Ujenzi wa Ghorofa Moja

Ujenzi wa Ghorofa Moja

idorome

Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
28
Reaction score
7
Naangalia option kujaribu kujenga kighorofa kimoja japo nilale juu, fundi ameniambia nichague kati ya option mbili
  1. kulaza matofali
  2. kutumia nguzo
Namaanisha kama nikilaza matofali floor slab ya juu itakua supported na hayo matofali bila nguzo. Kama nikiopt nguzo nitasimamisha matofali kawaida, niko tutani naombeni ushauri wataalamu ujenzi nitaanza soon ndio nafanya site clearance na kukusanya vifaa. Niko jijini
 
nijuavyo mimi kasheshe ya ghorofa ni kujenga foundation, hizo nguzo sidhani kama ni ghali kiasi cha kufanya ufikirie kujenga nguzo za matofali (kulaza matofali).

anyway ngoja nikae pembeni na mimi nijifunze zaidi
 
Technicaly kwa knowledge niliyonayo, option ya kuweka nguzo(columns) is the best kuliko ya kulaza tofali. Kwani kwa kusimamisha nguzo jengo linakuwa stable kistructure kuliko ukilaza tofali.

So ningekushauri uchague option ya nguzo.
 
Nakuunga mkono mkuu, faida nyingine ya nguzo unaweza badili design ya ndani(vyumba) wakati wowote upendavyo, ambapo kwenye tofali kulaza ni mgumu sio rahisi,
 
Mkuu mi sio eng ni architect...ninachoshangaa umeongea na fundi kabla hujaongea na architect.....ninachojua mimi architect ndiye mtu muhimu kumpa hayo mawazo ili anapodesign afikilie hilo....sasa ukiongea na fundi afu mchoro ukawa haujazingatia hizo option zako inakuwa...kwa msaa wa bure piga 0656509838 nitakushauri kuhusu ujenzi ukipenda tunaweza kufanya kazi yako pia
 
Unazungumzia kulaza matofali tu bila nguzo kwa sababu nchi hii Mungu ametujalia, hakuna matetemeko kivile! kwa wenzetu wenye matetemeko hata nguzo hazisaidii badala yake wanatumia steel poles kwenye nguzo na gypsum tu.
 
Mkuu mi sio eng ni architect...ninachoshangaa umeongea na fundi kabla hujaongea na architect.....ninachojua mimi architect ndiye mtu muhimu kumpa hayo mawazo ili anapodesign afikilie hilo....sasa ukiongea na fundi afu mchoro ukawa haujazingatia hizo option zako inakuwa...kwa msaa wa bure piga 0656509838 nitakushauri kuhusu ujenzi ukipenda tunaweza kufanya kazi yako pia
Watu wengine bana,
Mtoa Mada anajua pia kuna Engineer na Architect but ameleta hapa labda na kwa faida ya wengine, wewe unatoa namba ili mpelekane chemba, sio poa mkuu.

Wewe kama una ushauri mwaga hapa nasi wengine tufaidike!
 
Nina experience na option ya kulaza matofali.
I have no complain about it. Ila kuna vitu inabidi uvifahamu:
1. Hutaweza kubadilisha plan ya nyumba baadae kwa sababu kuta ndizo zilizobeba jengo. Kama huna mpango wa kubadili matumizi ya jengo that factor may be immaterial.
2. Hata unapolaza matofali ni LAZIMA utahitaji nguzo kadhaa, kwahiyo matumizi ya nguzo hayahepukiki kwa asilimia 100.

Advantage kubwa ya kulaza matofali ni kwamba starting costs zinakuwa sio kubwa. Nguzo za kubeba jengo gharama yake parefu. So kwa anayeamua kujenga hatua kwa hatua inaweza kuwa kipingamizi.
 
Uko sahihi mkuu sema mi sikai sana jf.....siko so active ndo maana nilifanya kumshauri kwa njia hiyo.
Pili inaonesha we ni finalizer sana sikunyingine shirikisha kwanza akiri sio wote waganga njaa kama unavyohisi......ni professional yangu na pia ninakazi yangu kabisa so sijaka kulia njaa kama ulivyofikiri wewe
 
mkuu umewahi kufika zenji? Jee unayajua maghorofa ya michenzani? yale majengo yana ghorofa tano, yamejengwa zaidi ya miaka 40 iliyopita na hayakutumia hata nguzo moja. yote yamejengwa kwa kulaza tofa, pia kuna jengo jengine liko mtendeni lina ghorofa nne nalo pia halikutumia nguzo bali tofali tu zimelazwa. hivyo kwa kagorofa kamoja we laza tu tofali
 
Vipi kuhusu ujenzi wa ghorofa moja kwa kutumia tofali za kuchoma hasa mkoa wa Morogoro?ushauri wenu wakuu
 
mkuu tatizo letu sisi watz tunafuata mkumbo tu yaani wote tukiona magorofa yanajegwa kwa nguzo za nondo nzito tunafuata hivyo hivyo ukienda vijijini utakuta kuna gorofa nzuri tu watu wanajenga kwa matofali ya kuchoma kwa mtiririko ufuatao msingi imara wa mawe na saa nyingine kwa mortar ya udongo mwekundu halafu ground floor ya matofali ya kuchoma yanayowekwa mawili mawili na floor ya juu ya tofali moja na sakafu ya mbao kutenganisha, hizo nyumba nyingine zina zaidi ya miaka 100 na ni imara tu
 
mkuu tatizo letu sisi watz tunafuata mkumbo tu yaani wote tukiona magorofa yanajegwa kwa nguzo za nondo nzito tunafuata hivyo hivyo ukienda vijijini utakuta kuna gorofa nzuri tu watu wanajenga kwa matofali ya kuchoma kwa mtiririko ufuatao msingi imara wa mawe na saa nyingine kwa mortar ya udongo mwekundu halafu ground flow ya matofali ya kuchoma yanayowekwa mawili mawili na flow ya juu ya tofali moja na sakafu ya mbao kutenganisha, hizo nyumba nyingine zina zaidi ya miaka 100 na ni imara tu

mkuu umenifaa sana kwa ushauri wako huu, manake hapo pekundu pananiumizaga sana kichwa nikifikiriaga kujenga kighorofa cha kuishi. Kama una ushauri zaidi wa jinsi ya kupunguza gharama za ground floor mwaga tunufaike zaidi mkuu
 
Mkuu mito,
Anza mdogomdogo tu mpaka utafika. If you can do it once then you can do it again. Kama unaweza kujenga ya chini then unaweza kujenga ghorofa, tofauti itakuwa muda wa kumaliza tu...
 
Mkuu mito,
Anza mdogomdogo tu mpaka utafika. If you can do it once then you can do it again. Kama unaweza kujenga ya chini then unaweza kujenga ghorofa, tofauti itakuwa muda wa kumaliza tu...

aaaha umenishauri kinadharia zaidi mkuu, yaani gharama za kujenga nyumba ya chini utalinganisha na za ghorofa mkuu, loh!
 
Faida za nguzo/columns.

1.zinapokea uzito kutoka kwenye beams na kupeleka mzigo/uzito ardhini.

2.zinazuia nyumba dhidi ya upepo mkali zikisaidiwa na beam/ringbeam.
(resistance of lateral forces due to wind or very heavy convectional rainfall).

3.zinashirikiana na ground beams kulifunga jengo na hivyo kupelekea
nyufa na matatizo mengine yatokanayo na tabia za udongo/tetemeko n.k
kuthibitiwa.

4.Kutumia nguzo katika jengo ni bora zaidi kwani ulifanya jengo
liwe kama limekamatwa ardhini na foundation bases tofauti na
kutumia tofari.

5.Vilevile tunavyotumia nguzo tunazidi kulidumisha jengo
kwa muda mrefu kwani ndani ya nguzo ni lazima pawekwe
nondo kwa hesabu maalum za kitaalamu tofauti na tofari.

Hivyo basi ni bora ukatumia ujenzi wenye kutumia zege na
nondo zaidi kuliko ule wenye kutumia cement na mchanga
pekee katika ujenzi wako.
 
Mkuu mito,
Anza mdogomdogo tu mpaka utafika. If you can do it once then you can do it again. Kama unaweza kujenga ya chini then unaweza kujenga ghorofa, tofauti itakuwa muda wa kumaliza tu...

Umemshauri vizuri sana. Nimeupenda ushauri wako.
 
Sijui kama haka kanakula tumilioni tungapi.... AMAFUMU ?

House-Exterior-3D-Model2.jpg
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom