Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Hatuwezi ithamanisha hiyo nyumba bila kujua imechimbwa msingi kwenda chini futi ngapi,
Foundation imetumia material yapi, pia tiles hapo ndani katumia zipi, na milango ya hapo ndani ikoje, ratio ya kiserikali inajulikana ni ya ukweli,
Ukikuta ni ujenzi wa serikali ninavyoujua million 120 zinakata.
Na kutokana na material katumia yapi
Huenda walifwatua tofali inchi 6 na ratio ikawa ni tofali 20 kwa mfuko.
Hayo yote rais anajua ndo maana akaja na conclusion hiyo.
 
Force account, kwani anajenga mkuu wa takukuru na wafanyakazi wake?si wameajiri local fundi (kampuni) unadhani faida wanapata vipi?
Local fundi analipwa kwa bei za soko kama unazoweza kumlipa wewe na mimi na sio kampuni. Sasa kama walitumia kampuni ndio matokeo yake mh. Rais analalamika.
 
Rais huwa mkurupukaji sana, gharama ya nyumba inategemea na mahitaji.
Siyo mkurupukaji wala nini pale, sema kagusa maslahi ya watu, lakini ukweli kausema!

Hata ukiweka wizi wako, official ama localy hawezi jenga nyumba hiyo zaidi ya mil.70.
 
Local fundi analipwa kwa bei za soko kama unazoweza kumlipa wewe na mimi na sio kampuni. Sasa kama walitumia kampuni ndio matokeo yake mh. Rais analalamika.
Ikiwa ni hivyo majengo ya hospitali za wilaya zilizotengewa bilioni 1 zingekuwa na majengo siyo chini ya 20 kila moja, hilo jengo kwa kazi za serikali ndio gharama yake...
 
Mbona Jaffo amejenga Gorofa Kwa Bilioni 1 na wengine wamejenga vile VIBANDA nao Kwa Bilioni 1.
 
Kama kuna finishing touches nzuri huko ndani, na structure ilijengwa kwa viwango stahiki, no way hiyo nyumba ni less than 100m.. mnaosema milioni sijui 60, 70 mnaongelea very low qualoty houses...
Tungelikuwa hatujajenga, tusiolewa finishing ya vifaa vya ujenzi vya kisasa tungelikubaliana na wewe.

Hiyo nyumba piga galagaza haivuki 70m.
 
Ikiwa ni hivyo majengo ya hospitali za wilaya zilizotengewa bilioni 1 zingekuwa na majengo siyo chini ya 20 kila moja, hilo jengo kwa kazi za serikali ndio gharama yake...
Majengo ya hospital za wilaya ni makubwa zaidi ya hilo nenda wanapojenda na uliza gharama zake then fananisha na jengo la TAKUKURU.
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090

Msingi sio na jamvi sio chini ya 10 ml
Kupandisha kwa haraka haraka tofali 4000 @1500 nchi 6= 6,750,000
Fundi 1,500,000

Lenta hapo Nondo 40 / tena zifungwe 3 badala ya nne @ 17000 =680,000

Mbao pcs 300 tofauti tofauti fanya 2,500,000

Mabati fanya bando 15 na za migongo @ 325,000= 4,850,000
Fundi 2,000,000

Badirisha gril @175,000 fanya yako 15 =2,625,000

Madirisha alminium@350,000=5,250,000

Bado kupiga lipu
Kupaka niru
Kupaka rangi
Wireling ya umeme
Mabomba
Kupiga gipsam
Kufunga milango
Kupiga tiles
Rangi ya nje
Vifaa vya umeme

Acheni masihara hiyo pesa ni sawa ukizigatia Serikali inanunua vitu grade na 1 kwangu me hawajaiba wako mle mle kabisaaa
 
Hatuwezi ithamanisha hiyo nyumba bila kujua imechimbwa msingi kwenda chini futi ngapi,
Foundation imetumia material yapi, pia tiles hapo ndani katumia zipi, na milango ya hapo ndani ikoje, ratio ya kiserikali inajulikana ni ya ukweli,
Ukikuta ni ujenzi wa serikali ninavyoujua million 120 zinakata.
Na kutokana na material katumia yapi
Huenda walifwatua tofali inchi 6 na ratio ikawa ni tofali 20 kwa mfuko.
Tufanye tunakubaliana na wewe, embu jaribu kutupigia 'rafu' tuone.

Ninavyojua ni kwamba, nenda chini,fukua msingi urefu utakavyo, laza tofari upendavyo, weka 'resho' unayoitamani hata ya karai15 kwa mfuko, hiyo nyumba haiwezi kumeza tofari zaidi ya 6000÷20×20,000/=? na mifuko 200×20'000/= ya kujengea pamoja na ripu, tufanye na 100 kwa ajili ya tiles jumla mifuko 600.

Weka bati hizo za migongo mipana 200×33,000/=?
Mbao za size mbalimbali hazizidi 500×12,000/=?
Hapa hatujapigia nondo na vifaa vingine vya msingi kwenye finishing, lakini tupo kwenye ishirini na,30haijakatika.

Embu isongeshe kwenye mchanga, nondo, tiles rangi,misumari, alluminium na grill, milango, wiring, gipsum uone kama inavuka70?
Gharama za ujenzi tunazikuza sana kwa nakusudi ajili ya aslahi binafsi ama kutokujua hadi tunaingia uoga na kupelekea watu kusalia hadi kufia 'mapangoni'
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Hii najenga LA milion 40
 
Unapozungumzia mali za serikali sio kama zetu mtaani,kwanza serikalini awaruhusu kujengea kitu kisicho kipya,watu wa manunuzi wanaelewa.

Pili,kuna bei elekezi za ununuaji vitu hasa kama wametumia mfumo wa tender,Mfano kalamu unayonunua wewe 300 bei ya kimanunuzi kwa serikalini unaweza kuta ni 500,hata ikishuka au ikipanda kama tayari upo kwenye mkataba wao watanunua kwa bei hiyo hiyo.

Note:sidhani kama nimeelezea vizuri ila nadhani utapata nilichokuwa nafikiria.
Aliyelalamika kua hapo kuna upigaji hayuko serikalini?,hayajui haya?,kumbuka amekaa wizara ya ujenzi zaidi ya miaka 10 so maswala ya ujenzi na thamani zake anazijua sana
 
Million 40 kwa nyumba ya serikali?
Au ni ya matofali 100 kwa mfuko?
Bati za gauge 32?
Foundation ya tofali 2 ardhini?
Ijengwe na Wapemba wa jenga uza?
 
Ukinipa M 143 nakuletea nyumba kama hiyo mbili na vimilioni vichache vinabaki.
Shida ujenzi wa miradi ya serikali unapitia mikononi ya wadau wengi. Utasikia injinia mshauri,mara project designer n.k na pia maelekezo ya kutaka ujenzi kuzingatia viwango maalum.Mfano mfuko wa simenti 1:20 tofali wakati nyumba binafsi ni 1:40. Vivyo hivyo kwenye bati n.k Matokeo yake kitu kidogo au nyumba ndogo thamani yake inakuwa kubwa. Hivyo binafsi sishangai hiyo thamani ni reasonable kabsa.
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Hii style ya paa la nyumba The Late DAB alipiga marufuku..any way apaumzike amani..hi nyumba nipe mimi 30M nakujengea na chenji inabaki..kuna mtu kapigwa apo
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Kinachoniskitisha TZ kwani upigaji mwingi ni hadi JPM mwenyewe augundue watendaji wale wengine hawaoni?what is behind this?
 
Back
Top Bottom