Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Hapa naona tunadanganyana ati mtu kajenga chumba kwa 1.8m urongo mtupu! Hata ya matofali ya kuchoma na kuzeka kwa nyasi siyo hivyo! Wengine wamesema ukweli Lakini hata wa 4m si sahihi! Ila ninachojua ni kuwa maskini ndiye hujenga na tajiri hata siku moja hajengi ndo maana hadi leo akina Mo wanaishi NHC.

Kwa maskini hasa nyumba ya kwanza, Huwezi kujua gharama za nyumba maana kila ukipata senti unatupa pale. Ukianza utakuwa na daftari lakini kadri siku sinavyoenda unachoka na kulitupa huko!

Nyumba inaisha ukiwa ndani, hivyo usiogope hata kuingia wakati huna hata paa, wengi nimewaona na hapo huwa wanakuwa na ari ya kumalizia nyumba kwani kuliko akanunue nyama kilo mbili 14,000 hiyo ni bora akanunue mfuko wa cement utakaopiga matofali 25 ili aendeleze ujenzi na akale mchicha.

Maskini nimeona kuna mtu ambaye inaonesha ukuta unanyonya maji ila anafikiri ni yale ya kunawa. Aidha inawezekana ni bomba linavuja hasa kwa wale wanaotumia mabomba ya tredi si ya PPR.

Siku nyingine nitaeleza hasara ya kununua nyumba hapa TZ hasa za NHC.

Usiku mwema
Kwa nini unahisi unadanganywa mkuu? 1.8 isijenge chumba ? Kinakuwa na standard ipi hicho chumba?

Kama huwezi kutunza kumbukumbu ni tatizo lako sio la jumuia.

Sent
 
Inaonesha wewe ni wale wale wa kupiga talalile humu kumbe kitu hujui. Kuna jamaa kasema alijenga miaka 6, mpaka nyumba ikamilike. Unadhani ni rahisi kuweka kumbukumbu kivile, ni wachache tu! Kwani ni impresti unatakiwa kuritaya!
Nafikiri mada yenyewe hujaielewa vizuri, au labda Mimi sijaelewa,
Mada inahamasisha wasio na nyumba , ili wasiogope kujenga , zinazingatiwa very initial costs za kumiliki nyumba na sio extravagant style za ujenzi wa akina mo na bakhresa, ukisema ujenzi wa kimaskini unakuwa sahihi kabisa , Ila ukihamasisha ujenzi wa kitajiri ndo unapokosea .

Huyo aliyejenga kwa miaka sita , hafai kuwa mfano hapa , maana swala la finishing ya nyumba Ni very dynamic , inategemea na utashi wa mtu, unaweza kuamua kujenga kila siku nyumba ambayo kimsingi ilishamalizika

Sent
 
Naona wewe utapenda ligi na mimi najaribu kuelimisha kwa kutumia uzoefu. Umenikumbusha kila wakati mke wangu hupenda kuuliza ‘nyumba hii ni kama million ngapi?’ Huwa namweleza kuwa unless uwe kibopa ila kimaskini maskini ni vigumu kutunza kumbukumbu. Nakumbuka juzi juzi anajenga akanambia, unajua mwanzoni nilianza kuweka kumbukumbu lakini mwishowe nilichoka nikaacha. Hela ya kudunduliza haiwekagi kumbukumbu. Wenzetu ulaya na nchi zilizoendelea huweka kumbukumbu kwa vile mapato ni fixed hakuna kudunduliza. Jiulize unaweza kujua kwa mwezi umetumia kiasi gani?

Yaan mkuu hata kwa mwezi hujui umetumia kiasi gani? , Hii discussion ndo sababu una I spoil , sio level yako we upo juu Sana
Nyumba yangu ya kwanza nilijenga miaka 11 iliyopita , record zake zote ninazo,, japo nilifanya markebisho kadhaa mbele yake , Ila ukiniuliza initial costs Hadi nahamia nitakwambia, idadi ya tofali ipo kwa record tofali ,2200, msingi Hadi kupaua,

Sent
 
Kiongozi huyu analipa nyumba kwa mwezi Laki 6 ,hivi hii laki 6 unayompa mtu kila mwezi kama ungetafta nyumba uswahili ya 120 kwa mwezi hivi hiki kiasi kinachobaki usingeanza peleka tofali site kila mwezi ?

Maana nakwambia hiyo laki sita bado matumizi yake binafsi kwa mwezi inawezq fika hata laki nane ..
Unajua wengi huwa wanahisi akitaka kujenga basi angojee hela ya paap yaan kama ujenzi milion 20 basi aipate hapo hapo au kama pungufu basi ana 7m ndio aanze ujenzi ..

Pana jamaa yangu mpaka leo hana kiwanja kwa kuamini ipo siku atapata hela nyingi atanunua kiwanja Sehemu nzuri yaan town ,Hataki kukaa porini ...hizi akili huwa zinawagarimu watu na mwisho wasiku umri unaenda hajafanya la maana na nguvu zinaisha ,
Hakuna maisha yanaumiza kama maisha ya kupanga mzee asikwambie mtu na wengi anajidanganya kwa vile leo anapata mia mbili miatatu anahisi siku zote itakuwa hivyo ,hajui maisha yana badilika na upepo huwa una change leo unaweza kumudu kodi nya nyumba kesho utaitafuta hata ya chumba kimoja .

Maisha kiongozi yanahitaji tahadhari na kujihami sana japo wengi wakakuona we mwoga wa maisha ila watambuwe hakuna m'babe wa maisha sasa ni vyema ukachukuwa tahadhari mapema ,na watu watakuja kuelewa hili baade
Yaan umeongea point wadada wana matumizi sana lkn sasa ivi kichwa kina muuma baada ya serikali kikomaa na manunuzi ya mfumo hahaha
 
Yaan mkuu hata kwa mwezi hujui umetumia kiasi gani? , Hii discussion ndo sababu una I spoil , sio level yako we upo juu Sana
Nyumba yangu ya kwanza nilijenga miaka 11 iliyopita , record zake zote ninazo,, japo nilifanya markebisho kadhaa mbele yake , Ila ukiniuliza initial costs Hadi nahamia nitakwambia, idadi ya tofali ipo kwa record tofali ,2200, msingi Hadi kupaua,

Sent
Huwa sitaki kubishana maana kutafuta umwamba ni mambo ya kitoto, bali hapa JF natafuta majadiliano na kuelimishana. pole sana na kwaheri
 
Ujenzi unapoleta mushkeli ni kwenye finishing
Kweli kabisa maana unaweza kuwa na pesa na ukaelewana na Fundi kuanzia msingi mpaka kupaua ukajua kazi iliyobakia ni kidogo kumbe finishing ni zaidi ya msingi mpaka kupaua.Hahaaaa ujenzi konyo ndo maana wenye nyumba baadhi wanekera wapangaji.
 
Huwa nawaza.Mtu
mmoja ana milioni 30 anaamua kujenga nyumba ya kuishi kisha hana uwezo was lishe ya familia na kutatua matatizo yanayomsibu kwa haraka.Mwingine anazo hizo pesa anaamua kufungua duka au mradi wowote ba unamnyookea vizuri lakini anaishi maisha ya kupanga Ila anauwezo

.Kumudu mlo wake vizuri
.Kusomesha mtoto shuke nzuri,kulipa ada za vyuoni za watototo
Kusaidia ndugu zake
.Kumiliki usafiri
.Kutibiwa.
Baadae saana kujenga.
Je ni
yupi anaishi maisha mazuri.Je mafanikio ni kujenga nyumba au kumudu maisha?
Kwa upuuzi ulioandika sidhani hata Kama unafamilia...Sasa jisifie kulisha vizuri ukiw umepanga halafu kibarua kiote nyasi...au Mungu epushe upate janga
 
Sikia mi kazi yangu ya kwanza nlipoacha Kama vijana walivyo nkanunua kagari.....mwaka mmoja mbele nkaona naongeza starehe ela haikai...nkauza gari na kununua kiwanja na kuweka msingi....kazi ya 2 niliamka.....wakati wenzangu wananunua gari...Mimi nkachukua BOQ ya mshkaji...nkawa naitumia ile Raman nacheki gharama kubwa natafuta mafundi wa3 nawauliza gharama hiyo hiyo namchagua yule aliye cheap....nashukuru Mungu nyumba yenye Raman ya million 70.nkajikuta nmetumia nusu.....all in all ujenzi ni hatua...Kama mdau alivyosema mda mwengine unakua Hadi kibarua...nashukuru RRONDO ameniamsha kuhusu gypsum nilikua nawaza hiyo finishing ntafuata ushauri wake
 
Mkuu nikupongeze kwa hatua hii uliyofikia,upo hatua 900 mbele ya anaenza leo nikupe moyo kwamba utaimaliza.me yangu ilisimama hivi almost miaka 7,I mean 7 years bila kufanya chochote na mfukoni hela sina kila nayoipata inatosha kwa matumizi ya wakati husika tu ila sikuwahi kukata tamaa,imani yangu ilikuwa ipo siku kama nipo hai nitaimaliza

Namshukuru Mungu,ndoto yangu amenipa uwezo wa kuitekeleza.hii pic ipo Google photos niliipiga mwaka 2017 siku ya jumapili,nikiwa hapa nilikutana na mjumbe wa mtaa akaniambia pagale lako linafuga wezi kama umeshindwa si umuuzie fulani (ni jirani yangu ana hela kidogo za kubadilisha mboga) na alikuwa ameshamnunua jirani yangu wa upande wa kushoto,nilijisikia huzuni sana nakumbuka nilikosa kauli sahihi ya kumjibu nikakaa kimya na hivi lilikuwa limefurika majani nikijiangalia mfukoni hela sina dah,binadamu wanajua sana kukatishana tamaa ila sasa maisha yanaendelea.

Mpaka nafikia hatua ya kuweka bati hizo tofali zilishabadilika rangi zikawa rangi nyeusi tii!kikubwa tusikate tamaa pumzi ikiwepo pambana.View attachment 1503264View attachment 1503265View attachment 1503266
Umenipa nguvu sana yakupambana
 
Nikupongeze kwa hatua hiyo mkuu,tatizo siyo kupata rejected gypsum tatizo ni kupata zinazofanana zote quality unayoitaka unless ukubali kuchanganya tofauti tofauti,hii idea nilikutana nayo mtaani ila mimi nilikuwa nataka gypsum za GYPROC hizi zinatoka Turkey nilipopeleleza kama nitaweza kununua nzima kadhaa kisha nichanganyiwe na ambazo zimeharibika kidogo nikaambiwa kwa brand hiyo kupata mbovu siyo rahisi kutokana na zinafungwa imara sana siyo rahisi kupata damage so wakasema za hivyo nitapewa za hapa hapa za Kichina hizi zinazotengenezwa Kisarawe.

Kama siyo mtu wa kuchagua sana hilo ni wazo zuri sana kama ukilifuata una-save pakubwa.
 
Asante ndg yangu nina yangu mwaka sasa hata nimesahau kwamba nina nyumba ila ngoja niamkie tena Shukrani mkuu
 
Nikupongeze kwa hatua hiyo mkuu,tatizo siyo kupata rejected gypsum tatizo ni kupata zinazofanana zote quality unayoitaka unless ukubali kuchanganya tofauti tofauti,hii idea nilikutana nayo mtaani ila mimi nilikuwa nataka gypsum za GYPROC hizi zinatoka Turkey nilipopeleleza kama nitaweza kununua nzima kadhaa kisha nichanganyiwe na ambazo zimeharibika kidogo nikaambiwa kwa brand hiyo kupata mbovu siyo rahisi kutokana na zinafungwa imara sana siyo rahisi kupata damage so wakasema za hivyo nitapewa za hapa hapa za Kichina hizi zinazotengenezwa Kisarawe.

Kama siyo mtu wa kuchagua sana hilo ni wazo zuri sana kama ukilifuata una-save pakubwa.
Tofauti ya gypsum za Turkey na China zikishapachikwa juu,zikifungwa mikanda na rangi ni nini?! Yaani tofauti ya tiles Spanish na za Kichina unaiona kabisa. Gypsum zina tofauti gani? Nimezitumia miaka sasa sijaona tatizo,tupe shule kidogo.
 
Binafsi siyo fundi so siwezi kueleza hapa tofauti zake nyingi ila ninazo mbili,mchina zinakuwa nyembamba kidogo na ni nyepesi mno kumenyeka,but nachofanya mimi huwa nampeleleza fundi aniambie ni bidhaa gani anayoona ni bora na nzuri kisha na-compare bei naangalia tofauti zake na zile atakazosema ni za kawaida,then napiga hesabu kama nitanunua hizi zinazoonekana za kawaida nita-save kiasi gani nje ya zile zinazoonekana bora!mf:zilihitajika board 61,nikaenda K/koo Gerezani nikauliza bei ya Gyproc jumla ni 14,500/= kisha nikaenda kwa Mchina nikakuta kuna tofauti ya 2500/= nikapiga hesabu nikakuta tofauti ni Tsh 152,500/= tu nikaona bora kuchukua za Uturuki,kama ningekuwa na-save zaidi ya 500,000/= ningechukua za China,mikanda haina tofauti labda mtu kuchagua yenye mauwa na plain.

Najua au nahisi upo wakati utafika sitaweza kufanya baadhi ya vitu kwa sababu ya majukumu au hata kama uwezo utakuwepo utahitaji kufanya mambo mengine nje ya ninayoyafanya sasa so najaribu kuweka vitu bora ili nyumba isidai matengenezo kwa kipindi kifupi.tunatofautiana uwezo wapo ambao kila baada ya miaka miwili huzibadilisha nyumba zao kwa kuweka materials mpya ila wengine hatuwezi hivyo unapokuwepo uwezo tunafanya mara moja tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vinavyotumika physically ndio unatakiwa usi-gamble. Mfano tiles ambazo kila siku zinakanyahwa,vyoo,taps,vifaa vya umeme etc. Ila vitu kama boards kuwa nyembamba hamna athari yoyote kwasababu hazikai pale juu ili mtu akanyage.
Mabati na mbao inabidi kuangalia sana quality kuliko savings.
 
Back
Top Bottom