Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Ni kweli kabisa. Mimi binafsi nimegundua kujenga vyumba viwili haina tofauti sana na vyumba vitatu. Yaani ongezeko la chumba kimoja ni dogo kifedha ila ni kubwa sana kwenye thamani na matumizi ya nyumba yako.
 
Kujenga ni kazi ngumu kweli.. Wenzetu wazungu hawajengi.. Nyumba wananunua kwa mkopo kwa kulipia kidogo kidogo huku unaishi ndani.. So pesa ya kulipa rent ndio inalipa mkopo.
Asilimia kubwa ya Wabongo wanajenga kwa kudunduliza ni kama unajenga kwa mkopo bila riba.
Kama unachukua mkopo wa nyumba 50m unalipa 1m kila mwezi(mfano) si Sawa na mtu anaenda site kila mwezi na 1m au kila wiki na 250,000 anasogeza tofali kadhaa?!
Tena wa mkopo utakuta ulikopa 40m unarudisha 50m hivyo realistically nyumba yako itakuwa ya 30 au 40m.
 
Heri moja kenda kuliko kumi nenda rudi, unajenga nyumba ya vyumba2, baada ya kuhamia unakaa miaka3 familia inakuwa kubwa. Mwisho unawaza kujenga nyumba nyingine kubwa.

Mkuu raha ya nyumba ujiachie. Sio unakuwa kwako utadhani upo geto, kajumba kadogooo.
 
Hivi kujenga mwisho ni nyumba moja?
 
Yamenikuta hayahaya Diana mie..[emoji25][emoji25]

Kutaka floor moja ya vyumba viwili limekuwa gofu sasa mweh[emoji26]
 
Nakumbuka wakati wa Jk awamu ya kwanza kuna boss wangu mmoja aliwahi kunishauri nisikimbilie magali niwekeze kwenye ardhi kweli nikaenda nikanunua bagamoyo kama 1 heka kwa 400k wakati huo nikaweka banda baadae nikanunua tena mitaa ya boko kwa 1.5m wakati huo nalipwa 3k per month ila akwambie mtu lazima ujibane ndio ujenge pale boko nilianza kujenga vyumba 2 kwa mbinde lengo nikae ila mazingira hayakunivutia sana sababu ya uswahili flan flan nikapapangisha pesa ya kodi nikianza kuongeza chumba kimoja kimoja awamu ya pili ya JK nikapata kazi sehemu hivyo salary ikapanda mpk 700k nikamalizia Nyumba boko nikapata sehemu nyingine mbezi juu nikaanza kujenga kidogo kidogo kwa nyumba ya nyuma chumba na sebule pale nilipokuwa nafanyia kazi kuna wadau niliwashauri tununue sehemu ila walinicheka kwamba kwanza mbali na ofisi halafu hiyo pesa natumia kujenga niweke kwenye biashara na biashara ingenilipa kuningenunua nyumba wengi wao walikimbilia kununua magali na kufungua biashara za nguo, salooni na nk ambazo sasa hivi zimekufa na kampuni yenyewe inaendea kufa mie sasa hivi nimeshamalizia nyumba kubwa Kule bagamoyo nimeweka mifugo kama kuku,kitz, ng'ombe wa maziwa,na Kule kazi nilishaacha sasa hivi nipo busy tu na mifugo na kilimo moro na kusoma kujiendeleza kuajiriwa sitaki hata kusikia, watu wengi wanafeli kwenye ujenzi kutokana na kutishwa, kuwa na matarajio makubwa kuliko kipato,starehe za muda mfupi bila kuwa na malengo ya muda mfupi, kusubiria apate pesa nyingi bila kujua zitatoka wapi kwa uzoefu wangu sijawahi kwenda site zaidi ya 3m nilichokuwa nafanya nikipata pesa nawekeza vifaa dukani mpk natimiza lengo na kingine ukipata nyumba 1 ni rahisi kidogo ya kupata ya 2
 
Jumla imekugharimu kiasi gani mpaka hapo ulipofikia?
 
Ni kweli kabisa unajenga vyumba vichache halafu unahamia utakuwa unamalizia kidogokidogo
 
Nami pia utafiti wangu umehitimisha kuwa watanzania wengi hawana uwezo wa kumiliki magari wanalazimisha tu, mtu gari yake ikichubuliwa kidogo tu anakaribia kuzimia kwa presha.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] haaaahaaaaaa


Kuna kitu nimekumbuka nimecheka sana dah[emoji1787][emoji1787][emoji16]
 
Ni kweli lakini inategemea kwa mfano kuna nyumba unaweza kuijenga na kwenyw finishing ikawa haikutesi sana.

Kuna nyumba nyingine ukishafika lenta ukiwa na 3M unamalizia ila nyingine inahitaji 30M hawa watu hawawezi kuwa sawa
Hii imenitokea kabisa...kupandisha boma nilienda vizuri...finishing hatariii..mtu unaishia kuishi kwenye gofu quality ya life inashuka kabisa..kweli kujenga ni mchakato
 
1.8 na nimehamia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…