Ujasusi Kwa mtu binafsi katika shughuli za kila siku

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UJASUSI KWA MTU BINAFSI KATIKA SHUGHULI ZA KILA SIKU.

Anaandika, Robert Heriel
Jasusi wa kujitegemea.

Dondoo
• maana ya ujasusi
• Ujasusi Kwa mtu Binafsi
• manufaa ya ujasusi Kwa mtu binafsi

Lengo kuu la andiko
• Mwisho wa Andiko msomaji atapata maarifa na ufahamu katika namna ya kupanga mipango, kutekeleza, na kuifanikisha; Kujilinda na kuwa salama na Amani.

Binadamu Kwa asili ni mbinafsi. Hulka hiyo ndio huwa chanzo kikuu cha migogoro mingi katika maisha ya watu wengi.

Furaha ni kiini cha maisha ya binadamu. Hata hivyo furaha hutofautiana Kati ya mtu mmoja na mtu mwingine. Hiyo hufanya maslahi ya watu kutofautiana.

Lakini upatikanaji wa furaha hizo ambazo ndio malengo ya wengi pia hutofautiana baina ya mtu mmoja na mtu mwingine hii inachangiwa na sababu/factors mbalimbali ikiwemo.

I. Utofauti wa Akili baina ya mtu mmoja na mtu mwingine,
ii. Utofauti wa uthubutu na ujasiri
iii. Utofauti wa Mazingira
iv. Utofauti wa muda, ikiwemo muda wa kufanya maamuzi na kutenda.
v. Utofauti wa wahusika wanaotuzunguka.
Unaweza kuwa na akili lakini ukazungukwa na watu wajinga, au unaweza kuwa mjinga Ila ukazungukwa na watu wenye akili. Au unaweza kuwa mjinga na ukazungukwa na wajinga wenzako. Halikadhalika na wenye akili.
Au ukazungukwa na watu wenye vipato vya chini au watu wenye vipato vya juu.

vi. Elimu, Ujuzi na maarifa.

Mambo hayo ndio hufanya watu tuwe tofauti katika kutimiza malengo yetu. Hivyo basi katika kutimiza Jambo lolote itakupasa uzingatia pia mambo hayo hayo hapo juu.

Jambo moja unalotakiwa kujua kile unachofikiri kichwani mwako ni cha thamani, muhimu na kinahitaji ulinzi mkali ndio maana Mungu muumbaji alitufanya tusijue mtu mwingine anafikiria nini kichwani mwake. Jambo Hilo pekee lingekufanya ujue kuwa Dunia sio sehemu Salama.

UJASUSI
Ujasusi unahusu taarifa. Upatikanaji, uchambuzi, uchakataji, utunzaji na utekelezaji wa taarifa.

Tunafahamu kuwa mipango, mbinu na mikakati na malengo ni sehemu ya taarifa.
Na taarifa zote hizo chanzo chake ni ubongoni, naam katika bongo ZETU.

"No Brain No Information" yaani "Bila Ubongo hakuna taarifa" hakuna mipango, mbinu, mikakati na malengo.
Hii ni kusema ubongo ni kitu muhimu na nyeti ambacho sharti itunzwe.

Ubongo haupo Kwa ajili ya Kutunza tuu kumbukumbu Kama watu wengi wajuavyo, Bali upo Kwa ajili ya kuzalisha(generate) mawazo, mipango, mbinu na mikakakati, na kuitafsiri, kuichambua, kuichanganua kisha baadaye ili itimie itatupasa itekelezwe Kwa upande wa nje WA mwili kupitia matendo ya Mwili Kama kuongea, kufanya Kwa mikono, kuandika, kukimbia, kutumia facial expressions n.k.

Vita kubwa kuliko zote Kwa binadamu ni Ile vita inayohusisha Akili na ubongo. Shambulizi lolote linalolenga kudhuru ubongo wa Mtu ndio shambulizi Baya kuliko yote.

Mtu anaweza akakushinda Kwa kuuharibu mwili wako au vita kuharibu majengo na miundombinu lakini ushindi huo ni wakitambo tuu. Ushindi wa milele ni ushindi wa kuudhuru ubongo wa Mtu/watu.

Weka akilini hili, kiungo pekee kwenye mwili wako ambacho kimelindwa Kwa nguvu zote ni Ubongo wako. Fuvu la kichwa ni mfupa mgumu Sana ambao unalinda ubongo wako usifikike Kwa urahisi.

Hii inatuambia nini?

Jibu hata wewe nafikiri unalo, unapaswa kulinda akili na ubongo wako kuliko kitu chochote kile.

Yote yaingiayo na yatokayo hakikisha yawe chini ya udhibiti wako.

Taikon mbona maelezo mengi, embu nenda kwenye hoja Acha kuzunguka!

"Sawa! Ngoja niache kuzunguka"

Nilianza na ubongo Kwa sababu ndio Msingi na center kuu ya Masuala ya Ujasusi.

Ujasusi wa Mtu Binafsi katika shughuli zake za kila siku!

i. Hakikisha unakuwa na kitabu cha kuhifadhi kumbukumbu zote muhimu kabla hujatoka nyumbani kwako au pakishakucha na hautoki nyumbani.
Kijitabu hiki utarekodi matukio muhimu Kwa kuyagawa katika makundi yake kulingana na vile utakavyoona.

ii. Hakikisha Ratiba yote na matukio yote muhimu Kwa muhtasari ambayo utayafanya Kwa siku hiyo umeyaandika.
Kwa mtiririko wa muda. Kila tukio ukishamaliza kulifanya unaweka Alama ya Tiki, kama hujafanya utaweka Alama ya X.

iii. Hakikisha wote utakaokutana nao wakajihusisha na wewe na kuzungumza na wewe kwa zaidi ya dakika moja yaani baada ya salama, weka kumbukumbu, jitahidi uelewe dhima kuu ya mazungumzo hayo.
Mara nyingi matukio yajayo yamebebwa na matukio yaliyopo au yaliyopita.

iv. Nyumbani pako hakikisha kuna Daftari la wageni ambalo wageni wakija wawe Registered muda na saa waliokuja na kuondoka.
Alafu kwenye Kitabu kingine ambacho sio Family Registered Books andika dhima ya mazungumzo makuu. Ikiwezekana andika na tabia ya Hali ya hewa.
Jitahidi ujifunze kuandika Kwa summarize au Kwa signs au codes.

v. Hakikisha pesa zote unazotumia ziwe Recorded kila siku.
Na zote zinazoingia ziwekee kumbukumbu.

vi. Rekodi migogoro mikubwa wewe na mwenza wako, kisha namna mlivyotatua migogoro hiyo.
Rekodi migogoro mikubwa au Hali usiyoielewa inayotokea kazini mwako, siku na saa, ikiwezekana na ulikuwa katika Dressing codes ipi na uliyegombana naye alikuwa katika Dressing codes ipi.
Mara nyingi migogoro huwa ishara ya Jambo linalotaka kutukia hivi karibuni linaweza kuwa Jambo zuri au Baya.
Halikadhalika na furaha fulani

vii. Fuatilia taarifa za habari, habari za kitaifa na kiulimwengu. Angalia dhima kuu na dira ya Dunia inaelekea wapi.
Angalia pia Utabiri wa Hali ya Hewa. Hii itakusaidia katika mipango na mikakati uliyojiwekea katika kutimiza malengo yako.

VIII. Fuatilia malengo, maono na makusudi ya makampuni na mashirika makubwa Duniani.
Hii itakusaidia katika kuona namna ya mipango na malengo yako.

ix. Hakikisha waliokaribu yako umewafanyia Vetting ya kutosha. Maana wengi ndio wata-determine Future yako.
Aidha kushinda au kushindwa.
Ni vizuri kila mwaka ukafanya Screening Kwa waliokuzunguka, upunguze wa Kupungua, usajili wakusajili.

X. Hakikisha unafikiri Kabla hujaongea, na ukiongea hakikisha unajisikiliza.
Ni vyema ukiwa na watu mkazungumza mambo yanayoeaunganisha ninyi kuliko kuongea mambo yako ya kibinafsi.
Mfano malengo na mikakati yako katika biashara au kazi unayoifanya.

X. Hakikisha unataarifa zote muhimu kuhusu kile unachokifanya, Yale yanayohusiana na ukifanyacho, na Yale yasiyohusiana na ukifanyacho.

X. Hakikisha kadiri uwezavyo ujue adui zako ni kina Nani kisha usionyeshe Kama umewajua.

Xi. Chunguza kila mara waliopo katika mzunguko wako ikiwemo Mkeo. Usikubali na kamwe usimuamini yeyote.
Hata kama umejua Mkeo sio muaminifu, take time kujibu mashambulizi au kutoa adhabu.

XII. Kuwa unemotionally, dhibiti mihemko yako ili kuepuka kutoa taarifa Kwa watu au adui zako bila ya ridhaa yako.
Mihemko ni moja ya mambo yanayoweza kukufanya adui zako wakakujua.

xiii. Dhibiti familia yako na iwekee mipaka.
Hakikisha mkeo awe chini ya udhibiti indirect awe anakuamini wewe pekee. Sio Wale wakupeleka Siri Kwa wachungaji au maaskofu au masheikhe.

Xiv. Jiwekee Misimu katika Mambo yako. Usiwe na msimu mmoja au Ratiba moja katika utekelezaji wa mipango yako.

xv. Kabla hujafanya lolote hakikisha umefanya calculations zote na kujua matokeo. Yaani chora ramani yote.

xvi. Usiombe ombe msaada au kutangaza shida zako. Huko ni kujitengezea maadui kupitia misaada ambayo labda utapewa Kwa lengo la kukuangamiza. Au wasikusaidie kabisa.

xvii. Kuwa msiri katika vitu ambavyo vinakupa Furaha.
Kama utaweza tengeneza mambo bandia yanayokupa furaha ili kuwapotosha adui zako hasa usiowajua.

Xviii. Tengeneza adui bandia au migogoro bandia ili kuangalia mzunguko WA wanaokuzunguka uko Imara kiasi gani.
Ikiwezekana gombana na Mkeo kama tukio bandia uone mzozo huo utaibua maadui wapi?

XIX. Hakikisha unamahusiano mazuri na mamlaka za Rohini. Kuwa na Diplomasia nzuri na Mungu aliyekuumba.
Kama utaweza jitahidi upate taarifa za kiroho hasa za maono na ndoto au ishara za maumbile na nature pale zinapoongea.

Kwa Leo tuishie hapa!
Ni Yule Mtibeli kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo toka ulimwengu huu mpaka ulimwengu mwingine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Andiko zuri sana, ubarikiwe, you are a great thinker...Kuna kaka yangu mmoja anaishi maisha kama hayo..
 
Baada ya kusoma vitabu kadhaa vya ujasusi, Hata Nilitaka Kujua wewe member ambae hatufahamiani, nikujue jina halisi, unaishi wapi, na kila kitu kuhusu wewe inawezekana sana. Kinachohitajika ni MUDA na Bajetu tu.

Strategies ni 7 tu ambazo zimesamaraiziwa kwa herufi 7 tu

COLOQAS
 
UJASUSI KWA MTU BINAFSI KATIKA SHUGHULI ZA KILA SIKU.

Anaandika, Robert Heriel
Jasusi wa kujitegemea.

Dondoo
• maana ya ujasusi
• Ujasusi Kwa mtu Binafsi
• manufaa ya ujasusi Kwa mtu binafsi

Lengo kuu la andiko
• Mwisho wa Andiko msomaji atapata maarifa na ufahamu katika namna ya kupanga mipango, kutekeleza, na kuifanikisha; Kujilinda na kuwa salama na Amani.

Binadamu Kwa asili ni mbinafsi. Hulka hiyo ndio huwa chanzo kikuu cha migogoro mingi katika maisha ya watu wengi.
Furaha ni kiini cha maisha ya binadamu. Hata hivyo furaha hutofautiana Kati ya mtu mmoja na mtu mwingine. Hiyo hufanya maslahi ya watu kutofautiana.
Lakini upatikanaji wa furaha hizo ambazo ndio malengo ya wengi pia hutofautiana baina ya mtu mmoja na mtu mwingine hii inachangiwa na sababu/factors mbalimbali ikiwem
I. Utofauti wa Akili baina ya mtu mmoja na mtu mwingine,
ii. Utofauti wa uthubutu na ujasiri
iii. Utofauti wa Mazingira
iv. Utofauti wa muda, ikiwemo muda wa kufanya maamuzi na kutenda.
v. Utofauti wa wahusika wanaotuzunguka.
Unaweza kuwa na akili lakini ukazungukwa na watu wajinga, au unaweza kuwa mjinga Ila ukazungukwa na watu wenye akili. Au unaweza kuwa mjinga na ukazungukwa na wajinga wenzako. Halikadhalika na wenye akili.
Au ukazungukwa na watu wenye vipato vya chini au watu wenye vipato vya juu.

vi. Elimu, Ujuzi na maarifa.

Mambo hayo ndio hufanya watu tuwe tofauti katika kutimiza malengo yetu. Hivyo basi katika kutimiza Jambo lolote itakupasa uzingatia pia mambo hayo hayo hapo juu.

Jambo moja unalotakiwa kujua kile unachofikiri kichwani mwako ni cha thamani, muhimu na kinahitaji ulinzi mkali ndio maana Mungu muumbaji alitufanya tusijue mtu mwingine anafikiria nini kichwani mwake. Jambo Hilo pekee lingekufanya ujue kuwa Dunia sio sehemu Salama.

UJASUSI
Ujasusi unahusu taarifa. Upatikanaji, uchambuzi, uchakataji, utunzaji na utekelezaji wa taarifa.

Tunafahamu kuwa mipango, mbinu na mikakati na malengo ni sehemu ya taarifa.
Na taarifa zote hizo chanzo chake ni ubongoni, naam katika bongo ZETU.

"No Brain No Information" yaani "Bila Ubongo hakuna taarifa" hakuna mipango, mbinu, mikakati na malengo.
Hii ni kusema ubongo ni kitu muhimu na nyeti ambacho sharti itunzwe.
Ubongo haupo Kwa ajili ya Kutunza tuu kumbukumbu Kama watu wengi wajuavyo, Bali upo Kwa ajili ya kuzalisha(generate) mawazo, mipango, mbinu na mikakakati, na kuitafsiri, kuichambua, kuichanganua kisha baadaye ili itimie itatupasa itekelezwe Kwa upande wa nje WA mwili kupitia matendo ya Mwili Kama kuongea, kufanya Kwa mikono, kuandika, kukimbia, kutumia facial expressions n.k.

Vita kubwa kuliko zote Kwa binadamu ni Ile vita inayohusisha Akili na ubongo. Shambulizi lolote linalolenga kudhuru ubongo wa Mtu ndio shambulizi Baya kuliko yote.
Mtu anaweza akakushinda Kwa kuuharibu mwili wako au vita kuharibu majengo na miundombinu lakini ushindi huo ni wakitambo tuu. Ushindi wa milele ni ushindi wa kuudhuru ubongo wa Mtu/watu.

Weka akilini hili, kiungo pekee kwenye mwili wako ambacho kimelindwa Kwa nguvu zote ni Ubongo wako. Fuvu la kichwa ni mfupa mgumu Sana ambao unalinda ubongo wako usifikike Kwa urahisi.
Hii inatuambia nini?
Jibu hata wewe nafikiri unalo, unapaswa kulinda akili na ubongo wako kuliko kitu chochote kile.
Yote yaingiayo na yatokayo hakikisha yawe chini ya udhibiti wako.

Taikon mbona maelezo mengi, embu nenda kwenye hoja Acha kuzunguka!

"Sawa! Ngoja niache kuzunguka"

Nilianza na ubongo Kwa sababu ndio Msingi na center kuu ya Masuala ya Ujasusi.

Ujasusi wa Mtu Binafsi katika shughuli zake za kila siku!

i. Hakikisha unakuwa na kitabu cha kuhifadhi kumbukumbu zote muhimu kabla hujatoka nyumbani kwako au pakishakucha na hautoki nyumbani.
Kijitabu hiki utarekodi matukio muhimu Kwa kuyagawa katika makundi yake kulingana na vile utakavyoona.

ii. Hakikisha Ratiba yote na matukio yote muhimu Kwa muhtasari ambayo utayafanya Kwa siku hiyo umeyaandika.
Kwa mtiririko wa muda. Kila tukio ukishamaliza kulifanya unaweka Alama ya Tiki, kama hujafanya utaweka Alama ya X.

iii. Hakikisha wote utakaokutana nao wakajihusisha na wewe na kuzungumza na wewe kwa zaidi ya dakika moja yaani baada ya salama, weka kumbukumbu, jitahidi uelewe dhima kuu ya mazungumzo hayo.
Mara nyingi matukio yajayo yamebebwa na matukio yaliyopo au yaliyopita.

iv. Nyumbani pako hakikisha kuna Daftari la wageni ambalo wageni wakija wawe Registered muda na saa waliokuja na kuondoka.
Alafu kwenye Kitabu kingine ambacho sio Family Registered Books andika dhima ya mazungumzo makuu. Ikiwezekana andika na tabia ya Hali ya hewa.
Jitahidi ujifunze kuandika Kwa summarize au Kwa signs au codes.

v. Hakikisha pesa zote unazotumia ziwe Recorded kila siku.
Na zote zinazoingia ziwekee kumbukumbu.

vi. Rekodi migogoro mikubwa wewe na mwenza wako, kisha namna mlivyotatua migogoro hiyo.
Rekodi migogoro mikubwa au Hali usiyoielewa inayotokea kazini mwako, siku na saa, ikiwezekana na ulikuwa katika Dressing codes ipi na uliyegombana naye alikuwa katika Dressing codes ipi.
Mara nyingi migogoro huwa ishara ya Jambo linalotaka kutukia hivi karibuni linaweza kuwa Jambo zuri au Baya.
Halikadhalika na furaha fulani

vii. Fuatilia taarifa za habari, habari za kitaifa na kiulimwengu. Angalia dhima kuu na dira ya Dunia inaelekea wapi.
Angalia pia Utabiri wa Hali ya Hewa. Hii itakusaidia katika mipango na mikakati uliyojiwekea katika kutimiza malengo yako.

VIII. Fuatilia malengo, maono na makusudi ya makampuni na mashirika makubwa Duniani.
Hii itakusaidia katika kuona namna ya mipango na malengo yako.

ix. Hakikisha waliokaribu yako umewafanyia Vetting ya kutosha. Maana wengi ndio wata-determine Future yako.
Aidha kushinda au kushindwa.
Ni vizuri kila mwaka ukafanya Screening Kwa waliokuzunguka, upunguze wa Kupungua, usajili wakusajili.

X. Hakikisha unafikiri Kabla hujaongea, na ukiongea hakikisha unajisikiliza.
Ni vyema ukiwa na watu mkazungumza mambo yanayoeaunganisha ninyi kuliko kuongea mambo yako ya kibinafsi.
Mfano malengo na mikakati yako katika biashara au kazi unayoifanya.

X. Hakikisha unataarifa zote muhimu kuhusu kile unachokifanya, Yale yanayohusiana na ukifanyacho, na Yale yasiyohusiana na ukifanyacho.

X. Hakikisha kadiri uwezavyo ujue adui zako ni kina Nani kisha usionyeshe Kama umewajua.

Xi. Chunguza kila mara waliopo katika mzunguko wako ikiwemo Mkeo. Usikubali na kamwe usimuamini yeyote.
Hata kama umejua Mkeo sio muaminifu, take time kujibu mashambulizi au kutoa adhabu.

XII. Kuwa unemotionally, dhibiti mihemko yako ili kuepuka kutoa taarifa Kwa watu au adui zako bila ya ridhaa yako.
Mihemko ni moja ya mambo yanayoweza kukufanya adui zako wakakujua.

xiii. Dhibiti familia yako na iwekee mipaka.
Hakikisha mkeo awe chini ya udhibiti indirect awe anakuamini wewe pekee. Sio Wale wakupeleka Siri Kwa wachungaji au maaskofu au masheikhe.

Xiv. Jiwekee Misimu katika Mambo yako. Usiwe na msimu mmoja au Ratiba moja katika utekelezaji wa mipango yako.

xv. Kabla hujafanya lolote hakikisha umefanya calculations zote na kujua matokeo. Yaani chora ramani yote.

xvi. Usiombe ombe msaada au kutangaza shida zako. Huko ni kujitengezea maadui kupitia misaada ambayo labda utapewa Kwa lengo la kukuangamiza. Au wasikusaidie kabisa.

xvii. Kuwa msiri katika vitu ambavyo vinakupa Furaha.
Kama utaweza tengeneza mambo bandia yanayokupa furaha ili kuwapotosha adui zako hasa usiowajua.

Xviii. Tengeneza adui bandia au migogoro bandia ili kuangalia mzunguko WA wanaokuzunguka uko Imara kiasi gani.
Ikiwezekana gombana na Mkeo kama tukio bandia uone mzozo huo utaibua maadui wapi?

XIX. Hakikisha unamahusiano mazuri na mamlaka za Rohini. Kuwa na Diplomasia nzuri na Mungu aliyekuumba.
Kama utaweza jitahidi upate taarifa za kiroho hasa za maono na ndoto au ishara za maumbile na nature pale zinapoongea.

Kwa Leo tuishie hapa!
Ni Yule Mtibeli kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo toka ulimwengu huu mpaka ulimwengu mwingine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mungu ni mkuu sana, tumbo lililokubeba hakika lilibeba tunu. Mkuu Robert Mungu akubariki sana, asante kwa dose hii.
 
Baada ya kusoma vitabu kadhaa vya ujasusi, Hata Nilitaka Kujua wewe member ambae hatufahamiani, nikujue jina halisi, unaishi wapi, na kila kitu kuhusu wewe inawezekana sana. Kinachohitajika ni MUDA na Bajetu tu.

Strategies ni 7 tu ambazo zimesamaraiziwa kwa herufi 7 tu

COLOQAS

😊😊🙏🏽🙏🏽
 
Back
Top Bottom