kwa makini, angalia ni jinsi gani inavyotaasisha dola kwa kusudi kuu la 'nchi ya usawa' kupitia 'Siasa za Ujamaa na Kujitegemea'... Kwamba, nchi iwe na sera zinaongozea utendaji wa kiserikali wenye kubudi kuakisi, miongoni mwa mengine kadhaa, yafuatayo:-
- 'Maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja';
- 'Kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake';
- 'Aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini';
- 'Matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi';
- 'Shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinaweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi';
- Nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya DEMOKRASIA na UJAMAA.
Chama cha Mapinduzi, ndicho yapaswa kiwe mdau, mletaji na msukuma mbele wa 'harakati za Mapinduzi'--na mapinduzi yanayosubiriwa ni yale ya 'kifikra'; kwa hiyo--Uwe ni mtu wa imani na subira; Kumchinja kobe kunahitaji 'taimingi'; na mapinduzi hayatatangazwa kwenye luninga... Yaone yote unayoyafikiri unaweza kuyaona na kubaini 'uadilifu' ama 'upotofu wa mambo' -- ya Chama hiki, tangu kilipoanzishwa hadi leo hii; lakini ni vema uwe na 'akiba ya maneno'...
Kwa hivyo, Chama cha Mapinduzi, ni chombo cha Agano na Azimio kwa Usoshalisti wa Kiafrika... Hiki si Chama kwa ajili tu ya ule muakisiko wa Machaguo yetu kitaasisi katika ngazi na madaraja ama madaraka kwa hatamu kidola... Chama cha Mapinduzi kikianguka, nguzo imara ya Mapinduzi Makubwa barani Afrika na hata dunia nzima itakuwa imetikiswa...
Ni labda tu, hata kwa juu juu hata wanachama wa hiki Chama kwa uwingi na umaarufu wake, hawazingatii shauri na azimio kuu ya kiitikadi ya Chama Tawala iliyo ni 'Mapinduzi'... Kwamba Chama hichi ni mshirika kwa 'Wanamapinduzi wote'--wa ndani na nje ya nchi...
Mapinduzi ni ujasiri katika nia na vitendo; vile vitendo vya kuachana na mifumo inayogawa wanajamii, na kuipa nafasi ile inayounganisha watu katika kuwatendea haki-sawa kwenye kuyafaidi mema ya nchi...
Kwa hivyo, tunafahamu Chama hiki alama yake ni 'Jembe na Nyundo'--kwamba hiki ni Chama cha Wakulima na Wafanyakazi... Lakini hivi ni kwa kuwa chama kilipoasisiwa, sura yetu ya kiustawi na nasibu ya maendeleo ilikuwa ni katika kuona ile 'hesabu' yetu, kwamba, taifa changa la Tanzania lilikuwa likijipambanua kwa michakato ya maendeleo vijijini zaidi kuliko mjini... Ardhi ikiwa ni rasilimali yetu ya msingi sana...
Mwalimu alipopendekeza tuwe na mikondo yetu wenyewe ya maarifa, tawala na mipango--ule mwanzo hasa wa kwa mfano, kuanzishwa kwa taasisi ya mafunzo ya mipango vijijini -mwishoni mwa miaka ya 70, kimsingi ni kwa kuwa ilikuwa dhahiri--maendeleo ya taifa ni zaidi ya 'Siasa za Nchi', kwa hivyo mipango ya maendeleo kwa mjini na vijijini inayo ufunguo wa upande wa pili kwa 'ujumuishi wa kheri na nafaka' ya nchi... Yote mawili hayatimii basi kuwa na jamii ilijijengea uwezo kifikra, tabia zinazofaa/rafiki kwa maendeleo ya pamoja na utamaduni.
Hili la 'Chuo cha Mipango' ndilo kwa mfano, limejibu "'Maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja'"... Kazi ikiendelea hata hivi sasa...
Basi fikiria kana kwamba, mapambano bado yanaendelea, Chama cha Mapinduzi unachokijua leo ni CCM 1.0--Ili uje kuibaini imekuwa CCM 2.0 basi ujue jicho lako litaanza kubaini kule kuwasili kwa sura ya 'uchumi tofauti' na huu uliotamalaki leo... Na basi, hata ujuzi na umahiri wetu kielimu utaanza kuwa tofauti... Elimu 2.0 kuhusika...
Akina Karl Max, na hata wafikirifu wengi tu wa mambo ya uchumi na siasa wamekuwa wakitumia Elimu 1.0... Kuna ukomo wa Kiuono na tafsiri katika sura na mienendo ya jamii...
Je, utawatambuaje wanamapinduzi? Hawa utawang'amua kwa wepesi wao; ule wa hao kuweza kuona namna ya kuliendea jambo kwa jicho la kibepari na vilevile jicho la kiujamaa bila shida, na basi wakaonesha 'njia ya katikati'... Kwa hivyo kiufundi, Karl Marx alikuwa ukingoni mwa kupindukia katika Elimu 2.0--lakini hakufika... Ndivyo basi yeye alidhani kimoja kitamsubiri mwenzake...
Mchawi wa Kukwama kwetu ni 'tabia'... Kwa hivyo, kaa ukijua Elimu 2.0 ni maarifa ya ujuzi wa kujua kupanga na kuchagua kwa 'daraja la kiroho'...
Elimu 1.0, japo yaweza kututoa tongotongo--hii ni bado ni kile Yesu alikitaja kama
adha ya kipofu kumuongoza kipofu mwenzake... Haina kinga dhidi ya fitina, husda, ulafi, unafiki, uchawa, uzandaki n.k katika muktadha wowote wa machaguo ya kitaasisi, wakati, jamii na matukio...
Elimu 2.0 italeta jibu juu ya lile jambo ambalo elimu 1.0 haiwezi kujibu; jambo lililotaasishwa na katiba yetu: "Shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinaweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi"
Itoshe kwa hapa kukazia neno, katiba ya nchi iliyopo sasa si 'kikwazo' kwa maendeleo, kudai eti hailandani na ulimwengu wa utandawazi. Umma usiojiongeza kumudu kubaini ukweli wa mambo unaweza kuyumbushwa na 'pepo za kupita'; lakini kumbe ni vema wanajamii wawe na vina vya upeo na maarifa sahihi... Elimu 2.0 si kisomo cha darasani, lakini hii 'yakamilisha' hekima ya mtu yeyote--mjinga na mwerevu... Kwa kuwa kila mtu ana ujinga na werevu wake, lakini si kila mtu anahekima juu ya jambo litendekalo katika jamii kwa minajili ya 'machaguo ya kitaasisi, wakati, jamii na matukio'....
Hmmm