Safi sana sasa hii mpaka hapo gharama ikoje
Safi sana sasa hii mpaka hapo gharama ikoje
Big up sana mkuu. Umepambana kiume.Mkuu nikupongeze kwa hatua hii uliyofikia,upo hatua 900 mbele ya anaenza leo nikupe moyo kwamba utaimaliza.me yangu ilisimama hivi almost miaka 7,I mean 7 years bila kufanya chochote na mfukoni hela sina kila nayoipata inatosha kwa matumizi ya wakati husika tu ila sikuwahi kukata tamaa,imani yangu ilikuwa ipo siku kama nipo hai nitaimaliza
Namshukuru Mungu,ndoto yangu amenipa uwezo wa kuitekeleza.hii pic ipo Google photos niliipiga mwaka 2017 siku ya jumapili,nikiwa hapa nilikutana na mjumbe wa mtaa akaniambia pagale lako linafuga wezi kama umeshindwa si umuuzie fulani (ni jirani yangu ana hela kidogo za kubadilisha mboga) na alikuwa ameshamnunua jirani yangu wa upande wa kushoto,nilijisikia huzuni sana nakumbuka nilikosa kauli sahihi ya kumjibu nikakaa kimya na hivi lilikuwa limefurika majani nikijiangalia mfukoni hela sina dah,binadamu wanajua sana kukatishana tamaa ila sasa maisha yanaendelea.
Mpaka nafikia hatua ya kuweka bati hizo tofali zilishabadilika rangi zikawa rangi nyeusi tii!kikubwa tusikate tamaa pumzi ikiwepo pambana.View attachment 1503264View attachment 1503265View attachment 1503266
Kabisa mkuu...uko sahihi sanaTrust me unahitaji kiasi kidogo sana kutoka vyumba viwili kwenda vitatu. Utachelewa kidogo tu kumaliza ujenzi ila haitakushinda.
Mkuu kwa nyumba hiyo umetumia kiasi gani mpaka kuimaliza?Kiongozi nilianza chumba kimoja master msingi nikja onganisha msingi wa chumba cha pili master nikaja msingi wa chumba cha tatu master ,kisha nikaja kunyanya vyumba viwili boma nikapiga linta na kuezaka nikaeka milango nikahamia nikaendeleza hicho kingine na kunganisha ukumbi na jiko na store ,ila ilikuwa mwendo wa kobe ,tena nilikuwa mchumi hatari naandika kila nachotumia hapo mpaka nyumba inasimama na nashinda site na mafundi mwanzo mwisho sametime nakuwa kibarua mwenyewe
Mkuu ujenzi pia hutegemea na mhusika, mfano mimi huwa siafiki sana huu ujenzi wa kuunganisha vyumba .Mkuu...
Nadhani hujaipata point yangu,pale juu #1 tumesema “kadiri mtu miaka inavyosogea na majukumu ndiyo yanavyozidi kuongezeka” sasa ndo tuchukulie upo ktk hatua hiyo una watoto unalipa ada,hawajavaa hujawatunza wazazi na ajabu ya ridhiki kipato ulichokuwa ukikipata wakati huo hukipati tena then kichwani lije lakufanya ujenzi mzee utawezana?
Kwa muktadha huo,kama ungeniomba ushauri hapo nyuma kabla hujaanza ujenzi kwenye angle ya kiwanja chako ningekushauri uanze ramani ya nyumba kubwa as long as wewe ni mtafutaji ungepigana tu nyumba ingeisha,kama tayari una familia hujakosea ila wengi wanaojenga huu ujenzi wa “najenga kwanza nyumba ya kawaida kisha nitaja jenga nyumba kubwa huko mbeleni” hizi space zilizobaki kwenye viwanja vyao kama siyo kuja kuziuza basi huishia kujenga vyumba vya uwani vya kupangisha na kuanza kupishana hovyo na wapangaji majumbani mwao na hizo hazikuwa ndoto zao.
Maisha yakikukaba koo utaweza. Hivi unafikiri kuna mtu anapenda kuishi nyumba ambayo haijakamilika??Mkuu ujenzi pia hutegemea na mhusika, mfano mimi huwa siafiki sana huu ujenzi wa kuunganisha vyumba .
Kuishi ktk nyumba isiyokamilika huwa siwezi.
Nina watu wangu wa karibu kama wawili shida sio maisha yaliwakaba ni kwa walifanya mambo kuzidi uwezo wao.Maisha yakikukaba koo utaweza, unafikiri kuna mtu anapenda kuishi nyumba ambayo haijakamilika??
Nami pia utafiti wangu umehitimisha kuwa watanzania wengi hawana uwezo wa kumiliki magari wanalazimisha tu, mtu gari yake ikichubuliwa kidogo tu anakaribia kuzimia kwa presha.
Shida hiyo boss, inasikitisha halafu watu wa hivyo huwa hawashauriki, ndiyo tunakuja kwenye point kuwa kujenga ni mipango, mtu mwenye akili anaanza mdogo mdogo unashangaa umemaliza,
Hio 30m ambayo mtu kaamua kujenga alipewa au aliokota kiasi kwamba akimaliza ujenzi tu anakuwa hana hata uwezo wa kulisha familia?!Huwa nawaza.Mtu
mmoja ana milioni 30 anaamua kujenga nyumba ya kuishi kisha hana uwezo was lishe ya familia na kutatua matatizo yanayomsibu kwa haraka.Mwingine anazo hizo pesa anaamua kufungua duka au mradi wowote ba unamnyookea vizuri lakini anaishi maisha ya kupanga Ila anauwezo
.Kumudu mlo wake vizuri
.Kusomesha mtoto shuke nzuri,kulipa ada za vyuoni za watototo
Kusaidia ndugu zake
.Kumiliki usafiri
.Kutibiwa.
Baadae saana kujenga.
Je ni
yupi anaishi maisha mazuri.Je mafanikio ni kujenga nyumba au kumudu maisha?
Hakika inawezekana Maya Angelou, weka nia kama una eneo anza kuweka material kidogo kidogo utakuja jishangaa umemaliza ujenziAsante kwa kunipa nguvu[emoji1434]
Garama ya chumba kimoja ni wastani wa tofali 400 ongeza na choo na tiles na vifaa vya bafuni na gypsam board na madilisha mawili na blandering pamoja na mabati na rangi ambayo kimsingi itakuwa imetumika vyumba vingine. Hoja yangu ni kuwa garama ya kujenga vyumba vitatu haitofautiani Sana na vyumba vinne. Sana Sana utakuwa umeokoa milio 2.5-3
Hahaha! Wee jamaa umetupa jiwe kwenye kundi la nyuki.Nami pia utafiti wangu umehitimisha kuwa watanzania wengi hawana uwezo wa kumiliki magari wanalazimisha tu, mtu gari yake ikichubuliwa kidogo tu anakaribia kuzimia kwa presha.
Sio lazima.Kwani lazima mtu ujenge nyumba moja!?
Ni hatari, lakini wengi wao hawapendi kuishi hivyo.Wewe na wanaoishi na familia chumba kimoja Cha kupanga watu 5 baba, mama, na watoto 3.
Nimemjengea mama kwanza ya vyumba4. Nina mpango wa kujenga ya vyumba5. Punguza hasira, maisha ni nyumba.Yako ina vyumba vingapi?
Viwanja vya bei nafuu viko mbali na miji, vijana wengi wanashindwa kujenga kutokana na hili. Upate kiwanja Mambwepande na kazi unafanya Posta. Ukimaliza ujenzi gharama ya kwenda kazini kila siku ni Kheri kupanga nyumba Sinza.