Ujenzi wa Nyumba: Je, ninaweza kujenga kanyumba kadogo kazuri kwa bajeti ya Mil. 6!?

Kama ni Dar huwezi. Sijui kama inatosha kujenga septic tank mbili peke yake!
 
Matofali 1000@1000= 1000000
Cement mifuko 15@15000=225000
Nondo 7@16000=112000
Mabati12@17000=204000
Milango 4@ 250000=1000000
Madirisha 5@ 350,000=1750000
Ufundi mwashi= 1200000
Jumla = 5599000
Hapo sijaweka gharama ya kuchimba choo. Mbao. Fundi wa kupau. Mchanga na maji
 
Vp kuhusu mchanga, kokoto, maji, ulinzi, kifusi, mifuko 15 haitoshi kujenga idadi ya tofali ulizoweka, vip kupaua atapaua mwenyewe? Tena bila mbao wala misumari?
Msimpotoshe jamaa.

Kama anataka chumba na sebule choo passport size sawa ila kwa nyumba kama nyumba kwa 6m bado.
 
oh asante kaka nilidhani ni milion 55 na kumbe ni milion 5 na asante kwa kunionesha kuwa inawezekana
 
kaka yaani ngoja nijaribu, yah niko maeneo ya arusha lakini ni kijijini ndani huku arumeru magharibi juu ya forest
 
asante kaka itabidi basi nianze hivyo hivyo mpaka kielelewe ....ilimradi kama nyumba itafika nakuezeka basi poa mengine itabid yaendelee badae
 
kaka yaani ngoja nijaribu, yah niko maeneo ya arusha lakini ni kijijini ndani huku arumeru magharibi juu ya forest
Kwa vyumba viwili inawezekana bhana, usiogope, ukiishia njiani ndio mwanzo wa kupata akili nyingine. Utakatishwa tamaa hapa mwisho utaishia "kuitumia Guest" hio amount au atakuja mtu hapa akutapeli
 
asante Dori, tofali za kuchoma kwa kweli mimi ninazipenda hasa ukijenga kwa kuzichora nyumba inakuwa poa inaondoa gharama zakufanya finishing kwa nje
 
Kuna kajumba nimejenga kijijini kwa pesa hiyo yaani kapo vizuri sana ningelikuwa mjini nakauza mil 30.
 
Huwezi(kama upo dar)

Labds tofali za kuchoma

Mkuu, tujenzi kwa kutumia tofali za kuchoma labda mikoani , tena kwenye miji midogo, kwenye miji mikubwa ujenzi kwa kutumia matofali ya kuchoma ni gharama zaidi. BTW tofali za kuchoma Dar zinapatikana wapi?
 
kaka yaani ngoja nijaribu, yah niko maeneo ya arusha lakini ni kijijini ndani huku arumeru magharibi juu ya forest

Kiding'a, Olmotonyi, sambasha, Nambere, Sasi, Mareu,Muklati, ............................??????? Chagua jibu, nkupe maujuzi......
 
maeneo ya arusha, wilaya ya arumeru magharibi
Huko ndio tabu kabisa mchanga ni ghali sana, nakushauri uanze na hizo hutamaliza lakin utafika mahali flan baadae utamalizia.

Duc In Altum.
 
Unaweza kujenga bedroom, sebule, jiko, choo nzuri. Hela inatosha. Kama vp npm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…