Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Naomba kuuliza wamesaini ili ujenzi uanze mwezi gani au mwaka gani maana bado sijaona ni mwezi gani au mwaka gani ujenzi uanze mwenye kujua anisaidie
Hiyo ilikuwa kiki ya kupoozea joto la uchaguzi..subiri kabla uchaguzi haujaisha watakuja kufanya uzinduzi mwingine wa kuanza kuleta matrekta site.
 
Unazinduliwaga Kila siku tokea 2006
Unashangaa nini? Ujenzi wa SGR ulizinduliwa, lakini kila wanapotoboa mlima, wanazindua utoboaji mlima, wakifika kwenye daraja wanazindua tena, wakifika kwenye stand wanazindua tena!! Upuuzi mkubwa, watu wanafanywa wajinga!!

Wewe hujaona barabara zilizojengwa wakati wa Kikwete, zimetumika mpaka zimeanza kuchakaa, zinazinduliwa tena? Hujaona viwanda vilivyoanza uzalishaji miaka ya mwanzoni mwa 2000 vikifunguliwa tena? Ndipo tulipofikia. Siasa za uwongo uwongo na hadaa nyingi. Lakini mdomoni, kila siku eti "msema kweli ni mpenzi wa Mungu", sijui ni mungu gani anayedhihakiwa kiasi hiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiki tu hizi wakati wa uchaguzi.
Mnagawana 60/40 % ya kitu gani ? Tuanze hapo.
Mafuta sio yetu biashara hapa ni unapitisha mafuta yako Tanzania charges zetu ni $/barell of oil sasa hio 60/40 inatoka wapi ?
Au ndo tunawapa uganda kwa kutupa tenda ?
Kuna mashaka na mapato kuwa madogo sana
Then bomba hilo kutumika kupitisha mafuta ya tanzania yakivumbuliwa ! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Uganda wao wana manasafirisha halafu wewe upeleke uganda !
Crude oio Tanzania inaweza kupatikana deep sea ya Mtwara na Zanzibar sasa uchimbe mafuta baharini then uyapeleke kwenye hili bomba unayapeleka wapi ? Mbona mambo ya ajabu sana haya.
Gas yetu ipo Mtwara kusini ya Tanzania unasema utatumia bomba hilo au jengine alongside kuwapelekea uganda gas. Well ni mkakati mzuri ila njia hio ni costly kwa itabidi ujenge pipeline ingine kutoka Mtwara hadi Tanga.
Ninavo jua hapa Dar tu hatuna gas ya Mtwara ni porojo tu kila siku.
Kama gas iko ya kusafirisha option nzuri ni kutumia SGR unayo jenga LPG tanks itafika uganda muda mfupi kwa gharama ndogo.
Anyway mkataba wa pipeline tushaweka mara 2 na hii ya Tatu na tatizo la kuchelewa sio corona bali ni fedha na mikataba yao uganda na Total.
Hatuwezi kufanya lolote kama uganda hawapo ready tutabaki kuweka tu sign
 
bomba ilikuwa zuga walitaka tu kujadiliana namna ya kukabiliana na Robert Amsterdam.
 
Chadema imejaza vijana vilaza pamoja na mgombea wao,eti chagueni mbunge atakayepiga kelele bungeni,Nani aliwaambieni kuwa bungeni ni mahali pa kupiga kelele?

Kilichofanyika Leo ni kusaini mikataba kwa ajili ya kuanza kwa utekelezaji that is ujenzi
 
Nakumbuka huu mradi ulizinduliwa 2016 Kwa mbwembwe sana na mikataba ikasainiwa hadharani na tukajulishwa kuwa mradi utakamilika mwezi wa nne Mwaka 2019 nashangaaa tena leo eti unazinduliwa na katika uzinduzi huo nimesikia maneno kuwa tunataka mazungumzo yafanyike mapema ili michakato ianze haraka, sijaelewa?

Au ni Lissu ndio anafanya watu warudie hadi mikataba? Huyu Lissu huyu atasababisha hadi ule mradi wa Umeme usainiwe upya haki Ya MUNGU, sijawahi ona kitu kama hiki na hii inaitwaje wakuu?

Mzeee wetu anazungumia ajira kuwa mradi utaajiri watu 13,000 anasahau kuwa Kikwete kila Mwaka Alikuwa anaajiri watu 60,000 kwa mwaka, yeye kazuia halafu anapigia upatu ajira Ya mafuta ya Uganda.
Wewe ni Mpuuziiiiiiiii ajira 60,000 kwa mwaka na miaka kumi 600,000! Hebu ongea na boyfriend wako kidogo akupunguze nyege la sivyo utaharibikiwa.

Angalia ziara ilianzia hapa

 
Nashukuru kwa hii taarifa kwaio watu tulikua mis informed..kwaio COCO itaendelea kuwepo? Au DODO? Au vyote kwa pamoja maana pascal mayalla yeye ni mkereketwa wa TOTAL na alifafanua vizuri
Mkuu, vyote vitaendelea kuwepo ! Na kwa kweli uwekezaji wa Total hapa Tanzania utaendelea kwa kiwango kikubwa sana. TOTAL ni number one in Africa and now number one in Tanzania. Kampuni hii ya Kifaransa ina interest sana Africa, Agip waliondoka miaka mingi, Esso na Caltex kadhalika, BP vile vile lakini Total hata ukisoma web site yake ina wekeza zaidi Africa.
 
Hahaha Promo ya Magufuli imebuma hiyo. Bomba halipo ni uongo wa kisukuma tu huo.
Kisukuma na Kiganda hakuna Mradi wa Bomba la Mafuta wala la Gesi ni jaribio la mwisho la kampeni za mgombea wa CCM baada ya kuishiwa pumzi na kushindwa kupiga push-up kuonyesha bado ana nguvu. Uganda kuna Uchaguzi pia wataendelea kusaini mikataba ujao utakuwa Uganda Bomba likibaki ndoto.
 
Jaribu kuwa msomaji, mzuri mradi umepewa baraka za kuanza rasmi. Tanzania tulishamaliza yote tuliotakiwa kuyafanya upande wetu, kazi ilibaki Uganda wanabishana juu ya kodi. Waganda wameshakubaliana, leo Museveni amekuja kuleta taarifa rasmi kwamba mradi uanze.

Hao watu 60,000 wa Kikwete kila mwaka wengine ndio wale watumishi hewa na wenye vyeti feki, kama Kikwete aliajiri 60,000 kwa miaka kumi yake aliingiza watu 600,000!! Huu ni uongo.
Huyu aliyeahidi ajira milioni nane atakua anaajiri wangap kwa mwaka ikiwa kikwete kwa 10yrs aliajiri watu laki6.......
 
Chadema mambo madogo kama haya mnashindwa kuyaelewa sasa ndio mtaweza saini mikataba mikubwa mikubwa kwa maslahi ya nchi??
 
Nakumbuka huu mradi ulizinduliwa 2016 Kwa mbwembwe sana na mikataba ikasainiwa hadharani na tukajulishwa kuwa mradi utakamilika mwezi wa nne Mwaka 2019 nashangaaa tena leo eti unazinduliwa na katika uzinduzi huo nimesikia maneno kuwa tunataka mazungumzo yafanyike mapema ili michakato ianze haraka, sijaelewa?

Au ni Lissu ndio anafanya watu warudie hadi mikataba? Huyu Lissu huyu atasababisha hadi ule mradi wa Umeme usainiwe upya haki Ya MUNGU, sijawahi ona kitu kama hiki na hii inaitwaje wakuu?

Mzeee wetu anazungumia ajira kuwa mradi utaajiri watu 13,000 anasahau kuwa Kikwete kila Mwaka Alikuwa anaajiri watu 60,000 kwa mwaka, yeye kazuia halafu anapigia upatu ajira Ya mafuta ya Uganda.

Hilo bomba sasa linakuwa nyenzo muhimu ya kutafutia kura katika mikoa lilikopita, wataambiwa habari ya ajira kedekede mpaka na mafuta yanayosafirishwa mengine watagawiwa wanainchi wenye magari bure na hata wasiokuwa na magari wanaweza kuyanywa endapo wataweza
 
Hahaha kesho Tundu Lisu akiuchanachana huo mradi wataukimbia.
Sasa Lisu ataachaje kuuchanachana wakati yeye anategemea kula kwa vile vibeberu vyake ?

Alafu wafuasi wake mnashangilia kama mazuzu?
. Uzuri hatapata zaidi ya 20% ya kura so hana madhara
 
Lisu ni debe tupu

Mhh ! ,hebu tuambie hapa mlikuwa mnafanya nini kama kweli yanayo semwa na Serikali kuhusu Safari ya Museveni !??Kubalini pumzi imekata mmemaua kuleta Maigizo .
IMG-20200914-WA0000.jpg
 
Bomba ka TAZAMA lipo miaka na miaka Lina peleka mafuta Zambia kuna nini mmeona toka hilo Bomba??? Hilo Bomba la Uganda ni wizi mtupu na udanganyifu kwa maskini wa fikra wa Tanzania. Wananchi amkeni hizo ni siasa uchwara. CCM tuweke hali za wananchi mbele sio huu ujinga wa bomba la mzungu. Nigeria kuna mabomba mangapi. Acheni ujinga
Kwamba hilo bomba la TAZAMA halina faida yeyote kwa nchi?

Hivi wafuasi wa Lissu akili zenu mmepeleka wapi? Yani unataka wakuletee kiburungutu cha pesa hapo nyumbani kwako na wakwambie hii ndio faida ya bomba la TAZAMA?

Aisee
 
Back
Top Bottom