Naangalia option kujaribu kujenga kighorofa kimoja japo nilale juu, fundi ameniambia nichague kati ya option mbili
- kulaza matofali
- kutumia nguzo
Namaanisha kama nikilaza matofali floor slab ya juu itakua supported na hayo matofali bila nguzo. Kama nikiopt nguzo nitasimamisha matofali kawaida, niko tutani naombeni ushauri wataalamu ujenzi nitaanza soon ndio nafanya site clearance na kukusanya vifaa. Niko jijini
Sio rahisi sana kutoa ushauri hapa kuhusu jambo hili. Kwanza huyo "fundi" unayemzungumzia ni "Architect" au "Structural Engineer" (ama ni "Mason" tu)? Hao wawili kama walihusika katika kusanifu jengo hilo basi unahitaji ushauri wao.
Uamuzi wa kutumia nguzo ama la unaweza kuwa ni structural au unaweza kuwa achitectural (or both!). Kwa hivyo, hao watu wawili ni lazima upate ushauri wao kwa sababu wao ndio wanalijua jengo lango linavyotakiwa kuwa na pia wanaijua site yako (na zaidi wanao wajibu wa kitaaluma/kitaalamu). Kama kwa sababu moja ama nyingine hukuwatumia wataalamu hawa katika kusanifu jengo lako,basi ushauri wangu ni kuwa fuata mchoro kama ulivyo (usifanye mabadiliko, unless mmoja wapo wa wataalamu hao ametizama (review) kazi yako na kukushauri/kuafiki mabadiliko hayo). Kama hata mchoro huna, basi hiyo ni "shughuli" nyingine tena!
Tukizungumzia nguzo, watu wengi wanafikiri zaidi zege na nondo! Wanasahau kuwa nguzo inaweza pia kujengwa kwa hayohayo matofali kutegemeana na aina ya mzigo au forces inayozatamiwa kukabiliana nazo na pia muonekano unaotegemewa.
Kwa ujumla uamuzi wa suala lako unahitaji kuzingatia pamoja na yafuatayo:
(a) Site - aina ya udongo na uwezo wake (bearing capacity)
(b) Aina na kiwango ya mzigo unaokusudiwa kubebwa (dead loads, live loads)
(c) Kiwango na ukuwa wa matofali unaotegemea kutumia (6", 5" etc, ya mkono/ya machine, mangapi kwa mfuko wa cement - kuna matofali unaweweza kukwaruza kwa vidole tu unaona linapukuchika!)
(d) Muonekano uanotegemewa - Wakati mwingine nguzo zinaongeza "ladha" ya jengo!
(e) Flexibility (nimeona wadau kadhaa wameligusia hili)
(f) Ukubwa/upana wa vyumba (spans) - kama ni span kubwa kuna uwezekano wa kuwa na tensile stress kubwa kwenye vertical members. Matofali hayawezi kuhimili tensile stress.
Kwa hayo machache, unaweza kuona umuhimu wa kuongea kwanza na wataalamu wako kabla hujafanya mabadiliko.
Nakutakia mafanikio mkuu.