Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Ninyi hata rais anye barabarani mtaona ni sawa tu... lumumba tumeshawazoea
 
Million 70 safi kila kitu, tuache unafiki
 
kama ina underground bunker inaweza kuzidi hiyo M143..

lakini kama ndio hiyo niionayo...jenerali amekulwa cha juu

simple like that.
Ofisi nyeti Kama hii haiwezi kukosa Underground bunker au STRONG vault.

Hizi gharama naona Ni halisi.
 
Tatizo wengi wetu hatuna utaratibu wa ku record gharama za ujenzi kwa kuogopa tutaumia zaidi.
 
Finishing million 15 tu?? Bro hauko serious
 
Hiyo nyumba huwezi kupaua kwa 10 million mkuu labda utumie makuti.
Kuna watu humu hawajawahi kujenga, au huwa wanajenga mtandaoni.

Hii nyumba imekula bati nyingi mno. Asilete masihara kabisa
 
Milioni 143, zinatoka nyumba kama hizo tatu [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
 
Million 40 ujenge labda utumie tofali za kuchoma na ndipo ujenge Nyumba yenye ukubwa huu.
Ujenzi uko juu waungwana

kuna jamaa hapo kaongelea gharama ki serikali ndio kidogo amenishawishi kuamini,lakini ki raia ningekuonesha picha ya nyumba kama hiyo na ina ukuta,na nyumba za nje bila kusahau maduka kama matatu na haijafikia gharama hizo
 
Vyumba vingapi kwani
 
Kwani kamjengo kana vyumba vingapi? Tuanze hapo[emoji38][emoji38], million 143 iwe na reason basi
 
Tatizo wengi wetu hatuna utaratibu wa ku record gharama za ujenzi kwa kuogopa tutaumia zaidi.
Ni kweli mkuu,
Wengi wanalichukulia jengo Kama Ni kupanga tofali na kufunika na cement.

Ila Kuna vitu vidogo vidogo vinapukuta Ela Sana.

Hasa hasa wakati wa FINISHING.
 
Kwa standard ya majengo ya serikali hata wakisema wamejengea 200M wala sishangai.

Kwangu binafsi hata 30M najenga kama hiyo.

*Ramani yakugongea.
*Hakuna jamvi.
*Tofali za kuchoma.
*Concrete beam "Lenta" nondo moja inalala
*Mbao siyo treated (zinapakwa oil chafu) tena mix na mirunda.
*Bati brand za kichina tena 30g
*Mafundi wote wa mitaani tu.
*Nasimamia mwenyewe A to Z.
*Napiga Ceiling boards.
*Tiles mchina (Goodone)
*Milango siyo mbao ngumu.
 
Gharama iliyotumika ni sahihi kabisa ,sababu kuna vitu vya ndani kama vile mtandao wa simu,internet na CCTV camera hapo sio chinii ya milion 40,Bado kuna viyoyozi na umeme.watu wanaongea tu ,mfano sisi tunaojenga kijengo kidogo tu cha tawi la benki ina kugharimu zaidi ya ml 350 hadi 400 ila watu wasiojua masuala ya ujenzi watajua kwamba pesa imepigwa hapo,mzee wetu tunajua kipindi hiki cha kampeni anataka kukosoa tu ila ukweli anaujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…