nyakubonga
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 5,960
- 9,978
Haswaa.Labda mafisadi ila sisi wana Kanda ya Ziwa tulishaamua, whether you like or not, we have already decided!! JPM Bridge.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haswaa.Labda mafisadi ila sisi wana Kanda ya Ziwa tulishaamua, whether you like or not, we have already decided!! JPM Bridge.
Kwanini wewe hukuitwa jina la ukoo wa jirani yako ukaitwa jina la baba yako aliekulea na kukusomesha?Hivi hili daraja kwann lisiitwe busisi bridge!?kwann tumekuwa wajinga hivi!?kiongozi atakuja na atapita( kufa); Kila kitu ni jina la kiongozi why!?? Kwann Nyerere hakufanya hivyo!?
Hayo madude meupe pembeni ni ya nini?View attachment 2597810
Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila
Viongozi mbalimbali wametembelea mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigongo Busisi ambalo pia linajulikana kama Daraja la JP Magufuli, leo Jumapili Aprili 23, 2023.
Daraja hilo linapatikana Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, bado lipo kwenye hatua ya ujenzi. Hivi ndivyo viongozi walivyozungumza baada ya kufika eneo la tukio.
View attachment 2597807
View attachment 2597261
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima:
Katika Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuna vitu viwili vinavyoweza kuwa katika vivutio, navyo ni Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Daraja la JP Magufuli (Daraja la Kigongo - Busisi).
Ukishuka Mwanza ukaja Busisi na kutumia saa zaidi ya tatu kuvuka ni rahisi kuahirisha kufanya utalii, lakini uwepo wa daraja hili utasaidia kurahisisha mawasiliano na hata utalii utaongezeka.
Kamati ya Ulinzi na Usalama tulikuwa tunafuatilia, kulikuwa na udokozi wakati ujenzi ukiendelea, mtu anaona anawaibia Wachina kumbe anawaibia Watanzania wenzake.
View attachment 2597808
Michezo hiyo ilikuwa inafanywa, tumefinya na tumeshatuma salamu kwa kuwa vifaa vilikuwa vinaibiwa na kupelekwa Usagara, Sengerema au Buhongwa.
Tukimkuta mtu ambaye ana vifaa vinavyotokana na mradi tutafunga duka na hatafanya tena biashara Mwanza na tutamfungulia kesi ya uhujumu uchumi kisha atatueleza anaoshirikiana nao.
View attachment 2597262
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja:
Nampongeza Rais Dkt. Samia anavyoendelea kufungua fursa mbalimbali ikiwemo daraja hilo, ukanda huu wa Ziwa Victoria tunatamani utalii uzidi kukua.
Utalii wa Ukanda wa Kaskazini ni kama umejaa kwa kuwa watalii wengi wanaenda huko, lakini tuna vivutio vingi Ukanda huu wa Ziwa pia, hivyo lengo la mradi hii kama ya daraja ni kufungua uwekezaji na kutengeneza mazingira ya utalii.
Tunataka watalii wanapokuja Nchini wazunguke huku na huku badala ya kuegemea upande mmoja.
Ukanda wa Ziwa tuna vivutio vingi kama ilivyo Ukanda wa Kaskazini, miundombinu ikikamilika kama barabara na daraja kutakuwa na ongezeko la Watalii na haya uchumi utakua kwa kuwa kutakuwa na mzunguko wa fedha.
Sekta ya Utalii inachangia pato kubwa Serikalini takribani 18% hadi 21%, kuna ajira na uwekezaji, pia watu wanaburudika.
View attachment 2597263
View attachment 2597811
Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila:
Daraja hili lina umuhimu kwa Watu wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla, mfano kufika Mwanza kwenda Geita au Sengerema ilikuwa ni lazima uzunguke hadi Kahama, hivyo Daraja la Busisi litarahisisha mzunguko wote huo.
Daraja hili litaunganisha watu wa Mwanza, Geita, Kagera na Nchi jirani ya Uganda, kwa huo ukaribu utatumia muda mfupi kwenda nchi nyingine zinazotuzunguka kama Rwanda.
Watu walikuwa wanatumia vivuko na mitumbwi na wanachukua zaidi ya saa mbili hadi nne huku kukiwa na msongamano, lakini daraja hili litawahisisha na kupunguza muda, wanaweza kutumia dakika tano kuvuka.
Daraja hili lilianza kujengwa Mwaka 2020 baada ya mkataba kusainiwa Mwaka 2019 na hatua ya ujenzi imefikia 72%.
Makubaliano ya mkataba ni kuwa linatakiwa kukamilika Februari 25, 2024 kulingana na makubaliano yaliyopo, kuhusu kasi ya Mkandarasi tunaridhishwa nayo.
TANROADS tunasimama kwa niaba ya Serikali katika mradi huu na sisi ndio tunaosaini mikataba na kusimamia mchakato wote ili kuhakikisha ubora unafikiwa kama ulivyopangwa.
View attachment 2597812
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya:
Tumefanya kazi kubwa katika Mkoa wa Mwanza kwenye Wilaya ya Sengerema na Misungwi, ambapo tumesaini mkatana wa ujenzi wa Kivuko cha Buyagu-Mbarika ambacho hakikuwepo kabisa Ziwa Victoria.
Hayo ni maeneo yanayotazamana lakini hakukuwa na kivuko, lakini kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu kukaonekana kuna umuhimu huo.
Baada ya kusikia kilio cha wananchi Rais Dtk. Samia akatoa maelekezo ya ujenzi wa kivuko kitakachokuwa na uwezo wakubeba wananchi 100 na tani 50 na kitajengwa na mkandarasi mzawa Songoro Marine.
Aidha, tumefanya ziara ya kushtukiza kuja kutazama maendeleo ya Daraja la Busisi lenye urefu wa Kilometa 3 ambalo linapita kwenye maji.
Hili ni moja ya madaraja marefu Afrika, taarifa ya Wakandarasi na msimamizi ni kuwa mradi utakamilika Februari 2024, fedha inayotumika ni ya Tanzania na bahati nzuri hakuna deni ambalo mkandarasi anaidai Serikali.
Likikamilika linatarajiwa kugharimu Tsh. Bilioni 716, faida ya uwepo wa daraja hili ni kama lango la kuingilia Mwanza.
Daraja limezingatia viwango vya juu, linaweza kuwa imara kwa zaidi ya miaka 100.
View attachment 2597813
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima
View attachment 2597814
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja
Meneja wa TANROADS Mwanza, Mhandisi Pascal Ambrose:
Mbali na araja la Busisi pia kuna mradi mingine kadhaa, mfano kuna barabara yenye takribani Kilometa 150 kutoka Mwananga hadi Kahama.
Usanifu umeshakamilika kuanzia Mwaka 2017, Serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Pia kuna usanifu tumeufanya wa barabara kutoka Mwanza hadi Nyanguge kuelekea mpakani na Simiyu.
Ili kupunguza msongamano kipande cha Mwanza hadi Nyanguge usanifu umefanyika wa njia nne.
View attachment 2597265
View attachment 2597877
View attachment 2597878
KivipHili daraja llimeisababishia nchi matatizo haswa
Kwann isiwe Busisi bridge!?Watu hawataki liitwe Magufuri Bridge.
Kaamua mamaako au Basha wako!!Tuliza mshono wewe bibi!! Mambo mengine hayakuhusu hilo daraja litaitwa JPM tumeshaamua!! Full stop!!
Maeng watakuja kutuambia nisije kukupiga kamba bureHayo madude meupe pembeni ni ya nini?
View attachment 2598697View attachment 2598698
Extrovert FRANCIS DA DON raraa reree
Mimi nikiwa mjinga aliyekuzaa atakuwaje!?Kwanini wewe hukuitwa jina la ukoo wa jirani yako ukaitwa jina la baba yako aliekulea na kukusomesha?
Katika huo ujinga wenu mm simo. Wajinga ni nyinyi
Huo ukanda huwa kuna magugu maji mengi sana,kuna wakati hadi yalikuwa yanasababisha hadi ferry zinasimama kwa muda ili wayaondoeNaona Magugu maji yameanza kuongezeka tena ziwa Victoria. Hii inaashiria uwepo wa uchavuzi wa mazingira kwa kujisaidia hovyo vichakani na ziwani. Maafisa Afya fanyeni kazi yenu ipasavyo, kagueni vyoo na utupaji wa takataka maeneo hayo......
Hayo madude meupe ndio ‘Concrete footing’ ya daraja lenyewe, hicho kidaraja cha chuma pembeni ni cha muda tu (temporary) kwa ajili ya kuvusha materials, equipment na mafundiHayo madude meupe pembeni ni ya nini?
View attachment 2598697View attachment 2598698
Extrovert FRANCIS DA DON raraa reree
Asante mkuu kwa maelezo mazuri sikufaham kabisa. Lakini mbona wanasema asilimia 72 tayari. Lakini navyoona ni asilimia 30.Hayo madude meupe ndio ‘Concrete footing’ ya daraja lenyewe, hicho kidaraja cha chuma pembeni ni cha muda tu (temporary) kwa ajili ya kuvusha materials, equipment na mafundi
Hiyo inafumuliwa, itaenda kutumika kwingine. Kuhusu asilimia 72 inawezekana, maana hapo inawezekana wanafaya precast ya super structure kiwandani, beams zikija zinatandikwa tu...Asante mkuu kwa maelezo mazuri sikufaham kabisa. Lakini mbona wanasema asilimia 72 tayari. Lakini navyoona ni asilimia 30.
Kwa hiyo wakimaliza wata dismantle iyo barabara ama itabaki kwa waenda kwa miguu?
Wote wawili mama yako na basha wako!Kaamua mamaako au Basha wako!!
Hizo ni Expansion joints mkuu 🤣🤣🤣Hayo madude meupe pembeni ni ya nini?
View attachment 2598697View attachment 2598698
Extrovert FRANCIS DA DON raraa reree
Unateseka ukiwa wapi?Kwani Magufuli alitoa pesa zake mfukoni. Tusipoteze asili ya maeneo liitwe Busisi
Kanywe sumu ufe.Hiyo kazi ya kuunganisha pori na pori kwa daraja imekula billioni 700 inaiuma kweli!
Kuliko matatizo yako na familia yako?Hili daraja llimeisababishia nchi matatizo haswa