Hapa naona tunadanganyana ati mtu kajenga chumba kwa 1.8m urongo mtupu! Hata ya matofali ya kuchoma na kuzeka kwa nyasi siyo hivyo! Wengine wamesema ukweli Lakini hata wa 4m si sahihi! Ila ninachojua ni kuwa maskini ndiye hujenga na tajiri hata siku moja hajengi ndo maana hadi leo akina Mo wanaishi NHC.
Kwa maskini hasa nyumba ya kwanza, Huwezi kujua gharama za nyumba maana kila ukipata senti unatupa pale. Ukianza utakuwa na daftari lakini kadri siku sinavyoenda unachoka na kulitupa huko!
Nyumba inaisha ukiwa ndani, hivyo usiogope hata kuingia wakati huna hata paa, wengi nimewaona na hapo huwa wanakuwa na ari ya kumalizia nyumba kwani kuliko akanunue nyama kilo mbili 14,000 hiyo ni bora akanunue mfuko wa cement utakaopiga matofali 25 ili aendeleze ujenzi na akale mchicha.
Maskini nimeona kuna mtu ambaye inaonesha ukuta unanyonya maji ila anafikiri ni yale ya kunawa. Aidha inawezekana ni bomba linavuja hasa kwa wale wanaotumia mabomba ya tredi si ya PPR.
Siku nyingine nitaeleza hasara ya kununua nyumba hapa TZ hasa za NHC.
Usiku mwema