Ujenzi rahisi kwa kutumia interlock blocks, jenga popote, jenga sasa

Yaani 50kgs za Cement unachanganya na udongo wenye uzito gani?
Nyie ni kampuni bila shaka mnafanya kazi kwa vipimo.
Hatupimi kwa kilo,na kama nilivyoelezea,ratio inategea na aina ya udongo uliyopo kwenye eneo lako,kuna jinsi ya kupima udongo ili kujua mchanganyiko wake,ukishajua ndio utajua mfuko mmoja upige tofali ngapi.
 
Mku nyumba room sita kwa udhoefu wako inaweza kutumia tofali ngapi?
Asante
 
Je jins zinavyoshikan hakuna haja ya kuweka nguzo kwa ajili ya kuzisaidia hizo tofali??
 
Mfuko unatoa kwanzia 80 mpaka 100 kulingana na udongo wa eneo lako
Kwa hiyo hata mchangwa wa dar unaweza kujengea hiz tofali?? Na je kwa kupangana huko ikitokea tetemeko la ardhi haziwez kuleta balaa?? Au huwa zinawekewa nguzo??
 
Je jins zinavyoshikan hakuna haja ya kuweka nguzo kwa ajili ya kuzisaidia hizo tofali??
Hazihitaji sababu zinajilock zenyewe hivyo zinashikana kwa balance moja nyumba nzima, zinakuwa na nguvu ya uvutano moja.
 
Mkuu, una uhakika kabisa ujenzi wa kutumia tofali hizo una save hadi 40%?, maana mimi nilikuwa mmoja wa wasimamizi wa nyumba za NHC miaka ya 2015-2017, ambapo tulisimamia miradi yote ya NHC Tanzania, ikiwemo na ule wa Mikwambe+Mwongozo
 
Kwa hiyo hata mchangwa wa dar unaweza kujengea hiz tofali?? Na je kwa kupangana huko ikitokea tetemeko la ardhi haziwez kuleta balaa?? Au huwa zinawekewa nguzo??
Hakuna madhara kaka,hatutumii mchanga,ni udongo tu,wenye ufinyanzi kwanzia 7% mpaka 40%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…