Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Hayo mafuta moja Sio yetu pili wanaingia gharama za kuchimba na kiwanda sisi kote huko hatupo

Deal liko fair
 
Mahesabu ya kibiashara huwa yananiwacha pembeni, Fikiria kampuni ya Twiga kwenye madini. Tanzania ina hisa 16% lakini faida tunagawana 50/50 na wenye hisa 84%😃😃
Madini ya kwetu yako ardhi yetu mafuta Sio yetu Ni ya waganda deal liko fair Sana tu
 
Hayo mafuta moja Sio yetu pili wanaingia gharama za kuchimba na kiwanda sisi kote huko hatupo

Deal liko fair
Unajua gharama za matunzo ya hilo bomba na umeme wa kuchemshia hayo mafuta? Kwanini a give up hiyo 20 percent
 
Mimi nimeelewa tofauti na wengi mnavyotafsiri. Nichoelewa ni kuwa umiliki wa hiyo miundo mbinu ya kusafarisha mafuta Tanzania itamilki 60% na Uganda 40%. Maana yake ni hii; kama mradi unagharamiwa kwa mkopo, Tanzania tutawajibika kulipa 60% na Uganda watalipa 40%.

Miundo mbinu kama "entity" utakuwa na mapato na matumizi; kama mapato yakizidi matumizi Tanzania na Uganda kama wabia watagawana kwa uwiano wa 3:2
 
Madini ya kwetu yako ardhi yetu mafuta Sio yetu Ni ya waganda deal liko fair Sana tu
Kwa hiyo hayo mafuta yanachimbwa kwenye ardhi Tanzania? Leo mnakubali kuwa hiyo inawezekana na Mnafuta zile kelele za 50/50 haiwezekani John ni muongo? Mgao wa mapato ktk Biashara na uwekezaji haiendeshwi kwa amri za Bunge bali kwa makubaliano ya kimkataba.
 
Rais Museveni ametembelea tanzania Kikazi

Rais Magufuli: Km 330 za bomba hili zipo Uganda. Kwa Tanzania, bomba litapita kwenye mikoa 8, wilaya 24 na kata 132. Tathmini kwa Tanzania, watu zaidi ya 90,000 watalipwa fidia; ni takribani bilioni 21

21Bil gawa kwa watu 90,000 ni 233,333/=
Fidia gani hii?
 
Huu mradi wa bomba unazinduliwa kila baada ya miezi mitatu kiasi kwamba tumechoka kuusikia. Kwani lazima uzinduliwe kila mara? Kuna shida gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…