Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Kama nyumba ya kuishi..residential house and not an office! Ila haiwezi kujengwa kwa 40,000,000 au 60,000,000 kma walivyosema PM na Rais. Likewise, 145,000,000 ni nyingi !
 
Hatuwezi ithamanisha hiyo nyumba bila kujua imechimbwa msingi kwenda chini futi ngapi,
Foundation imetumia material yapi, pia tiles hapo ndani katumia zipi, na milango ya hapo ndani ikoje, ratio ya kiserikali inajulikana ni ya ukweli,
Ukikuta ni ujenzi wa serikali ninavyoujua million 120 zinakata.
Na kutokana na material katumia yapi
Huenda walifwatua tofali inchi 6 na ratio ikawa ni tofali 20 kwa mfuko.
Umemaliza ubishi!
 
*Tofari 5000×1500= 7, 500, 000Tsh

*kokoto na mchanga=2, 000, 000Tsh

*Nondo 100×25000=2, 500, 000Tsh

*ciement mifuko 200×15000=3, 000, 000Ts

*Mabati 80(Gauge 28)
75×33000= 2, 640, 000 Tsh

* mbao= 3, 100, 000Tsh

*madirisha na milango (complete)=
16, 000, 000Tsh

*Tiles +gypsum+rangi=
7, 000, 000Tsh

*maji(pamoja na masinki ya jikoni, chooni) + umeme= 7, 000, 000Tsh

*maitaji madogo madogo
1, 000, 000Tsh
* ufundi Tsh. 10, 000, 000/=

Jumla Tsh 60, 000, 000/=
Mbona kila mtu nyie anajifanya alichukua quotation zake, kwanini wao wasiseme ili kutoa utata

Sent from my HRY-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo nyumba tuseme kupaua ni milioni 10
Msingi na jamvi milion 10.
Kupandisha tofali juu milion 10
Finishing milion 15
Ziada milini 10.

Jumla milioni 55!

Magu yupo sahihi hapo pana upigaji!

Kwa hiyo hela milioni 143 ilitakiwa zitoke nyumba kama hizo 3
Nikupe hiyo pesa ukanijengee kama hiyo !?
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Hapo bado ukuta wa fence!
 
Ila kumbuka huwez jenga nyumba ya taasisi ukasupervise kama yako, hii inaenda na wataalam, tofali hadi upeleke maabara, zege pia, i bet kwa construction process halisi zikifuatwa hii nyumba inafika 110mil.
Kumbuka kila kitu kinatakiwa kiwe standard
Na isipokua standard inakua shida tena😀
 
Mheshimiwa Raisi yupo sahihi kabisa, kwa milioni 40 with effective supervision unajenga kama hiyo
Milioni arobaini hapana, ila kwa mil 100 au zaidi nakubali. Hapo hujui tiles wameka za viwango gani, bati hiyo ni gauge 28 , ratio ya zege hapo ni kama ya madaraja. Mi nadhani kama imefuata standard zile za serikali kabisa inaweza kufika hata mil 120 au zaidi. Tusiwe emotional Sana kwenye haya mambo, tuwe logical. Hapo huenda kila kona ya nyumba kuna nguzo, hapo tayari gharama inaongezeka, huenda katikati ya msingi na lintel kuna ring beam nyingine.
 
Kama kuna finishing touches nzuri huko ndani, na structure ilijengwa kwa viwango stahiki, no way hiyo nyumba ni less than 100m.. mnaosema milioni sijui 60, 70 mnaongelea very low qualoty houses...
Ni kweli kabisa mkuu
 
Huwezi mkuu, nyumba za serikali hazijengwi na vifaa vya ujenzi vya hovyo hovyo.
Tofali grade one tena za kulaza mara nyingi, ratio ya cement ya hali ya juu na bati gauge 26.
Huwa mnakurupuka mnalinganisha na vibanda vyetu vya mtaani.
Pili huwa kuna bei ya elekezi ya ujenzi mfano mdogo...
...majengo ya hospitali cost/sqm huwa ni 850,000
...magodauni cost/aqm ni 500,000
Msiwe mnakurupuka kama rais wetu.

Huwezi kuzunguka nyumba eti ukapata gharama za ujenzi.
Pitia manunuzi na pitia kitabu cha consultants uone mapendekezo yao katika ujenzi pamoja na samani zilizopo ndani
Well said
 
Hiyo nyumba tuseme kupaua ni milioni 10
Msingi na jamvi milion 10.
Kupandisha tofali juu milion 10
Finishing milion 15
Ziada milini 10.

Jumla milioni 55!

Magu yupo sahihi hapo pana upigaji!

Kwa hiyo hela milioni 143 ilitakiwa zitoke nyumba kama hizo 3
Sio kweli mkuu, tofali moja iliyotumika hapo haipungui 2200 kwasababu ratio ya tofari ya serikali ni kali na tofari ni mpaka ipelekwe maabara kupimwa. Wakuu tusipngee kwa mihemko. Ratio ya zege hapo ni kama ya madaraja ya mfugale. Hiyo nyumba kama imefuata standard zote za serikali inaweza isipungue 120M
 
Shida ujenzi wa miradi ya serikali unapitia mikononi ya wadau wengi. Utasikia injinia mshauri,mara project designer n.k na pia maelekezo ya kutaka ujenzi kuzingatia viwango maalum.Mfano mfuko wa simenti 1:20 tofali wakati nyumba binafsi ni 1:40. Vivyo hivyo kwenye bati n.k Matokeo yake kitu kidogo au nyumba ndogo thamani yake inakuwa kubwa. Hivyo binafsi sishangai hiyo thamani ni reasonable kabsa.
Kwa standard za serikali hiyo thamani ni sahihi kabisa kama imefuata standard zote
 
Tufanye tunakubaliana na wewe, embu jaribu kutupigia 'rafu' tuone.

Ninavyojua ni kwamba, nenda chini,fukua msingi urefu utakavyo, laza tofari upendavyo, weka 'resho' unayoitamani hata ya karai15 kwa mfuko, hiyo nyumba haiwezi kumeza tofari zaidi ya 6000÷20×20,000/=? na mifuko 200×20'000/= ya kujengea pamoja na ripu, tufanye na 100 kwa ajili ya tiles jumla mifuko 600.

Weka bati hizo za migongo mipana 200×33,000/=?
Mbao za size mbalimbali hazizidi 500×12,000/=?
Hapa hatujapigia nondo na vifaa vingine vya msingi kwenye finishing, lakini tupo kwenye ishirini na,30haijakatika.

Embu isongeshe kwenye mchanga, nondo, tiles rangi,misumari, alluminium na grill, milango, wiring, gipsum uone kama inavuka70?
Gharama za ujenzi tunazikuza sana kwa nakusudi ajili ya aslahi binafsi ama kutokujua hadi tunaingia uoga na kupelekea watu kusalia hadi kufia 'mapangoni'
Hapo unapiga hesabu mifuko ya saruji, piga hesabu ya matofari mzee. Tofali moja haipungui sh.2000 maana ratio yake ni kali sana.kokoto hawatumii chafu, wanatumia zile za barabarani
 
Mheshimiwa Raisi yupo sahihi kabisa, kwa milioni 40 with effective supervision unajenga kama hiyo
ndiyo shida ya mambo ya zabuni na tenda. Siku zote lazima iwe juu. Ila wanhetumoamJKT tungeambiwa 20M maana free labour
 
Huwezi mkuu, nyumba za serikali hazijengwi na vifaa vya ujenzi vya hovyo hovyo.
Tofali grade one tena za kulaza mara nyingi, ratio ya cement ya hali ya juu na bati gauge 26.
Huwa mnakurupuka mnalinganisha na vibanda vyetu vya mtaani.
Pili huwa kuna bei ya elekezi ya ujenzi mfano mdogo...
...majengo ya hospitali cost/sqm huwa ni 850,000
...magodauni cost/aqm ni 500,000
Msiwe mnakurupuka kama rais wetu.

Huwezi kuzunguka nyumba eti ukapata gharama za ujenzi.
Pitia manunuzi na pitia kitabu cha consultants uone mapendekezo yao katika ujenzi pamoja na samani zilizopo ndani
Mkuu umeongea point, watu wanalinganisha na zile Nyumba za chanika zinazouzwa m40 wakati zimejengwa na tofali za biskuti bati g30. Tofali za serikali mfuko mmoja unatoa tofali 20-25
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Nyumba ya kawaida sana million 140 sio kweli labda kama kiwanja wameuziwa million 100 mikochen
 
Kama kuna finishing touches nzuri huko ndani, na structure ilijengwa kwa viwango stahiki, no way hiyo nyumba ni less than 100m.. mnaosema milioni sijui 60, 70 mnaongelea very low qualoty houses...
Wewe wacha mambo yako Rais amesema milioni 43!
 
Back
Top Bottom