Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

Asante Mh: Mbunge wangu,
Mimi ni mkazi wa Kigamboni na nina uwekezaji wa ardhi kwenye maeneo mbalimbali ya kigamboni.
Nina mpango wa kufanya uwekezaji wa hela nyingi kiasi Mwasonga, je kuna hatari yeyote ya kuniua kwa presha kulingana na mipango ya serikali[?
Pili tumeona kweli umeme umefika Kimbiji na maendeleo ni ya kasi, je na Mwasonga mipango ipo vipi?
Natanguliza Shukrani
QUOTE=Dr F. Ndugulile;8803138]Baba Deo! Tumefikisha umeme Kimbiji. Kimbiji inakuwa kwa kasi hususan baada ya Ujenzi wa Kiwanga cha simenti.
Wafanyakazi wa Kiwanda hiki wanaishi Kisota na hakuna sehemu nzuri za kula kwa watumishi.
Nitoe rai kwa wadau kuwekeza kwenye makazi na huduma nyingine za muhimu kwa jamii. Kimbiji inakuwa kwa kasi sana. Tembeleeni muone.[/QUOTE]
 
Mh tunashukuru kwa michango yako yenye tija na tunajivunia kuwa na mbunge msikivu na mtendaj mahiri rai yangu ni kuhusu huu mrad wa nyumba za wanajesh hapa shinyanga karibu na kimbiji ambao unaendeshwa na wachina kuna dhuruma kubwa na manyanyaso makubwa wananchi wako wanatendewa dhidi ya ardhi yao wanalazimishwa kuhama pasipo makubaliano naomba lifuatilie hili kwani we ndo mtetezi wao
Hili nilalifahamu. Wakazi wa eneo hili walilipeleka shauri mahakamani. Bado tunafuatilia katika ngazi nyingine za maamuzi.
 
Asante muheshimiwa mbunge wetu kwa majibu yako, kwani yanatuondolea sintofahamu tulizonazo wapiga kura wako.

Baada ya kukuta hiyo hali niliamua kuanza kupaendeleza kwani eneo langu ni zuri na nalipenda sana nilikuwa sijafikiria kupauza hata kidogo.

Swali lingine mheshimiwa: mradi wa kigamboni umeishia wapi?maana waliothamini kibada hawajalipwa hadi leo na wengine bado nyumba zetu hazijathaminiwa . Ninaishi kibada mtaa wa uvumba

Suala la tathmini ya Mji Mpya wa Kigamboni katika Mitaa ya Kifurukwe na Uvumba, kata ya Kibada bado ni kitendawili, changamoto hapa ni upatikanaji wa fedha, waliosema pesa ipo, hawakuwa wakweli.
 
Hii post imenifundisha kuwa watanzania tuna kiu na kero nyingi lakini hatuna fursa ya namna ya kuwafikishia
viongozi wetu husika,hii iwape fundisho wabunge wetu kuwa tunahitaji ukaribu wenu.Hongera Mh.Dr.F.Ndungulile
 
Asante Mh: Mbunge wangu,
Mimi ni mkazi wa Kigamboni na nina uwekezaji wa ardhi kwenye maeneo mbalimbali ya kigamboni.
Nina mpango wa kufanya uwekezaji wa hela nyingi kiasi Mwasonga, je kuna hatari yeyote ya kuniua kwa presha kulingana na mipango ya serikali[?
Pili tumeona kweli umeme umefika Kimbiji na maendeleo ni ya kasi, je na Mwasonga mipango ipo vipi?
Natanguliza Shukrani
QUOTE=Dr F. Ndugulile;8803138]Baba Deo! Tumefikisha umeme Kimbiji. Kimbiji inakuwa kwa kasi hususan baada ya Ujenzi wa Kiwanga cha simenti.
Wafanyakazi wa Kiwanda hiki wanaishi Kisota na hakuna sehemu nzuri za kula kwa watumishi.
Nitoe rai kwa wadau kuwekeza kwenye makazi na huduma nyingine za muhimu kwa jamii. Kimbiji inakuwa kwa kasi sana. Tembeleeni muone.
[/QUOTE]

Mwasonga, kata ya Kisarawe II ni eneo linalokuwa kwa kasi. Kuna DSM Zoo, Camel Oil wanajenga Kiwanda cha naziwasilisha, kuna uchimbaji wa visima vya maji vya Dasawa na mpango wa Ujenzi wa chuo kikubwa cha Kilimo na teknolojia cha Wakorea n.k.

Kwa sasa umeme umefika eneo la Camel Oil. Lengo langu umeme ufike Mwasonga centre. Tumekuwa na changamoto ya fidia kwa sehemu zitakazopita nguzo na nyaya. Bado tunaendelea kufanya majadiliano na baadhi ya wakazi waliokuwa wamegomea zoezi hili.
 
Mtuombee sisi wajumbe wa Bunge la Katiba ili hekima, busara na maslahi mapana ya Tanzania yazingatiwe. Hiki ni kipindi muhimu na nyeti sana kwa ustawi wa Taifa letu.

Kwenye kATIBA hapo nyie wajumbe wa magamba hamna lolote mtakuwa watu wakugonga meza tu jambo lolote lenye maslahi kwa CCM bila kujali maslahi ya wananchi. Nyie mnajali MAFISADI tu sitashangaa mkimpitisha Fisadi CHENGE kuwa mwenyekiti.
 
Nashukuru kwa mtazamo wako.
 
Nashukuru kwa mtazamo wako.

Mh Mbunge mi Nikuombe tu uwe mvulivu ktk kupokea maoni mbalimbali ya Watu! Na pia nikupongeze kwa ujasili wako Wa kuwepo humu JF mojakwamoja! Tunawaitaji sn viongozi wetu kubadilishana Mawazo kidogo!

Jaribu kuwambia na waheshimiwa wabunge wenzako waje humu tuwe tunajadiliana nao na kusikia Kero za wananchi Moja kwa Moja!

Asante sn Mkuu!
 
Mh Mbunge mi ningeomba unifahamishe kitu kimoja! Kuna uvumi mitaana kwamba kigamboni baadhi ya sehemu itakua chini ya Wamarekani! Nini majibu yako kutokana na huu uvumi?

Mh Dr F. Ndugulile swali lenyewe ni hilo Hapo juu!
 
Last edited by a moderator:
Mh Mbunge mi Nikuombe tu uwe mvulivu ktk kupokea maoni mbalimbali ya Watu! Na pia nikupongeze kwa ujasili wako Wa kuwepo humu JF mojakwamoja! Tunawaitaji sn viongozi wetu kubadilishana Mawazo kidogo!

Jaribu kuwambia na waheshimiwa wabunge wenzako waje humu tuwe tunajadiliana nao na kusikia Kero za wananchi Moja kwa Moja!

Asante sn Mkuu!
Nami nafurahi kuwa hapa kwani nafasi hii inanipa fursa ya kujifunza mengi. Niombe mijadala iwe yenye tija na staha kwa faida ya wote.
Najua kuwakuna Wabunge na Mawaziri humu ndani, wengi wanaingia kwa ID tofauti na si majina yao halisi.
Katika ulimwengu wa teknolojia, forums na social media ni mfumo mzuri wa mawasiliano iwapo unatumika vizuri.
 
Nashukuru Mheshimiwa kwa kujibu swali langu moja la umeme, ingawa la pili kuhusu uwekezaji hujalijibu moja kwa moja.

Naomba niongeze swali lingine, je eneo la Kijaka inafaa kuliendeleza kwa ujenzi wa nyumba au kuna masuala yeyote ya kiserikali?

Mwasonga, kata ya Kisarawe II ni eneo linalokuwa kwa kasi. Kuna DSM Zoo, Camel Oil wanajenga Kiwanda cha naziwasilisha, kuna uchimbaji wa visima vya maji vya Dasawa na mpango wa Ujenzi wa chuo kikubwa cha Kilimo na teknolojia cha Wakorea n.k.

Kwa sasa umeme umefika eneo la Camel Oil. Lengo langu umeme ufike Mwasonga centre. Tumekuwa na changamoto ya fidia kwa sehemu zitakazopita nguzo na nyaya. Bado tunaendelea kufanya majadiliano na baadhi ya wakazi waliokuwa wamegomea zoezi hili.[/QUOTE]
 
Nami nafurahi kuwa hapa kwani nafasi hii inanipa fursa ya kujifunza mengi. Niombe mijadala iwe yenye tija na staha kwa faida ya wote.
Najua kuwakuna Wabunge na Mawaziri humu ndani, wengi wanaingia kwa ID tofauti na si majina yao halisi.
Katika ulimwengu wa teknolojia, forums na social media ni mfumo mzuri wa mawasiliano iwapo unatumika vizuri.

Ni Kweli Mkuu!

Asante sn kwa maelezo yako!
 
Mh Dr F. Ndugulile swali lenyewe ni hilo Hapo juu!

Si Kweli! Uvumi unaotoka na kutakuwa na taarifa sahihi. Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mradi wa Serikali wa kujenga Mji mbadala pembezoni mwa DSM.

Wazo la Mji Mpya wa Kigamboni ni zuri na wananchi wanaliunga mkono. Matatizo yapo kwenye utekelezaji. Matatizo yenyewe ni kama yafuatayo:

1. Sheria zinazosimamia mchakato huu ni nzuri (Sheria ya Ardhi na.4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Mipango Miji na.8 ya 2007). Wanaovunja Sheria ni watendaji wa Wizara ya Ardhi na sio wananchi. Wananchi wanataka Serikali ifuate Sheria.

2. Ushirikishwaji: Watendaji wa Wizara ya Ardhi wanataka haki ya mwananchi kama mmiliki wa ardhi ianze na kuishia katika kulipwa fidia pekee. Wananchi wanataka wawe wadau katika mradi huu na kupewa kipaumbele cha kwanza kwenye ardhi yao.

3. Kumekuwa na usiri na sintofahamu kuhusu haki, Stahili na hatma za wananchi wa Kigamboni: Wananchi wanataka washirikishwe kikamilifu na haki zao ziwekwe wazi na waziafiki.

4. Ucheleweshaji mkubwa wa mradi: Kwa muda wa miaka Sita wananchi wa Kigamboni hawajanipa, hawakarabati, hawawezi kuuza Nyumba wala viwanja vyao na hawakopesheki kwenye mabenki. Hali inayoletea unyonge na kudumaza maendeleo yao binafsi.

Matatizo haya yakitatuliwa, mradi unaweza kupokelewa vizuri zaidi na wananchi.
 
Nakupongeza mh. Mbunge Dr F. Ndugulile kwa kutumia muda huu kwa kujibu hoja mbali mbali za wanananchi tofauti na wengi wa chama chako wapo humu lakini kwa ID fake.

Hongera sana mkuu
 
Si Kweli! Uvumi unaotoka na kutakuwa na taarifa sahihi. Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mradi wa Serikali wa kujenga Mji mbadala pembezoni mwa DSM.

Wazo la Mji Mpya wa Kigamboni ni zuri na wananchi wanaliunga mkono. Matatizo yapo kwenye utekelezaji. Matatizo yenyewe ni kama yafuatayo:

1. Sheria zinazosimamia mchakato huu ni nzuri (Sheria ya Ardhi na.4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Mipango Miji na.8 ya 2007). Wanaovunja Sheria ni watendaji wa Wizara ya Ardhi na sio wananchi. Wananchi wanataka Serikali ifuate Sheria.

2. Ushirikishwaji: Watendaji wa Wizara ya Ardhi wanataka haki ya mwananchi kama mmiliki wa ardhi ianze na kuishia katika kulipwa fidia pekee. Wananchi wanataka wawe wadau katika mradi huu na kupewa kipaumbele cha kwanza kwenye ardhi yao.

3. Kumekuwa na usiri na sintofahamu kuhusu haki, Stahili na hatma za wananchi wa Kigamboni: Wananchi wanataka washirikishwe kikamilifu na haki zao ziwekwe wazi na waziafiki.

4. Ucheleweshaji mkubwa wa mradi: Kwa muda wa miaka Sita wananchi wa Kigamboni hawajanipa, hawakarabati, hawawezi kuuza Nyumba wala viwanja vyao na hawakopesheki kwenye mabenki. Hali inayoletea unyonge na kudumaza maendeleo yao binafsi.

Matatizo haya yakitatuliwa, mradi unaweza kupokelewa vizuri zaidi na wananchi.

Hapo katika uvunjaji wa sheria mawizarani ndipo panapoifanya serikali hii ipo ipo tu. Ina maana viongozi wakuu wa kitaifa hawalioni hilo la uvunjaji sheria wizara ya ardhi?

Na hatua gani mbadala zinachukuliwa. Inakuwa ni ndoto sasa kuhusu mpango wa mji mpya Kigamboni.

Hili wananchi hatutawasamehe
 
Ni mradi mzuri kwa Dr.Dau kustaafu nao hapo atakula kiulaini.Dr.Dau kaekeza sana kigamboni ndiyo maana hata daraja ni muhimu sana kwake kuliko
Uko sahh mkuu Dr Dau kawekeza sana ,yupo ufukwen kabisa,na nilishafanya kaz kwake.ana nyumba kama 3 za gorofa na eneo la kutosha pamoja Adamu malima MB mkulanga.
 
4. Ucheleweshaji mkubwa wa mradi: Kwa muda wa miaka Sita wananchi wa Kigamboni hawajanipa, hawakarabati, hawawezi kuuza Nyumba wala viwanja vyao na hawakopesheki kwenye mabenki. Hali inayoletea unyonge na kudumaza maendeleo yao binafsi.

Matatizo haya yakitatuliwa, mradi unaweza kupokelewa vizuri zaidi na wananchi.
Mh. Mbunge, Asante sana kwa majibu yako mazuri na Moyo wako Wa uwazi na uwajibikaji!

Naamini kutokana na maelezo yako mazuri na machache Wengi tumeridhika!
 
Back
Top Bottom