Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

Ni mradi mzuri kwa Dr.Dau kustaafu nao hapo atakula kiulaini.Dr.Dau kaekeza sana kigamboni ndiyo maana hata daraja ni muhimu sana kwake kuliko

Binafsi ninawashukuru sana NSSF kwa uwekezaji mkubwa katika Jimbo la Kigamboni. Ujenzi wa Daraja, ujenzi wa nyumba 600 za Toangoma, mradi wa Azimio na ule utakaoanza hivi karibuni eneo la Dungu ni mchango mkubwa sana kwa wana-Kigamboni.
Nitakuwa mchoyo wa Fadhila kama sitawapongeza NHC pia kwa uwekezaji wa kasi maeneo ya Kibada na hivi karibuni kwenye eneo la Mwongozo.Ukweli lazima tuuseme na tutoe pongezi panapostahili.
 
Safi sana Hon Dr..! Sisi wakazi wa Kijiji cha Kijaka pamoja na Kata nzima ya Kimbiji tunatarajia makubwa toka kwenu!!

Baba Deo!

Tumefikisha umeme Kimbiji. Kimbiji inakuwa kwa kasi hususan baada ya Ujenzi wa Kiwanga cha simenti.

Wafanyakazi wa Kiwanda hiki wanaishi Kisota na hakuna sehemu nzuri za kula kwa watumishi.

Nitoe rai kwa wadau kuwekeza kwenye makazi na huduma nyingine za muhimu kwa jamii. Kimbiji inakuwa kwa kasi sana.

Tembeleeni muone.
 
Ni kweli Hon Dr.!! Tutajitahidi tufanye kauwekezaji kadogo ila jambo la kusikitisha eneo langu ni eneo lililokataliwa kupimwa na Manispaa wanasema ni eneo tarajiwa la jeshi. Naomba tusaidie Hon Dr.
 
Hakuna sheria inayokukataza kuendeleza eneo lako. Zuio lilikoma Oktoba 2010.

Mh mbunge, mimi nina site yangu karibia na mradi wa iqbal sijatembelea huko muda mrefu, nilipoenda hivi karibuni nimekuta nyumba nyingi karibu na huo mradi zimepigwa chapa ya azimio nilivyoulizia nikaambiwa hizo nyumba iqbal ameshazinunua hivyo hilo eneo limekuwa la iqbal.

Swali langu: kama mimi sitaki kuuza sehemu yangu itakuwaje? je ni lazima?
naomba unisaidie kunifafanulia muheshimiwa mbunge
 
Hakuna sheria inayokukataza kuendeleza eneo lako. Zuio lilikoma Oktoba 2010.
Mkuu una uhakika? ... Unaweza kutupa documents?
Maana nasikia KDC inakuja, na imeongezewa mpaka pemba mnazi, buyuni hata kuweka nguzo tunakatazwa.
 
Mh.F.Ndungulile,kunajambo moja nataka kujua kutoka kwako,ila nisingependa kulianika hapa,nipe japo karuksa,niku-pm.
 
Huu ndiyo mfano wa mawasiliano yenye tija. Kama viongozi wetu wangelikuwa wawazi kiasi hiki basi kashfa ya Dar kuitwa Rumourville ingejifia kifo cha asili. Hongereni sana wanaJF na Ndugu Mbunge kwa kuonesha nini maana ya kujibu kero za umma kwa wakati bila unyani wowote.
 
Mh mbunge, mimi nina site yangu karibia na mradi wa iqbal sijatembelea huko muda mrefu, nilipoenda hivi karibuni nimekuta nyumba nyingi karibu na huo mradi zimepigwa chapa ya azimio nilivyoulizia nikaambiwa hizo nyumba iqbal ameshazinunua hivyo hilo eneo limekuwa la iqbal.

Swali langu: kama mimi sitaki kuuza sehemu yangu itakuwaje? je ni lazima?
naomba unisaidie kunifafanulia muheshimiwa mbunge
Ninavyojua wamiliki wa ardhi ndio wanamuuzia mwekezaji huyu. Si lazima kuuza na wala ulazimishwi. Ila nikushauri kutembelea eneo lako mara kwa mara kwani utapeli wa ardhi unazidi kuongezeka.
 
Mkuu una uhakika? ... Unaweza kutupa documents?
Maana nasikia KDC inakuja, na imeongezewa mpaka pemba mnazi, buyuni hata kuweka nguzo tunakatazwa.

Si kweli! Kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji na 8 ya 2007 na tamko la Serikali, zuio la kutoendeleza eneo halitozidi miaka miwili. Tamko lilitolewa tarehe 28 Oktoba 2008. Miaka miwili iliisha Oktoba 2010.

Kigamboni Development Authority (KDA) ilishaanzishwa ila bado inasua sua. Ni kweli eneo la mradi limeongezwa hadi kata ya Pemba Mnazi ila si kweli kwamba unakatazwa kuweka Alana za mipaka kwenye eneo lako. Weka nguzo kama unataka kwenye eneo lako.
 
Mtuombee sisi wajumbe wa Bunge la Katiba ili hekima, busara na maslahi mapana ya Tanzania yazingatiwe. Hiki ni kipindi muhimu na nyeti sana kwa ustawi wa Taifa letu.

Msitekwe akili kwa manufaa ya wana ccm toka zanzibar wenye uchu wamadaraka huku tanganyika ili hali wewe mtanganyika huna ruhusa y kumiliki ardhi wala kuwa kiongozi zanzibar
 
Mh tunashukuru kwa michango yako yenye tija na tunajivunia kuwa na mbunge msikivu na mtendaj mahiri rai yangu ni kuhusu huu mrad wa nyumba za wanajesh hapa shinyanga karibu na kimbiji ambao unaendeshwa na wachina kuna dhuruma kubwa na manyanyaso makubwa wananchi wako wanatendewa dhidi ya ardhi yao wanalazimishwa kuhama pasipo makubaliano naomba lifuatilie hili kwani we ndo mtetezi wao
 
Wana jamvi kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa magorofa unaendelea Kigamboni. Ni Kigamboni ndandani mbele Zoo. Wengi wa wafanyakazi ni wazungu wenye asili ya Kigiriki. Kazi inafanyika usiku na mchana. Wenye ukweli kuhusu mradi huo mtujuze. Karibuni wanajamvi.
Asante ndugu mbunge kwa ufafanuzi mzuri, maana walishajipanga kwa majungu
 
Si kweli! Kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji na 8 ya 2007 na tamko la Serikali, zuio la kutoendeleza eneo halitozidi miaka miwili. Tamko lilitolewa tarehe 28 Oktoba 2008. Miaka miwili iliisha Oktoba 2010.

Kigamboni Development Authority (KDA) ilishaanzishwa ila bado inasua sua. Ni kweli eneo la mradi limeongezwa hadi kata ya Pemba Mnazi ila si kweli kwamba unakatazwa kuweka Alana za mipaka kwenye eneo lako. Weka nguzo kama unataka kwenye eneo lako.

Mh Mbunge mi ningeomba unifahamishe kitu kimoja! Kuna uvumi mitaana kwamba kigamboni baadhi ya sehemu itakua chini ya Wamarekani! Nini majibu yako kutokana na huu uvumi?
 
Ninavyojua wamiliki wa ardhi ndio wanamuuzia mwekezaji huyu. Si lazima kuuza na wala ulazimishwi. Ila nikushauri kutembelea eneo lako mara kwa mara kwani utapeli wa ardhi unazidi kuongezeka.

Asante muheshimiwa mbunge wetu kwa majibu yako, kwani yanatuondolea sintofahamu tulizonazo wapiga kura wako.

Baada ya kukuta hiyo hali niliamua kuanza kupaendeleza kwani eneo langu ni zuri na nalipenda sana nilikuwa sijafikiria kupauza hata kidogo.

Swali lingine mheshimiwa: mradi wa kigamboni umeishia wapi?maana waliothamini kibada hawajalipwa hadi leo na wengine bado nyumba zetu hazijathaminiwa . Ninaishi kibada mtaa wa uvumba
 
Mtuombee sisi wajumbe wa Bunge la Katiba ili hekima, busara na maslahi mapana ya Tanzania yazingatiwe. Hiki ni kipindi muhimu na nyeti sana kwa ustawi wa Taifa letu.

Mh Mbguge, kuna uwezekano Wa bunge la katiba kurushwa live Au ndio itakua hivi hivi kimyakimya?
 
Najua kuna wabunge wengi humu lakini wanashindwa kuonyesha ushirikiano, kwa hilo nakupa pongezi Mb: Dr ndungulile. Na wabunge wengine waige mfano wako. Maana wabunge wengi majimboni hawaonekani kwa hivyo kwenye mitandao ya kijamii inaweza ikawa sehemu mojawapo ya kusikiliza kero na sitofahamu kutoka kwa jamii.
 
Back
Top Bottom