Ni mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 7,000. Mradi huu ni ubia kati ya kampuni ya Azimio na NSSF.
Bw Iqbal ni mwenye eneo hilo na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Azimio.
Dkt Faustine Ndugulile
MB-Mbunge Kigamboni
Asante kwa taarifa. Ni sehemu ya mradi wa new Kigamboni?
Hapana! Huu ni mradi tofauti.
Safi sana mkuu, nimefarijika kusoma jinsi umewasiliana na wapiga kura wako!!!!
Hapana! Huu ni mradi tofauti.
Si Kweli! Uvumi unaotoka na kutakuwa na taarifa sahihi. Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mradi wa Serikali wa kujenga Mji mbadala pembezoni mwa DSM. Wazo la Mji Mpya wa Kigamboni ni zuri na wananchi wanaliunga mkono. Matatizo yapo kwenye utekelezaji. Matatizo yenyewe ni kama yafuatayo:
1. Sheria zinazosimamia mchakato huu ni nzuri (Sheria ya Ardhi na.4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Mipango Miji na.8 ya 2007). Wanaovunja Sheria ni watendaji wa Wizara ya Ardhi na sio wananchi. Wananchi wanataka Serikali ifuate Sheria.
2. Ushirikishwaji: Watendaji wa Wizara ya Ardhi wanataka haki ya mwananchi kama mmiliki wa ardhi ianze na kuishia katika kulipwa fidia pekee. Wananchi wanataka wawe wadau katika mradi huu na kupewa kipaumbele cha kwanza kwenye ardhi yao.
3. Kumekuwa na usiri na sintofahamu kuhusu haki, Stahili na hatma za wananchi wa Kigamboni: Wananchi wanataka washirikishwe kikamilifu na haki zao ziwekwe wazi na waziafiki.
4. Ucheleweshaji mkubwa wa mradi: Kwa muda wa miaka Sita wananchi wa Kigamboni hawajanipa, hawakarabati, hawawezi kuuza Nyumba wala viwanja vyao na hawakopesheki kwenye mabenki. Hali inayoletea unyonge na kudumaza maendeleo yao binafsi.
Matatizo haya yakitatuliwa, mradi unaweza kupokelewa vizuri zaidi na wananchi.
Nami Nashukuru. Tuzidi kuwasiliana ili kubadilisha mawazo kuhusu ya msingi kwa Kigamboni na Taifa letu. Sisi Wabunge sio kwamba tunakuwa kila kitu, mengine ya msingi hutoka kwa wale tunaowawakilisha.
Kama robo yenu mngekuwa hivi hakika tungekuwa tumesogea hatua za uhakika zaidi!!!!!!!Nami Nashukuru. Tuzidi kuwasiliana ili kubadilisha mawazo kuhusu ya msingi kwa Kigamboni na Taifa letu. Sisi Wabunge sio kwamba tunakuwa kila kitu, mengine ya msingi hutoka kwa wale tunaowawakilisha.
Nami Nashukuru. Tuzidi kuwasiliana ili kubadilisha mawazo kuhusu ya msingi kwa Kigamboni na Taifa letu. Sisi Wabunge sio kwamba tunakuwa kila kitu, mengine ya msingi hutoka kwa wale tunaowawakilisha.
Mimi leo nitakuwa msomaji tu mpaka kesho nifanikishe ya TANRODS yetu mh Mbunge
Dr hizo zitauzwa zitagawiwa bure kwa wananchi km mwalimu nyerere alivyofanya Magomeni ilala na kinondoni
Mkuu!
...Mkuu cha bure kinatoka wapi nchi hii....Ukipewa bure ujue kuna mtu anagharamia....Nyumba hizi zitauzwa na kupangishwa....
Nami Nashukuru. Tuzidi kuwasiliana ili kubadilisha mawazo kuhusu ya msingi kwa Kigamboni na Taifa letu. Sisi Wabunge sio kwamba tunakuwa kila kitu, mengine ya msingi hutoka kwa wale tunaowawakilisha.