Henge
JF-Expert Member
- May 14, 2009
- 6,933
- 1,511
Vipi kuhusu ujenzi wa ghorofa moja kwa kutumia tofali za kuchoma hasa mkoa wa Morogoro?ushauri wenu wakuu
mkuu hii ni mpaka nguzo za zege huwezi kujenga bila nguzo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipi kuhusu ujenzi wa ghorofa moja kwa kutumia tofali za kuchoma hasa mkoa wa Morogoro?ushauri wenu wakuu
Idorome, Mimi pia ni Architect,
Fundi wako yupo sahihii, msikilize, ila zingatia ubora wa udongo hapo unapojenga hiyo nyumba yako.
Nyumba ya ghorofa moja haiitaji nguzo, ni kwa kufuata kasumba watu hujenga nyumba na nguzo, unaweza kujenga ghorofa moja bila nguzo, binafsi nimejenga ghorofa kadhaa hapa mjini (including yangu) bila nguzo na hazina tatizo hata kidogo,
Zingatio
Hakikisha tofari zinakuwa imara kama unachukua option 1. na kama hauamini tofati zako basi ni bora ukachukua option 2.
Ningejua unajenga wapi ningekueleza matofari mazuri yalipo.
spacarchitects@gmail.com
Idorome, Mimi pia ni Architect,
Fundi wako yupo sahihii, msikilize, ila zingatia ubora wa udongo hapo unapojenga hiyo nyumba yako.
Nyumba ya ghorofa moja haiitaji nguzo, ni kwa kufuata kasumba watu hujenga nyumba na nguzo, unaweza kujenga ghorofa moja bila nguzo, binafsi nimejenga ghorofa kadhaa hapa mjini (including yangu) bila nguzo na hazina tatizo hata kidogo,
Zingatio
Hakikisha tofari zinakuwa imara kama unachukua option 1. na kama hauamini tofati zako basi ni bora ukachukua option 2.
Ningejua unajenga wapi ningekueleza matofari mazuri yalipo.
spacarchitects@gmail.com
mkuu hii ni mpaka nguzo za zege huwezi kujenga bila nguzo
Mkuu kwa hilo ghorofa la 144sqm, ulitumia tofali kama ngapi kwenye msingi tu?Zemacopolo hili gorofa lina ukubwa gani?
Linapokuja swala la slab kusema kwelie size matters yaani kama unataka mambo ya sqrm 180 basi andaa mfuko wa kutosha kwani kushona mkeka wa jamvi pale panalika sana nondo za 12mm na hazikimbiliki zitalika tuu. Mimi nimejenga 144sqrm na hapo zimelika nondo za kutosha.
Nimesema hapo awali kama una forecast ya cash ya kama 20 million per phase basi gorofa unaweza kujenga. Maana msingi wa gorofa utakula kuanzia 20 million kisha kujenga mpaka kwenye slab haifiki hata 8 million, then slab at least 25 million then unapandisha kwa at least 8 million then kufunika add another 15 million. hapo kama 70 million inakuwa imesimama. Baada ya hapo tukutane kwenye finishing.
Ukijipanga unaweza kaka. Nimimi nimethubut na nasema yoyote anaweza akijipanga.
Mkuu jee foundation yake inatumia nondo? Au pia saruji tumkuu umewahi kufika zenji? Jee unayajua maghorofa ya michenzani? yale majengo yana ghorofa tano, yamejengwa zaidi ya miaka 40 iliyopita na hayakutumia hata nguzo moja. yote yamejengwa kwa kulaza tofa, pia kuna jengo jengine liko mtendeni lina ghorofa nne nalo pia halikutumia nguzo bali tofali tu zimelazwa. hivyo kwa kagorofa kamoja we laza tu tofali
MkuuKiongozi,
Mimi niko Dar es Salaam, Kibada.
Hapo kwa mahesabu ya harakaharaka unahitaji:
Mirunda 120
Marine boards 27
Cement mifuko 65
Mchanga lori 7ton trip 2
Kokoto lori 7ton trip 3
Nondo mm12 pcs180
Nondo mm8 pcs 40
Nondo mm16 pcs 36
Mbao 2X6 pcs pcs 40
Mbao 2X2 pcs 15
Mbao 2X4 pcs 10
Ufundi - maelewano ( kusuka nondo sh. laki 2. kupiga mbao laki 2, fundi laki 2, kumwaga zege laki 2 jumla laki 8)
Jumlisha na vikorokocho vingine kama misumari etc ambavyo bei yake sio deciding factor.
Kadirio la kati jumla ni sh. mil. 8.
Gharama hii inaweza kupungua kwa kiasi kikubwa iwapo vitatumika vifaa vya kukodi au used.
Unaweza kukodi mkuuNaomba kujua gharama za vile vibao vinavyowekwa kwenye ujenzi wa maghorofa,na je usipoweka nini madhara yake
Nadhani anaongelea vibao vya mradi...Unaweza kukodi mkuu
Hii project ulishaimaliza....Naangalia option kujaribu kujenga kighorofa kimoja japo nilale juu, fundi ameniambia nichague kati ya option mbili
Namaanisha kama nikilaza matofali floor slab ya juu itakua supported na hayo matofali bila nguzo. Kama nikiopt nguzo nitasimamisha matofali kawaida, niko tutani naombeni ushauri wataalamu ujenzi nitaanza soon ndio nafanya site clearance na kukusanya vifaa. Niko jijini
- kulaza matofali
- kutumia nguzo
Si ghorofa tu hata nyumba za kawaida ni bora kujenga kwa kutumia nguzo. Kuna wakati nyumba unaikuta ipo chini na barabara ipo juu, hivyo ni rahisi kuipandisha kama ina Nguzo. Uimara wa nyumba ni muhimu sana. Katika ujenzi kumbuka kuwa masikini ndiye hujenga nyumba na wala si tajiri kwani mdogomdogo huimarisha nyumba kuliko kujenga fasta.Faida za nguzo/columns.
1.zinapokea uzito kutoka kwenye beams na kupeleka mzigo/uzito ardhini.
2.zinazuia nyumba dhidi ya upepo mkali zikisaidiwa na beam/ringbeam.
(resistance of lateral forces due to wind or very heavy convectional rainfall).
3.zinashirikiana na ground beams kulifunga jengo na hivyo kupelekea
nyufa na matatizo mengine yatokanayo na tabia za udongo/tetemeko n.k
kuthibitiwa.
4.Kutumia nguzo katika jengo ni bora zaidi kwani ulifanya jengo
liwe kama limekamatwa ardhini na foundation bases tofauti na
kutumia tofari.
5.Vilevile tunavyotumia nguzo tunazidi kulidumisha jengo
kwa muda mrefu kwani ndani ya nguzo ni lazima pawekwe
nondo kwa hesabu maalum za kitaalamu tofauti na tofari.
Hivyo basi ni bora ukatumia ujenzi wenye kutumia zege na
nondo zaidi kuliko ule wenye kutumia cement na mchanga
pekee katika ujenzi wako.
Complications,Si ghorofa tu hata nyumba za kawaida ni bora kujenga kwa kutumia nguzo. Kuna wakati nyumba unaikuta ipo chini na barabara ipo juu, hivyo ni rahisi kuipandisha kama ina Nguzo. Uimara wa nyumba ni muhimu sana. Katika ujenzi kumbuka kuwa masikini ndiye hujenga nyumba na wala si tajiri kwani mdogomdogo huimarisha nyumba kuliko kujenga fasta.
Siimanishi za barazani nazungumzia za kwenye kona ili ziunganike na renta. Siyo Complications mkuu ila ni kuimarisha nyumba ili kireki zisikunyime usingiziComplications,
Nyumba ni ya chini, hizo nguzo za kazi gani??
Au unamaanisha zile zinazokaa pale barazani??
Renta ni kodi au? linter semaSiimanishi za barazani nazungumzia za kwenye kona ili ziunganike na renta. Siyo Complications mkuu ila ni kuimarisha nyumba ili kireki zisikunyime usingizi
lintel kwa kizungu au Renta kwa kiswahiliRenta ni kodi au? linter sema