Hatuwezi ithamanisha hiyo nyumba bila kujua imechimbwa msingi kwenda chini futi ngapi,
Foundation imetumia material yapi, pia tiles hapo ndani katumia zipi, na milango ya hapo ndani ikoje, ratio ya kiserikali inajulikana ni ya ukweli,
Ukikuta ni ujenzi wa serikali ninavyoujua million 120 zinakata.
Na kutokana na material katumia yapi
Huenda walifwatua tofali inchi 6 na ratio ikawa ni tofali 20 kwa mfuko.
Tufanye tunakubaliana na wewe, embu jaribu kutupigia 'rafu' tuone.
Ninavyojua ni kwamba, nenda chini,fukua msingi urefu utakavyo, laza tofari upendavyo, weka 'resho' unayoitamani hata ya karai15 kwa mfuko, hiyo nyumba haiwezi kumeza tofari zaidi ya 6000÷20×20,000/=? na mifuko 200×20'000/= ya kujengea pamoja na ripu, tufanye na 100 kwa ajili ya tiles jumla mifuko 600.
Weka bati hizo za migongo mipana 200×33,000/=?
Mbao za size mbalimbali hazizidi 500×12,000/=?
Hapa hatujapigia nondo na vifaa vingine vya msingi kwenye finishing, lakini tupo kwenye ishirini na,30haijakatika.
Embu isongeshe kwenye mchanga, nondo, tiles rangi,misumari, alluminium na grill, milango, wiring, gipsum uone kama inavuka70?
Gharama za ujenzi tunazikuza sana kwa nakusudi ajili ya aslahi binafsi ama kutokujua hadi tunaingia uoga na kupelekea watu kusalia hadi kufia 'mapangoni'