Ujenzi maghorofa ya Magomeni kuanza. TBA waahidi kuukamilisha kwa wakati

Ujenzi maghorofa ya Magomeni kuanza. TBA waahidi kuukamilisha kwa wakati

Sheria ya manunuzi imekufa??? siioni wapi procurement imefanyika, tuendako ni kugumu.
Nenda PPRA, ukapate unayohitaji, huyu mleta mada kaleta taarifa kwa ufupi kinachoendelea, maswala mengine nenda kachimbe sehemu stahiki ujiridhushe
 
Lupyee....alietaja humu mambo ya chama ni nani...??
 
Nadhani ilishafanyiwa marekebisho, hata hivyo serikali ina wataalamu wake wenye uwezo wa kusimamia na kujenga kwa kuwalipa per diem/allowances kwa nini waingie gharama ya mabilioni ya ziada ilhali kuna watu inawalipa mishahara

Hiyo sheria imefanyiwa marekebisho lini? Tuambie hiyo sheria iko wapi nasi tuipitie. Kwa conlusion yako hapo juu unaeleza kuwa serikali ina wave taratibu na sheria za manunuzi ikiamua, na hii ni sahihi?!
 
Hiyo sheria imefanyiwa marekebisho lini? Tuambie hiyo sheria iko wapi nasi tuipitie. Kwa conlusion yako hapo juu unaeleza kuwa serikali ina wave taratibu na sheria za manunuzi ikiamua, na hii ni sahihi?!
Kuna kitu wahandisi na wahasibu wanaita "forced account"!Hapa wahasibu na watu wa manunuzi huitumika kuagiza materials kama ilivyo kwenye makadirio ya wahandisi na ujenzi hufanywa na vibarua na mitambo ya serikali chini ya usimamizi wa wahandisi wa serikali!Mfano ni kama daraja la ruvu likikatika huwezi kufuata sheria ya manunuzi ili kujenga daraja mbadala, au kama gharama ya kujenga structure kwa wakandarasi amabyo wame bid ni kubwa kuliko makadirio ya mhandisi na pesa iliyotengwa napo pia "forced account" hutumika!
 
ZIKIWA zimepita siku 20 tangu Rais John Magufuli atoe ahadi ya ujenzi wa nyumba za kisasa katika eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam, Wakala wa Majengo nchini (TBA) umesema unatarajia kuanza ujenzi huo rasmi Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Elius Mwakalinga alisema kuwa tayari serikali imewapa Sh bilioni tano, kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.

“Tunashukuru serikali kwa kutoa fedha tunachoweza kuahidi sisi ni kupiga kazi ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati,” alisema Mwakalinga.

Alisema kuwa baada ya Rais, kuwataka TBA kuanza ujenzi huo mara moja, na kwamba tangu Septemba 20 mwaka huu, ulianza kwa hatua za mwanzo ikiwa ni pamoja kuandaa michoro na kurejesha mipaka ya eneo hilo ambayo itasaidia katika kupanga nyumba zinazotarajiwa kujengwa.

Aidha alisema kuanza kwa ujenzi huu kunatarajia kutengeneza ajira zaidi ya 600 kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa siku moja.

Aliongeza kuwa ujenzi huo, utakuwa na nyumba tano zenye ghorofa nane kila moja ambazo zitawaweka wakazi 644 waliobomolewa nyumba zao mwaka 2011, majengo mawili ya ofisi pamoja na majengo ya biashara.

Aidha, alisema nyumba hizo hazitawanufaisha wale waliobomolewa nyumba zao pekee bali hata wananchi wengine wanaweza kunufaika na nyumba hizo.

Hata hivyo, Mwakalinga alisema eneo linalotarajiwa kujengwa nyumba hizo ni ekari 13 pekee kati ya ekari zaidi ya 30 zilizopo. Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa Mradi huo, Humprey Killo, alisema kwa sasa wanaendelea kutoa udongo wenye rutuba ambao hauhitajiki katika ujenzi baada ya kukamilika wataanza kuchimba misingi kwa ajili ya ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika baada ya miezi 12.

Hivi karibuni wakati Rais akiweka jiwe la msingi katika eneo hilo, alisema ahadi ya ujenzi wa nyumba za kisasa katika eneo hilo, itaanza kutekelezwa ndani ya miezi miwili na ujenzi wa nyumba hizo utakamilika ndani ya mwaka mmoja, ambapo wakazi hao 644 watapatiwa nyumba za kuishi watakazoishi kwa muda wa miaka mitano bure.

Alisema wakazi hao waliotabika kufuatilia haki yao mahakamani kwa muda wa miaka mitano tangu mwaka 2012 walipotolewa kwenye nyumba hizo, watapatiwa nyumba hizo za kisasa kulingana na taarifa zao na orodha ya majina yao ambayo Rais huyo anayo.


Chanzo: Habarileo
hivi kama unakumbuka waliahidiwa kuuziwa kwa bei rahisi ndo hayo maghorofa watanunua kweli hasa ukiangalia hali ya wale waliokuwa wanalalamika kwenye ule mkutano
 
Sheria ya manunuzi imekufa??? siioni wapi procurement imefanyika, tuendako ni kugumu.

sheria ya manunuzi ni ya kinafki ndiko serikali inapomalizia pesa, zetu za kodi , na 10% za viongozi na huko ndiko upanuzi, wa Dar ulikojengwa kwa 600b,
biki ina ya 200 inauzwa kwa 96usd ,
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Kuna kitu wahandisi na wahasibu wanaita "forced account"!Hapa wahasibu na watu wa manunuzi huitumika kuagiza materials kama ilivyo kwenye makadirio ya wahandisi na ujenzi hufanywa na vibarua na mitambo ya serikali chini ya usimamizi wa wahandisi wa serikali!Mfano ni kama daraja la ruvu likikatika huwezi kufuata sheria ya manunuzi ili kujenga daraja mbadala, au kama gharama ya kujenga structure kwa wakandarasi amabyo wame bid ni kubwa kuliko makadirio ya mhandisi na pesa iliyotengwa napo pia "forced account" hutumika!

Nijuavyo mimi kuna 'emergency' procurement kwa situation kama hiyo uliyoitaja hapo juu, na zaidi method inayotumika kwenye nature ya namna hiyo ni 'single source procurement', na hiyo ina procedure zake nenda kwenye msaafu utakuta vifungu kwenye sheria za manunuzi utaikuta, nayo haiko bwerere ina utaratibu wake wa kutosha ki emergency hivyo hivyo. PPRA hawakuachi bure bila kukamilisha hizo taratibu ndugu.
 
Mafisadi Chadema watajinyonga kwa wivu wao leo miaka 20 hata ofisi imewashinda wamepanga makaburini ufipa!!!.

Mungu akubaliki sana Magufuli
WANAKUFA HUKO WALIKO
 
HAKIKA MAGUFULI NI MTU WA VITENDO ZAIDI
 
sheria ya manunuzi inaanzia kwenye upatikanaji wa washauri wataalamu wa mradi (consultants) then wakandarasi (contractors)then subcontractors then suppliers. slikakali au taasisi yake haiwezi kuwa Cliet, alafu consultant alafu contractor alafu subcontractor alafu supliers. sheria ya manunuzi inakataza
et serikali haiwezi kuwa client hivi we hata client unajua maana yake kweli, au niambie ni wapi au kifungu gani serikali haiwezi kuwa client au unasomasoma tu hat huelewi maana yake
 
Back
Top Bottom