Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Naona watu wanaosema kupaua mil 10 finishing mil 15 hawajui maana yake. Labda wanazungumzia za uswahilini
Mkuu kwani hapo kimetumika kitu gani kupaua?
Si ni hizi hizi mbao za kutoka iringa na mabati yenyewe hayo si ndio haya haya tunahopaulia huku mtaani?
 
Hivi majengo yapi ya selikali ambayo huku mtaani hayapo?

Ujenzi wa hayo majengo hauna tofauti yeyote na huu tunaofanya huku mtaani
Ratio ya tofali 25 per bag,tiles ndo 9 per bag. Umejenga hivyo nyumba yako?
 
Hiyo nyumba tuseme kupaua ni milioni 10
Msingi na jamvi milion 10.
Kupandisha tofali juu milion 10
Finishing milion 15
Ziada milini 10.

Jumla milioni 55!

Magu yupo sahihi hapo pana upigaji!

Kwa hiyo hela milioni 143 ilitakiwa zitoke nyumba kama hizo 3

Sasa unasemaje magu yupo sahihi wakati yeye kasema mil 43 na wewe unasema ujasema mil 55?

Au kwa akili yako mil 55 ni sawa na mil 43?
 
Inashangaza kuwa watu wanatoa makadirio ya jengo bila kujua hata lina mita ngapi za mraba kwa ukubwa. Haiwezekani kupata gharama bila upembuzi jadidi.
 
Ninyi hata rais anye barabarani mtaona ni sawa tu... lumumba tumeshawazoea
Mimi naomba sasa hivi selikali na magufuli aache kuhangaika na wabadhirifu au wapigaji!

Hii mivyama imetufanya tuwe wapumbavu,!
Rais pale ana data zote anatokea mtu kwa vile ana mtazamo wake na akishameza bendera ya chama anasema hapo rais anasema uongo! Lakini jambo hilo hilo angesema mtu wa chama chake angshangilia na makofi juu,,

Imefika wakati Magufuli hata akikemea waizi hadharani wapinzani wanapinga!

Magufuli aachane na mitanzania ilishazoea kupigwa aache iendeled kuibiwa!
 
Mkuu kwani hapo kimetumika kitu gani kupaua?
Si ni hizi hizi mbao za kutoka iringa na mabati yenyewe hayo si ndio haya haya tunahopaulia huku mtaani?
Unajua kama mabati yanatofautiana quality na hivyo bei? Unajua mbao zinatofautiana ubora na bei? Mtu anayejua maana ya ujenzi (hasa finishing) hawezi kusema 142m ni kubwa
 
Unajua kama mabati yanatofautiana quality na hivyo bei? Unajua mbao zinatofautiana ubora na bei? Mtu anayejua maana ya ujenzi (hasa finishing) hawezi kusema 142m ni kubwa
Mkuu mbao unazo sema wewe huwa zinauzwa nazijua sana uzuri mimi natokea iringa najua mbao!

Mbao unzosema wewe ni za gharama ni zile zinazokuwa treated ambazo huuzwa kwa futi na fugi moja ni around 1000 inategemea na mkoa
Sasa hapo au kuna mbao zingine zaidi ya hizi ninazozijua mimi?
 
Kwa standard ya majengo ya serikali hata wakisema wamejengea 200M wala sishangai.

Kwangu binafsi hata 30M najenga kama hiyo.

*Ramani yakugongea.
*Hakuna jamvi.
*Tofali za kuchoma.
*Concrete beam "Lenta" nondo moja inalala
*Mbao siyo treated (zinapakwa oil chafu) tena mix na mirunda.
*Bati brand za kichina tena 30g
*Mafundi wote wa mitaani tu.
*Nasimamia mwenyewe A to Z.
*Napiga Ceiling boards.
*Tiles mchina (Goodone)
*Milango siyo mbao ngumu.
Ni nyumba gani ya serikali utajenga kwa tofali za kuchoma au tiles za kichina?
 
Kwa huku nilipo haifiki ila sijajua gharama ya ujenzi huko dodoma eneo hilo!
Rais pia akue yeye ndiye anaipaisha dodoma hivyo kuna gharama zinapanda pia. Naamini hiyo nyumba haifiki milioni 150 ila pia huwezi ijemga kwa milioni 40 ikafika hapo...
 
Sasa unasemaje magu yupo sahihi wakati yeye kasema mil 43 na wewe unasema ujasema mil 55?

Au kwa akili yako mil 55 ni sawa na mil 43?
Yupo sahihi sana hiyo nyumba haiendani na milion 143, wote tunajua bei za vifaa na tumejenga pia,

Hata kama ukisema ni bei ya kiselikali lakini bei za vifaa tunazijua, siyi kwamba hiho nyumba materials wametoa angani hapana. Ni haya haya.
 


Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano.

View attachment 1514090

Hivi kwanini wanasiasa wa bongo wanajitia kujua kila kitu hata vile ambavyo viko nje ya taaluma yao? Gharama za ujenzi ziko juu na mtu huwezi kutoa makadirio kwa kuangalia tu.
By the way, nani anajua gharama harisi za kununua madege ya atcl?
 
Huenda pia kuna ukuta wa uzio haujaonekana katika picha
 
Endeleeni kupima kwa macho tu mpaka kuche bebeni futi pamoja na QS muende Chamwino hapa hamtapata jibu
 
Huwezi mkuu, nyumba za serikali hazijengwi na vifaa vya ujenzi vya hovyo hovyo.
Tofali grade one tena za kulaza mara nyingi, ratio ya cement ya hali ya juu na bati gauge 26.
Huwa mnakurupuka mnalinganisha na vibanda vyetu vya mtaani.
Pili huwa kuna bei ya elekezi ya ujenzi mfano mdogo...
...majengo ya hospitali cost/sqm huwa ni 850,000
...magodauni cost/aqm ni 500,000
Msiwe mnakurupuka bila kuwa na ufahamu sahihi

Huwezi kuzunguka nyumba eti ukapata gharama za ujenzi.
Pitia manunuzi na pitia kitabu cha consultants uone mapendekezo yao katika ujenzi pamoja na samani zilizopo ndani
Sasa kwanini nyumba za serikali ndio zinaongoza kwa ubovu?
 
Back
Top Bottom