Ujasusi na uongozi: Mafanikio ya rais Putin katika kuirejesha tena Urusi

Fanya research ya kujua uchumi wa urusi kabla na baada ya Putin..
Russian economy
2013:$2.1trillions
2016:$1.31trillions
sourec:World bank.
Putin anscheza na upepo tuu katika global politics tuu,Ila hana ecomomic plans za ku rescue urusi hapo ilipo kwenye uchumi usioeleweka.Yani ndani ya miaka mi 3 uchumi unaporomoka kwa zaidi ya 40% halafu bado utajiita raisi imara?...Unakaa kila siku kutunisha misuli na propaganda za kijeshi huku uchumi haueleweki,afu uansema unataka kuirudsha Russia nguvu kama enzi za USSR?,seriously?..Nachoamini ni kwamba Nchi yoyote duniani haiwezi kuwa super power kama huna uchumi imara na stable wenye vyanzo vuingi vya mapato,sio kutegemea mafuta tuu,bei ikishake kidogo tu kwishaaa,sio pesa sio uzalishaji,kila kitu kitakuwa hovyo hovyo.Russia haipo imara kama watu wanavyoaminishwa hapa,Alichofanya Putin ni ku wing upepo wa global politics basi.Marekani imekuwa ikichukiwa sana baada ya kuivamia Libya,Dunia ililaumu sana,sasa Putin aliona hiyo opportunity na kuitumia vizuri,alichokifanya ni kucheza karata vizuri kule syria na kuwing sympathy kwa ulimwengu kwamba anafanya kitu sahihi kabisa.Hicho ndicho kilichompandisha chart sana Putin,but kwa swala eti putin anaplan kuirudisha russia yenye nguvu kwa uchumi huu mbovu usiyokuwa na stable growth,inflation kila mwaka inakuwa juu sababu ya kutegemea mafuta kama roho ya uchumi.Kikubwa atarudisha zile zama za mashindano ya silaha(arms race) kitu ambacho russia hataweza kushina kutokana na uchumi mbovu,hata Putin analifahamu vizuri sana hili,he wont wing the arms race with USA,ndo maana ana hakikisha kila siku jina la russia linatajwe kwe vyombo vya habari kama wanavyotajwa sasa kuhusu kuingilia uchaguzi wa marekani,Kitu ambacho ni nonsense kabisa lakini anachukua sifa dunia nzima,ila kwa mtu sound mind atajiuliza,why ali hack zile e mail za clinton na DNC?..ili iweje sasa,imebadili nini labda?..kama ni kutafta russia itajwe tuu kwende media as propaganda hapo sawa.Putin anaelewa kabisa US foreing millitary policy and strategy zinatoka pale pentagon na wala sio kwamba Trump ndo atafanya changes kubwa kiivyo...kama huamini fuatilia mgogoro wa south china sea na ucheki na strategies za pentagon ku i contain China na Urusi kupitia south korea na japan..Cheki move za NATO akiongozwa na US kule poland na Romania,Usitegemee siku Trump atakuja na sera ya kuitaka US ku pull out from Poland or Romani,Hiyo ni ndoto na Putin knows that.So putin ataendelea kutumia pesa nyingi kutengeneza silaha kwa ajili ya ku counter US threats na kusahau kujenga uchumi,Arms race na US hatoiweza sababu ya uchumi mbovu.Kila siku ukifuatilia habari utaona contracts kibao kati ya serikali ya US na makamuni ya kutengeneza silaha,either wana upgrade au kutengeneza silaha mpya..Yaani unataka kuwa super powe na uchumi mbovu?..Nomba hiyo nafasi tumpe china sio Russia.
 
makonda give me a break! jamaa kasoma muccobs sidhan tiss wanachukua watu kwenye taasis za watu wenye uwezo mdogo kitaaluma kama muccobs
Chuo kilipewaje hadhi ya chuo kikuu kama kinauwezo mdgo kitaaluma au huelewi unachojibu
 

Nimekupata kabisa mkuu!
 
K

kwanini hawaivamii urusi sasa?
Rudia kusoma post yangu taratibu. Nchi yoyote yenye silaha za nyuklia tayari ina garantii ya kutoshambuliwa milele kwa kuwa mshambuliaji na mshambuliwa na watazamaji (dunia nzima kwa case ya vita ya US na Urusi) watakufa.. Kutakuwa hakuna maisha tena duniani mionzi ya sumu itakuwa mikali sana hakuna kiumbe kitasavaivu(Kiingereza wanaita mutually Assured Destruction). Kwa jinsi hii hakuna raisi wa Marekeni mwenye akili timamu ataishambulia urusi (ama uchina) isipokuwa tu kama Marekani inajibu mapigo kwa kushambuliwa kwanza.. Una follow?
Nimekupata kabisa mkuu!
 
Ni idea mpya mkuu silifahamu ili ila naamini linawezekana kwa mataifa ya nyuklia kuogopwa kama korea ya kaskazini na iran
ndo hivyo mkuu ndo maana Marekani anakomaa na kale kajamaa ka korea kaskazini (pia pamoja na Israel wanawakomalia Waajemi wa Iran) wasipate hizi silaha manake wakizipata tu basi mchezo utakuwa umekwisha kutakuwa hakuna tena vichapo vya reja reja wala kumtishia nyau mtu
 
mkuu kila dola kuu (empire) kwa wakati wake huwaga zinanyanyasa sana mataifa ama dola dhaifu..kuanzia kina Genghis Khan and Kublai Khan wa Mongolia , kina Ottoman wa dola ya kituruki, kina Julius Caesar wa dola ya Kirumi , dola ya kiarabu ya Umayyad (ambayo iliteka maeno mengi yakiweya uhispania ya leo) n.k. Kifupi kila dola kwa wakati inatembeza kichapo kila sehemu ili wapinzani wasiamke.lakini pia kila kitu kina mwanzo na mwisho na wao wakti wao ukifika basi itaamka dola nyingine kuu...
 
Huku kwetu shida kubwa ni kutanguliza maslahi ya chama kuliko taifa, kama tungeondoa uccm, ucuf na uchadema mbona hali ya taifa ingekuwa nzuri zaidi.
Wengi wetu tumefunikwa na wingu la uchama kwanza mengine baadae. Tujaribu kushaurika jamani kwa manufaa ya taifa, tusiishi kwa chuki, wivu na ubinafsi
 
Ww jamaa huwa napenda sana post zako unajua sana kufanya uchambuz aisee dah hongera mkuu
 
Nisaidie mkuu namna ya Ku bold baadhi ya maneno ili yaonekane *makubwa*

[HASHTAG]#MALCOM[/HASHTAG] LUMUMBA

Kama unatumia computer, highlight neno unalotaka kulibold, then hapo kwenye task bar juu bonyeza Bolded B letter.
Au rahisi zaidi, highlight the content, halafu tumia shortcut kwa kubonyeza Ctrl pamoja na herufi B kwenye keyboard yako kwa pamoja.
 
NIngependa usome kitabu cha The Death Of The Dissident, utakipenda sana na utakubali ambition aliyokuwa nayo Putin tangu kijana.
 
Shushushu wewe, kuna thread iliwekwa hapa jinsi ya kuwakamata watu wanaotumia fake ID, sasa wewe unataka muwasiliane na huyu jamaa et umpe kitabu ili iweje! Wewe mwelekeze duka atakalopata hicho kitabu baaasi.
Acha uoga na ulimbukeni, hicho kitabu kiko out of print huwezi kipata duka lolote, humu ndani hatuchunguzani, kama ni kazi unayoifanya basi ni wewe na siku ukitatizwa na ninachokisema au kukiandika, rejea kwenye ID yangu, ambayo ni jina langu halisi, nanimeweka picha yangu halisi, sina uoga na ninachokiandika wala kukisema humu, wewe kinachokuogopesha ni nini wakati kitabu chenyewe kilikuwa huru kununuliwa na mtu yeyote, huwezi kukifanananisha na Shadow World/Animal Farm au Satanic Verses, hiki hakijawahi kuwekewa pingamizi sehemu yoyote duniani kasoro Russia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…