Ujenzi wa Nyumba: Je, ninaweza kujenga kanyumba kadogo kazuri kwa bajeti ya Mil. 6!?

Ujenzi wa Nyumba: Je, ninaweza kujenga kanyumba kadogo kazuri kwa bajeti ya Mil. 6!?

Matofali 1000@1000= 1000000
Cement mifuko 15@15000=225000
Nondo 7@16000=112000
Mabati12@17000=204000
Milango 4@ 250000=1000000
Madirisha 5@ 350,000=1750000
Ufundi mwashi= 1200000
Jumla = 5599000
Hapo sijaweka gharama ya kuchimba choo. Mbao. Fundi wa kupau. Mchanga na maji
Madirisha anaweza kuweka ya kawaida ya 120k au 150k.
Cement 15@13500
Mabati aende kiwandan bundle moja la 28grade 240000 pale tazara zinakuwa 12/14.
 
Wadau, mafundi ujenzi, ninaomba msaada, ninayo ardhi kubwa sana, ila nimechoka kupanga na headaches za landlord. Nimejibana nikakuta nina milioni 6, je ninaweza kujenga ka nyumba kadogo
kenye atleast two bedrooms sebule ka jiko n.k. yaani niweze kujenga kumaliza kwa bei hiyo!?,

Asanteni!?
.......INAWEZEKANA.........ILA INATEGEMEA NA MAENEO ULIYOPO.......
 
Mmmh! Mkulu kama ni Dar jipange tena! Ujenzi si kitu kidogo unaweza kupata ka heart attack khaa!
 
Kuna watu unawaskia kwenye media, magazeti mtu kajenga jumba la bilion 2 halafu nakuja hapa nakutana na mtu anajenga nyumba ya Milion 6! Ya bilion 2 ni hela ya mvuja jasho ya mlipa kodi! Wenye utajiri ifike mahali huo utajiri kama si halali wafilisiwe! Bora ile sayari ya Nibiru igonge dunia tujue moja Wote twende sana! Maana hamna namna tena
 
Ukisema nyumba ndogo unakosea,ungesema nyumba ndogo ya vyumba vingapi?kwanza inategemea na aina ya tofali unazotaka kutumia,za kuchoma au za cement,pili utafyatua mwenyewe au utanunua,je unataka msingi uwe wa mawe au tofali,je unataka ramani gani,sloop mgongo wa tembo au hizi za kisasa,nyumba iwe na choo ndani,sisytem ya maji masafi na machafu iweje,finishing gymsam au silibord,unapiga plasta,utaweke drill madirishani,utaweke dirisha la mbao au alminium.kiujumla hiyo hera ndogo
 
Kuna watu unawaskia kwenye media, magazeti mtu kajenga jumba la bilion 2 halafu nakuja hapa nakutana na mtu anajenga nyumba ya Milion 6! Bora ile sayari ya Nibiru igonge dunia tujue moja! Maana hamna namna tena
Hahahahaaaaa dah hasira sana mkuu [emoji12]
 
Kanyumba kadogo unaweza sana lakini "KAZURI" hutoweza inabidi ujipange tena.
 
Nitafte kupitia 0765394329 nikupatie ramani ya kanyumba ka hvo afu ukatathmini
 
kama uchagui chakula jenga mabanda ya Noah baada ya mwaka utakuwa na Nyumba ya maana
 
Huku Namtumbo unajenga,
Mvua zikikata unafytua Tofali za udongo.
Toka kufyatua hadi kuchoma ni 60Tsh.
Bati za msouth bando moja ni 19000 na zinakaa 10
Cement kwa ajili ya sakafu mfuko mmoja ni 16000
Labour charge ni low kwa huku.

Boriti ni 7500
So unaweza kukadiria ukubwa wa kimjengo chako


weee! Bati la msouth bando moja ni 19,000? na zinakaa 10? cheki vizuri hizo data zako za bei then uniambie nije ninunue huko, maana nimejenga nyumba hapa Mwanza, vyumba 3, sebule, dining na jiko, na vyumba vyote ni self, ila Napata mawazo sana juu ya bei ya Mabati ya msouth kwa hapa mwanza, ipo juu sana,
 
weee! Bati la msouth bando moja ni 19,000? na zinakaa 10? cheki vizuri hizo data zako za bei then uniambie nije ninunue huko, maana nimejenga nyumba hapa Mwanza, vyumba 3, sebule, dining na jiko, na vyumba vyote ni self, ila Napata mawazo sana juu ya bei ya Mabati ya msouth kwa hapa mwanza, ipo juu sana,
Doh sifuri more moja imekosekana
 
Labda uwe na building materials zote zinazohusika hapo chini hiyo ikusaidie km labor charge.
 
nyumba simple, mgongo wa tembo. sitting room ktkt bedrm kulia, kitchen kushoto. yaan iwe nyumba ya nyuma. kwa maana kwamba kubwa itajengwa baadae kwa mbele. choo cha muda nje.
 
k
tofali 1m
mbao mnazi 5k
bati 1m
milango 1m
madirisha 5k
fundi kujenga 6k
fundi bati 4k
mawe 4k
cement 6k

ongeza 3 unajenga nyumba ya vyumba 2 sebure choo na jiko kijijini kwetu.
how much is K..navyofahamu K means * 1000
 
we anza hiyo helà ni nzuri kuanzia nyumba siyo had uwe na cash ya kumaliza.
 
Back
Top Bottom