Si Kweli! Uvumi unaotoka na kutakuwa na taarifa sahihi. Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mradi wa Serikali wa kujenga Mji mbadala pembezoni mwa DSM. Wazo la Mji Mpya wa Kigamboni ni zuri na wananchi wanaliunga mkono. Matatizo yapo kwenye utekelezaji. Matatizo yenyewe ni kama yafuatayo:
1. Sheria zinazosimamia mchakato huu ni nzuri (Sheria ya Ardhi na.4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Mipango Miji na.8 ya 2007). Wanaovunja Sheria ni watendaji wa Wizara ya Ardhi na sio wananchi. Wananchi wanataka Serikali ifuate Sheria.
2. Ushirikishwaji: Watendaji wa Wizara ya Ardhi wanataka haki ya mwananchi kama mmiliki wa ardhi ianze na kuishia katika kulipwa fidia pekee. Wananchi wanataka wawe wadau katika mradi huu na kupewa kipaumbele cha kwanza kwenye ardhi yao.
3. Kumekuwa na usiri na sintofahamu kuhusu haki, Stahili na hatma za wananchi wa Kigamboni: Wananchi wanataka washirikishwe kikamilifu na haki zao ziwekwe wazi na waziafiki.
4. Ucheleweshaji mkubwa wa mradi: Kwa muda wa miaka Sita wananchi wa Kigamboni hawajanipa, hawakarabati, hawawezi kuuza Nyumba wala viwanja vyao na hawakopesheki kwenye mabenki. Hali inayoletea unyonge na kudumaza maendeleo yao binafsi.
Matatizo haya yakitatuliwa, mradi unaweza kupokelewa vizuri zaidi na wananchi.