Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Walikua wanaajiliwa 60000 na wanaostaafu wangapi?
 
Hao wanaomtembelea kikazi mbona huwa awaendi kumtembelea akiwa Ikulu dar?? Chattle Kuna nini chaziada ambacho kinawafanya waende kwake chattle na sio ofisi zake magogoni?? Kikwete au mkapa mbona hatukuwaona Hawa kina mseveni wakiwatembelea huko msoga au masasi?? Upuuzi mtupu na mikakati ya kikatili dhidi ya upinzani TU.
 
Museveni kasoma chuo kikuu mlimani nadhani unalijua hilo.

Hawezi kuja kumuombea kura Tundu Lissu asiyemheshimu Hayati Nyerere.

Kasoma mlimani so what? Kwanza alichokifanya Museveni ni kosa kidiplomasia. Hairuhusiwi mtu kutoka nje ya nchi kuja kuingilia siasa za ndani ya nchi nyingine. Nilijua lazima utatepeta tu kwenye hii hoja. Na sio ww peke yako ni wanaccm wote mmeshapanick. Kwasasa wapinzani waanze kutegemea ushindani wa kikatili, maana tayari ccm imekata pumzi mpaka wanamuita rais wa nchi nyingine kuja kuwaombea kura.
 
Halafu kwa leo hakukuwa na muwakilishi hata mmoja wa Total

Total hawawezi kuja maana wanajua hizo ni kampeni za kitapeli. Hiyo inaonesha kuwa ccm wako kwenye panicking mode. Tutegemee kuanzia sasa siasa za kimafia kuchukua hatamu, maana tayari ccm wameshakata pumzi. Huwa wanasema eti ccm inafanya mikutano sehemu nyingi, na mimi huwa nawaambia wana mikutano mingi lakini yenye hoja duni za kiushawishi.
 
Mzeee wetu anazungumia ajira kuwa mradi utaajiri watu 13,000 anasahau kuwa kikwete kila Mwaka Alikuwa anaajiri watu 60,000 Kwa Mwaka yeye kazuia Halafu anapigia upatu ajira Ya mafuta ya Uganda
Jaribu kuwa msomaji, mzuri mradi umepewa baraka za kuanza rasmi. Tanzania tulishamaliza yote tuliotakiwa kuyafanya upande wetu, kazi ilibaki Uganda wanabishana juu ya kodi. Waganda wameshakubaliana, leo Museveni amekuja kuleta taarifa rasmi kwamba mradi uanze.

Hao watu 60,000 wa Kikwete kila mwaka wengine ndio wale watumishi hewa na wenye vyeti feki, kama Kikwete aliajiri 60,000 kwa miaka kumi yake aliingiza watu 600,000!! Huu ni uongo.
 
Kwa iyo Safari yote hiyo kumbe dhumuni ni kumuombea kura??? Kweli Ccm mna hali mbaya sana! Kawaletea na hela za kuhonga nini??? Maana haiwezekani mradi huo huo kila siku mnazindua tu!!
 
Nimejiuliza wanajenga kwa pesa ya serikali zao 100 perce ?
Isijekuwa Jiwe ameshaingia mfukoni maana hachelewi. Nimemsikia Mu7akisma hiyo bilioni 14 ni kurumure...Yani wanaanza kulima shamba so wanaingia mfukoni. Kama ulimsikiliza vizuri hadi yule mhaya akatafsiri maana ya kirumure
Na bilioni 14 siyo Shs. Ni madolari
 

Nakubaliana na hii hoja.hii ni campaign tu hakuna kingine.
 
Kwa iyo Safari yote hiyo kumbe dhumuni ni kumuombea kura??? Kweli Ccm mna hali mbaya sana! Kawaletea na hela za kuhonga nini??? Maana haiwezekani mradi huo huo kila siku mnazindua tu!!
Tatizo lako we ndugu yangu huwa unapenda sana kuropoka .
 

Huwa nikisikia hizi njozi za kitapeli za hawa viongozi nacheka mpaka basi. Hivi Magufuli anasema wamekaa na Museveni ndani ya dakika 5 tu wakakubaliana Tanzania ipate 60% kisha uganda wabakie na 40%, wakati huohuo Total ambao wanatoa $3.5b gawio lao halionyeshi ni kiasi gani! Wakati hayo mahoka ya kuiombea ccm kura yakiendelea, hao viongozi hawajui kuwa tunajua kuna makubaliano ya kuwa na sarafu ya pamoja ya EA, na hadi leo haijafanikiwa. Naomba Mungu asinichukue mapema ili niendelee kuona hizi futuhi.
 
Wataalam, mimi sijaelewa hapo jamaa anaposema na sisi Tanzania tutalitumia hilo hilo bomba kupeleka gesi huko Uganda. Sasa gesi, hata kama ni liquefied natural gas (LNG) na mafuta yatakuwa yanapishanaje kwenye hilo bomba? Yaani gesi inakwenda Uganda na mafuta yanakwenda Tanga! Au watapeana zamu?
Msinicheke, haya mavitu sina utaalamu nayo.
 
Nadhani kaja kutusaidia kampeni kiaina. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji848][emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…