Ujenzi wa ghorofa: Nimeshaleta kifusi cha kwanza

wakuu kuna watu naona wanatumia izi kokoto nyepesi maarufu kama za kokoto za ubuyu kwenye ujenzi wa gorofa. izi usalama wake ukoje nazo?zinafaa kutumika?
Za ubuyu ghorofa? Sidhan kama zipo recommended kitaalam, japo kama ulivyosema watu wanazitumia sana tu kujengea, unajua ujenzi kiviwango uko hivi nyumba iliyojengwa kwa kuzingatia viwango na ambayo haikujengwa kiviwango tofauti hutoiona leo ila baada ya muda kupita, au kukitokea let say tetemeko ndo utaona tofauti zake. Ndo maana kuna maghorofa yamejengwa miaka mitatu iliyopita leo hii slab inabanduka banduka, au unakuta zile slab zinazotumika kuweka taa unakuta zinameguka zenyewe.
Kiukweli ukitaka kujenga ghorofa na bajeti yako ipo tight tumia wataalamu watakuguide sehemu za kupunguza gharama, watakushauri materia ambayo sio ghali sana n.k
 
Mkuu unavyoandika ina maaha kuna watu wanajenga kwa siku moja??Hivyo vitu vyote umesema hapo unaweza kuvifanya ndani ya miaka 3 au 4 pole pole hatua kwa hatua
 
Mh hilo jengo ni kwa matumizi gani...na ni ghorofa ngapi?

Mfano wake ni kama huu. Ni residential
Hebu nishauri mkuu; Jengo linalofanana na hili;
✅Column nondo ngapi na mm ngapi
✅Msingi mita ngapi. Je, kimo cha msingi ni lazima kiwe sawa kwa pande zote za jengo? Au upande wa kulia inaweza mfupi zaidi ya kushoto?
✅Kama ni msingi wa tofali, ratio iweje? tofali 25 kwa mfuko inatosha?
 
View attachment 3075312
Mfano wake ni kama huu. Ni residential
Hebu nishauri mkuu, jengo linalofanana na hili column nondo ngapi na mm ngapi, msingi mita ngapi, kama ni msingi wa tofali, ratio iweje? tofali 25 kwa mfuko inatosha?
Mh ok sawa yeye ndo mtaalam ila alikupa sababu why atumie nondo 6 za 16 kwa column?
 
Mh ok sawa yeye ndo mtaalam ila alikupa sababu why atumie nondo 6 za 16 kwa column?
Hapana hakunipa, ilikuwa ni mazungumzo ya awali tu.

Hebu nishauri mkuu; Jengo linalofanana na hili;
✅Column nondo ngapi na mm ngapi
✅Msingi mita ngapi. Je, kimo cha msingi ni lazima kiwe sawa kwa pande zote za jengo? Au upande wa kulia inaweza mfupi zaidi ya kushoto?
✅Kama ni msingi wa tofali, ratio iweje? tofali 25 kwa mfuko inatosha?
Ardhi ni tambalale na udongo wa mfinyanzi
 
Inategemea na aina ya udongo.
 
Mimi sio mtaalam wa ujenzi japo nina ideas ila nimeona umesema udongo ni mfinyanzi, kwa udongo huu Engineer anaweza kuwa sawa, na ni vizuri sana ukatumia mtaalam wa ujenzi mwenye uzoefu wa kutosha.
 
Umekua baba levo fundi majumba unatoa taalifa za ujenzi wa nyumba yako ambayo unajenga kwa faida yako na mke na familia
Ushauri wa bure iyo gorofa andika jina la mama yako sku izi wanawake hawaeleweki unaweza maliza kujenga afu mkajikuta mnagawana flow
 
Alizingatie hili
 
Hatua ya kwanza kwanza ya ujenzi wa Ghorofa ni kuondoa vifusi wakati wanachimba msingi ...kumbuka msingi wa Ghorofa unaenda chini kama Shimo
 
Mpaka hapo hujengi chochote wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…